REPORT UN:WATANZANI NI MIONGONI MWA WATU WASIO NA FURAHA NA WALIO KATA TAMAA DUNIANI


Wakati Tanzania ikitajwa kuwa ni miongoni mwa nchi zenye amani na utulivu, imebainika kuwa Watanzania ni miongoni mwa watu wasio na furaha na waliokata tamaa hapa duniani.

Ripoti inayoonyesha orodha ya nchi zenye furaha duniani ya mwaka 2013 (World Happiness Report 2013), imeitaja Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi 10 za mwisho duniani kati ya nchi 156 zilizofanyiwa utafiti huo.

Ripoti hiyo iliyoandaliwa na kundi la wataalamu kutoka Umoja wa Mataifa (UN), kati ya mwaka 2010 na 2012, inaonyesha kuwa Tanzania imeshika nafasi ya 151 ikiburuta mkia pamoja na nchi za Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Benin na Togo.

Upatikanaji wa huduma za jamii, mtazamo wa watu kuhusu rushwa, umri wa kuishi, ukosefu wa kazi, pato la taifa na ukarimu wa watu katika nchi husika, ni baadhi ya vigezo vilivyoangaliwa wakati wa kuandaa taarifa hiyo.

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka alieleza kushtushwa na ripoti hiyo kwa maelezo kwamba ni asilimia 11.7 tu ya Watanzania wasio na ajira na kwamba wale wanaofanya kazi, wanapata huduma zote za msingi, ikiwa ni pamoja na kwenda likizo na mishahara inayolingana na taaluma zao.

“Watanzania wana furaha, kwa upande wa wafanyakazi wanapata haki zao zote wanazostahili, sijui ni vigezo vipi wametumia…kwa mujibu wa takwimu za 2006 ni asilimia 11.7 ya Watanzania ndio waliokuwa hawana kazi, lakini wakati huo idadi ya watu ilikuwa ndogo, hivi sasa imeongezeka,” alisema Kabaka na kuongeza:“Usafiri ndiyo tatizo linalowasumbua wafanyakazi wengi kwa kuwa wanachelewa kwenda kazini.”

Naye, Naibu Waziri wa Fedha, Saada Salum alisema pamoja na vigezo vingine vilivyotumika kutambua furaha ya Watanzania, umaskini ndiyo unaoweza kuwa chanzo cha Tanzania kushika nafasi za mwisho.

“Inategemea na vigezo vingine walivyovitumia, nakubali kuwa Tanzania ni maskini pengine hali hiyo imeifanya nchi kushika nafasi ya mwisho,” alisema Salum.

Nchi zilizoongoza

Taarifa hiyo imezitaja nchi tano; Denmark, Norway, Uswisi, Netherlands na Sweden kuwa ndizo zinazoongoza kwa watu wake kuwa na furaha zaidi duniani, huku Angola ikishika nafasi ya kwanza Afrika na ya 61 duniani ikifuatiwa na Algeria (73), Libya (78), Ghana (86), Zambia (91), Lesotho (98), Morocco (99) na Swaziland (100).

Kwa upande wa Afrika Mashariki, wananchi wa Uganda ndio walionekana kuwa na furaha zaidi kwani nchi hiyo imeshika nafasi ya 120 wakifuatiwa na Kenya (123), Tanzania (151), Rwanda (152) na Burundi (153).


Ripoti hiyo inabainisha kuwa kati ya mwaka 2005 na 2012, nchi 60 duniani ziliongeza viwango vya furaha kwa watu wake, kati ya hizo 16 zikiwa barani Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara.

-Mwananchi
Udaku Specially Blog
Tags

Post a Comment

15 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hii ripoti iko sahihi kabisa. watu wanapozidi kunywa pombe ujue wana msongo wa mawazo. ajira hakuna wizi umezidi.

    ReplyDelete
  2. Mawaziri wetu wanafiki hawa eti 'wenye ajira wanapata huduma zote' shame on you.kwa mshahara wa laki 2 mtu ataishi vip?anakodi, chakula cha familia, masomo ya watoto na mengine.afu unategemea wawe na furaha kwa lipi?hizi takwimu ni za kweli na wala sio za kupika, nimeishi Sweden na uholanzi na nimejionea

    ReplyDelete
    Replies
    1. Usitegemee serikali utakuwa na furaha .serikali sio soln

      Delete
    2. Siyo mwajiriwa wa serikali lakini jaribu kufuatilia mishahara ya serikali kama south Africa, Botswana, hata zimbambwe ulinganishe na tz ni majanga.wanasiasa ni wabinafsi sana leo hii tunasikia waziri mkuu anakunja mil 26, mwalimu akiambulia lak 2

      Delete
  3. Watu wamejaa ubinafsi. Rushwa kila sehemu. Utu hakuna. Viongozi wetu badala ya kutusaidia wanatukandamiza. Watu ni madili tu hakuna cha haki. Hapo furaha itatoka wapi? Ni vilio tu.

    ReplyDelete
  4. Kazi hakuna maisha magumu furaha itoke wapi kujiajiri mitaji hakuna wacha tufe na stress na kutukanana kwenye mablog

    ReplyDelete
  5. Hatuna furaha kweli,unashtuka nini wewe mwanamke mrs kabaka?mnaishi kwa raha nyie na familia zenu,na bado mkatambike uchi makaburin labda mwaka 2015 mapinduzi lazima..machief nanga wakubwa nyieee.

    ReplyDelete
  6. Ni kweli Watanzania hawana raha wagomvi,umbea,kukatisha Watu tamaa.Uchawi uvivu

    ReplyDelete
  7. bongo watu SHANGWE tu mbona, hao watu wa UN waje hapa Rose Garden jioni leo jumamosi;

    ReplyDelete
  8. Wewe fisadi na mafisadi wenzako ndiyo mna uwezo wa kukaa hapo Rose Garden. Majizi

    ReplyDelete
  9. Ndio hizo pombe za rose garden zinazokufariji kwa mda. Lala uamke kesho utaanza kumbuka umetumia sh ngapi kulewa pombe ili utoe stress, sana unajiua kidogo kidogo na vihela vya mcmu. Na hapo ulipo pombe zipo kichwa. Wizi mtupu!

    ReplyDelete
  10. Ms. G. Kabaka may be sio mTanzania kama jina lako la ubini linavyoonyesha. Umaskini ambao unasababishwa na siasa chafu na chama kilichojisahau, kwani viongozi wanaishi maisha tofauti na ya kibepari! Watawakumbukaje wananchi? Wanachotaka kutoka kwao KURA tu.

    ReplyDelete
  11. Hata waliajiliwa mishahara yao alingani na kipato hali cha mtanzania hatuwezi kuwa na furaha hata siku moja, uangalia viongozi hawajali hilo wala kulitambua hilo.

    ReplyDelete
  12. hivi watanzania watakua na furaha kwa lipi kodi ndio hizo zinazidi kuongezwa kwa walala hoi ili tuwanufaishe wakubwa ambao ndio hao wanapata mishahara mikumwa bila wao kukatwa kodi jamani serikali tunaomba mtuache nasisi tupumue nyie mishahara ni mikubwa kodi hamkatwi hamuoni hata haya mkikaa hapo bungeni kwenu nakutuwazia sisi walalahoi kuwa leo mtumie mbinu gani zakutuchukulia hata hiki kidogo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad