TEAM YA MPIRA WA MIGUU YA WANAWAKE TANZANIA YAICHAPA MSUMBIJI 10 BILA

Dar es Salaam. Timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania kwa vijana chini ya miaka 20 imeanza vizuri kampeni zake za kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2014 kwa vijana chini ya miaka 20 baada ya kuichapa Msumbiji 10-0 katika mechi iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Vijana hao wa Tanzania waliianza mechi hiyo kwa kasi, ambapo katika dakika ya 6 walipata bao la kwanza lililofungwa na Neema Paul baada ya kupata pasi ya Therese Yona.

Mfungaji wa bora wa mashindano ya Airtel Rising Stars yaliyofanyika

Nigeria mwaka huu, Shelder Boniface aliiandikia Tanzania bao la pili katika dakika ya 24.

Kama hiyo haitoshi, vijana wa Tanzania walizidi kulisakama lango la Msumbiji, ambapo katika dakika ya 32 Tanzania ilipata bao la tatu ambalo lilifungwa na Deonisia Daniel kwa mpira wa faulo uliokwenda moja kwa moja nyavuni.

Katika dakika ya 41 vijana wa Tanzania ambao waliibuka mabingwa kwa upande wa wanawake katika mashindano ya Airtel Rising Stars yaliyofanyika Nigeria walipata bao la nne ambalo lilifungwa na Amina Ali kwa shuti kali akiwa nje ya 18.

Vijana hao wa Tanzania walifunga bao katika dakika ya 45, lakini likakataliwa na hivyo kwenda mapumziko ikiongoza 4-0.

Kipindi cha pili Tanzania ilianza kwa kasi tena na kupata bao la tano katika dakika ya 47 ambalo lilifungwa na Neema Paul baada ya kuunganisha kwa kichwa krosi ya Therese Yona.

Tanzania ilipata bao la sita ambalo lilifungwa na Shelder Boniface baada ya kumalizia mpira uliotemwa na kipa wa Msumbiji kutokana na shuti la Stumai Abdallah.

Dakika ya 82, Tanzania iliandika bao la saba lililofungwa na Amina Ali kwa shuti kali, pia dakika 86 Tanzania iliandika bao la nane kwa mkwaju wa penalti iliyofungwa na Deonisia Daniel baada ya Shelder kuangushwa katika eneo la hatari.


Vijana hao wa Tanzania hawakutosheka na ushindi kwani katika dakika ya 89 walipata bao la tisa lililofungwa na Amina Ali, pia katika dakika ya 90 walifunga bao la 10 lililofungwa na Stumai Abdallah.

Udaku Specially Blog
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad