TFF YAMUOMBA RADHI TAMBWE...BAADA YA KUMYIMA MPIRA WA ZAWADI ..YEYE AKATAA

Lucy Mgina na Martha Mboma
BAADA ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kudai limemuomba radhi mshambuliaji wa kimataifa wa Simba, Amissi Tambwe, raia wa Burundi, straika huyo ameibuka na kudai ni uongo.
Tambwe alifunga mabao manne katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mgambo JKT Septemba 18, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar na kunyimwa mpira kama zawadi baada ya mechi kumalizika.
Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, alisema wamemuomba radhi straika huyo kutokana na kutopewa mpira huo licha ya kuwa suala hilo halipo kwenye sheria za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Alisema waliamua kumuomba radhi kama ‘fair play’ lakini walimtaarifu aufuate katika ofisi za shirikisho hilo, pia mwamuzi aliyemnyima mpira huo hawezi kuadhibiwa.
“Tulimuomba radhi kutokana na tukio lile na tulimtaka aje kuchukua mpira wake, nafikiri atakuwa anajipanga ili aje kuchukua siku yoyote,” alisema Wambura.
Championi lilienda mbele na kumtafuta straika huyo anayeongoza kwa kufunga mabao kwenye ligi kuu kwa sasa akiwa ameshatupia nane wavuni ambapo alidai hajafuatwa na mtu yeyote kuhusiana na suala la kupewa mpira na hafikirii tena suala hilo.
“Sijafuatwa na mtu yeyote na wala sina wazo lolote kuhusiana na ishu hiyo ya mpira na kama wataamua wenyewe kuniletea au wakiukabidhi kwa viongozi wangu sawa tu nitauchukua,” alisema Tambwe na kuongeza:

“Naumwa malaria tangu jana (juzi) na sijafanya mazoezi yoyote kwa kuwa mwili unaniuma sana.”  

Udaku Specially Blog
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad