ZITTO KABWE"SIJAMUOA MTOTO WA KIKWETE..SIPO BUNGENI KUPIGANA NGUMI"

Naibu katibu mkuu wa chadema taifa Zitto Kabwe akiwahutubia wananchi wa Mji wa Mpanda katika viwanja vya maridadi hapo jana ambapo alikanusha uvumi ulionea kuwa amekuwa kimya na amepunguza makali yake bungeni kwa sababu amemuoa mtoto wa Raisi kikwete alikana kumuoa mtoto wa kikwete
Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi yetu Blog

Naibu katibu mkuu wa Taifa wa CHADEMA Zito Kabwe amekanusha uvumi ulioenea wa kuwa amemuowa mtoto wa Rais Kikwete na ndio maana amepunguza makali yake Bungeni ya kuuliza maswali na kuchangia hoja 
Zito alitowa kauli hiyo ya kukanusha uvumi wa kumuowa mtoto wa Rais Kikwete hapo jana juzi wakati akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Mpanda kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Maridadi mjini hapa
Alisema uko uvumi ambao umeenea hapa nchini kuwa makali yake yamekupungua bungeni kutokana na yeye kumuowa mtoto wa Rais Kikwete wakati sio kweli yeye hajamuowa mtoto wa Kikwete 

Alifafanua kuwa yeye Bungeni hayuko kwa ajiri ya kupigana ngumi bali yeye siku zote toka amekuwa mbunge amekuwa akipigania kutoa hoja zenye nguvu ndani ya Bunge kama hana hoja za msingi huwa hakulupuki ovyoovyo
Alieleza ndio maana katika kikao kijacho cha Bunge ameisha wasilisha maombi ya mswada binafsi wa kupendekeza kufutwa kwa sheria ya mwaka 1976 sheria namba 3 ambayo amedai inavinyima haki na uhuru vyombo vya habari 

Wako viongozi wamekuwa wakiitumia vibaya sheria hiyo na hasa pale wanapo kuwa wamekosolewa au kuandikwa vibaya na magazeti mbona mie Zito nilikuwa naandikwa vibaya na kusingiziwa kuwa nimejenga nyumba ya gorofa Dodoma wakati hata kiwanja sina Dodoma lakina hata siku moja sija vichukia vyombo vya habari alisema Zito
Alisema kitendo cha kuyafungia magazeti ya Mtanzania na Mwananchi ni ukiukwaji wa katiba kwani kila mwananchi ana haki ya kupata habari na kitendo hicho kinapunguza ajira kwa vijana 

Alisema leo hii Serikali inapenda kufanya mambo yake kisiri na ndio maana hata mishahara yetu sisi wabunge ambao mmetuchagua nyinyi wananchi hamjuwi wakati ni haki yenu ngoja niwatajie mshara anao pata waziri na Wabunge 

Mshahara wa Mbunge kwa mwezi anapa kwa mwezi shilingi Tsh 11,200,000 wakati waziri mkuu anapata mshara wa shilingi milioni 26 kwa mwezi na kila kitu anapata bure kama ni kosa kutamka mshahara wa ni kosa basi namie nichukuliwe hatua kama magazeti yalivyo fungiwa na kesho nikiwa Wilayani Sikonge ntataja na Rais anapata mshahara kiasi gani kwa mwezi 
Kuhusu katiba aliomba marekebisho ya katiba yazingatie zaidi kuwapa mamlaka ya maamuzi wananchi kuliko viongozi kama ilivyo sasa na alishauri mbunge awe mbunge tuu na asiwe waziri kwani mbunge anapo kuwa waziri matokeo yake ni wananchi waliomchagua wanakosa uwakilishi bungeni 

Alisema anao mfano hai kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda toka amechaguliwa kuingia Bungeni mwaka 2000 hajawahi kuuliza swali hata moja bungeni kama kuna mtu anaushahidi wa swali lolote ambalo Pinda aliwahi kuuliza yeye Zito yuko tayari kumpa shilingi laki mbili mwananchi huyo 

Alifafanua kuwa Pinda alichaguliwa kuwa Mbunge kwa mara ya kwanza na aliteuliwa kuwa naibu wa Tamisemi hivyo nafasi hiyo ya uwaziri imembana muda wote kuuliza maswali 

CHANZO BOFYA HAPA>>http://kataviyetu.blogspot.com/2013/...RBtcU.faceboo

Udaku Specially Blog
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mnafki hana rafiki bora tumejua mapema.kijana kanunuliwa tayari na tume walizo muweka NANI ASIYE JUA TUME YA MADINI KUNA MIJI HELA.

    ReplyDelete
  2. Mimi sioni kibaya cha hayo Magazeti mpaka kufungiwa kama ni kutaja mishahara ya wafanyakazi wa serikari na tena ni haki ya Wananchi wote kujua mbina nchi za wenzetu kama us kila raia anajua mshahara wa Obama mawaziri wake wote ata europe mishara ya viongozi kila raia anajua na wanaandika ktk magazeti kila leo na nimeona kwa macho yangu mwenyewe si km nimeambiwa na sijasikia ata chombo kimoja kipewa onyo wala kufungiwa sababu ni haki ya eaia kujua..nashangaa TZ wanafungia hayo magazeti THAT IS NOT FAIR AT ALL..na kufanya ivyo wao wanajua vijana wangapi wenye familia wamekosa ajira..Wao iyo aiwauhusu koz ni serikari..pls pls hio si serikari inaoongozwa na viongozi kwajiri ua wananchi bali ni serikari inayoongozwa na watu binafsi kwa maslai binafsi na wanaona aibu sababu wanapata mishahara mikubwa na hakuna wanachofanya cha maana just SHAME ON YOU all na Serikari yenu...kuna watanzania zaidi ya milion tano awana uhakika ata wakula na nyinyi mnapokea mishahara mikibwa ivi na amjari ata wananchi wanaishi vipi na wana matatizo gani ni kujinufaisha nyinyi na familia zenu...Utaona mtu ameanza kazi serikarini lakini baada ya miezi mitano kashanunua nyumba zaidi ya moha na magari ya bei kubwa kama si rushwa ni nini...Mi ni mtanzania halisi wa kuzaliwa but sijawai na nimeapa my self kuwa SITOPIGA KURA kwa kiongozi yoyote wa nchi til end of my self na sio kama sitaki ila ALL OF YOU NOT FAIR..

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad