HAWA NDIO WAIMBAJI WAKALI WA NYIMBO ZA INJILI WANAO TAMBA AFRIKA MASHARIKI

KAMA utahitajika kuwataja wasanii kumi wanaofanya vizuri katika muziki wa Injili Bongo na hata Afrika Mashariki, haitakuwa rahisi kuyaacha majina ya Rose Mhando, Bahati Bukuku, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Christina Shusho, Siana Ulomi, Martha Mwaipaja, Jeni Miso na Jennifer Mgendi.

Ni kwasababu hao ni waimbaji ambao katika kila duka linalouza kazi za muziki huo, ni vugumu kupita saa mbili kabla mmoja wao hajauza kazi yake.

Katika wakati ambao wanamuziki wa Bongo Flava na dansi wanalilia kupata soko la kazi zao, waimbaji wa Injili wanaendelea kula kuku kwa mrija kwani kazi zao sokoni zinanunuliwa kama njugu.

Kwa baadhi ya nchi, nyimbo zao hupigwa hata katika kumbi za starehe kwa kuamini ni nyimbo za kujirusha kutokana na mvuto wake.

Rose Mhando

Huyu ndiye kiboko yao, wanamuziki wa Bongo Flava wanamfahamu kwa jinsi anavyowapiga bao katika uuzaji wa kazi zake, si tu katika CD na video, Rose Mhando pia ni kinara wa mauzo katika miito ya simu.

Diamond ambaye anasifika kwa kuuza miito ya simu, akikutana na Rose Mhando anakaa chini kwani mapema mwaka huu alimwacha mbali kwa kuingiza Sh29 milioni ndani ya miezi mitatu huku Diamond akiingiza Sh21 milioni.

Albamu zake za ‘Mteule Uwe Macho’, ‘Kitimutimu’, ‘Jipange Sawasawa’ na ‘Utamu wa Yesu’ bado zinaendelea kufanya vizuri pamoja na kuwa wasanii wengine wanaingiza albamu mpya kila kukicha.

Bahati Bukuku

Huyu anatajwa kushikilia nafasi ya pili ya mauzo ya CD na video katika maduka mbalimbali ya kazi za sanaa Bongo. Pamoja na kutotoa kazi mpya mara kwa mara, albamu yake moja ilimfanya kuwa mwimbaji namba mbili katika mauzo na matamasha nchini.

Tamasha lolote la Injili haliwezi kukamilika bila kupigwa nyimbo kama ‘Waraka wa Amani’, ‘Nimesamehewa Dhambi’, ‘Nyakati za Mwisho’ na ‘Mapito’.

Mwanamuziki huyu kwa sasa anatamba na albamu mpya aliyoizindua mwezi uliopita iitwayo ‘Dunia Haina Huruma’.


Upendo Kilahiro

Inavyoonekana muziki wa Injili unamlipa sana kwani ameweza kuanzisha Chuo cha Ushonaji kiitwacho, New Day Africa Foundation, ambacho wanafunzi wake hawalipi hata shilingi moja kwa muda wanaochukua ujuzi chuoni hapo.

Kilahiro anayetamba na nyimbo za ‘Unajibu Maombi’ na ‘Usinipite’, ni msanii namba tatu kwa mauzo ya nyimbo za Injili Bongo.

Upendo Nkone

‘Niacheni Niimbe’, ‘Nimebaki na Yesu’, ‘Uniongoze Yesu’ na ‘Nakaza Mwendo’, ni baadhi ya nyimbo zinazofanya kazi zake ziendelee kununuliwa kwa wingi. Kila anapoachia wimbo mpya, huendelea kuzifanya zile za zamani ziwe nzuri zaidi.

Mbali na kuuza kazi zake, pia ni mwanamuziki anayeongoza kwa kufanya matamasha ndani na nje ya Bongo. Mara kwa mara hufanya ziara nchini Kenya ambako anakubalika na kuheshimika.

Christina Shusho

Huyu anazo sababu zaidi ya mia moja za kuwa mwanamuziki anayeuza sana katika muziki wa Injili. Kwanza sura yake inapokaa kwenye ‘kava’ inampa mteja hamu ya kutoa pesa yake kununua CD, pili unapopata bahati ya kuisikia sauti yake kwa mara ya kwanza, hakika utataka kuisikia tena na tena na tatu tungo zake zinazogusa maisha ya kawaida na kiroho zimekuwa kivutio kikubwa.

Flora Mbasha, Jeni Misso, Jennifer Mgendi, Martha Mwaipaja na Siana Olomi nao wanaingia kwenye kundi hilo, lakini wanapishana kidogo kutokana na sababu mbalimbali zilizotolewa na wafanyabiashara wa kazi hizi.

Waimbaji Jeni Misso, Martha Mwaipaja na Siana Olomi ni kama wanachipukia kwenye soko kuu la kazi hizi, lakini wamekuwa wakichuana na wakongwe akina Flora Mbasha na Jennifer Mgendi ambao wamekuwa katika muziki huu kwa muda mrefu.

Wafanyabiashara wa kazi hizi wanasema, Jennifer Mgendi na Flora Mbasha, waliwahi kuwa vinara wa mauzo lakini walipoanza kujichanganya na biashara nyingine iliwapunguzia mashabiki ambao walianza kununua kazi za waimbaji wengine.

Flora Mbasha kujihusisha na kampeni mbalimbali zikiwamo za  vyama vya siasa na Jennifer Mgendi kujiingiza katika uigizaji wa filamu, zinatajwa kuwa ni sababu zilizowarudisha nyuma.

Yote kwa yote hii ndiyo ‘krimu’ ya wasanii wanaoongoza sokoni kwa muziki huo, tamasha lolote la muziki wa Injili Bongo au Afrika Mashariki, haliwezi kukamilika bila uwepo wa waimbaji hawa.
Tags

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Yani kelele zenu zoooote hakuna wasanii wa kiume kama vile bony mwaitege, solomon mukubwa na wengine wengi ama soko la muziki wa injili ni la wanawake tu?

    ReplyDelete
  2. Shalom Ninawapogeza sana waimbaji wa Tanzania Mungu Awabariki - Apostle Peter Minja

    ReplyDelete
  3. waimbaji wakiume wamewasahau huo ni upendeleo, mbona hata nao wamo jaman acheni hizo hat mungu hapend

    ReplyDelete
  4. Za uzima watumishi wa Mungu!
    Waimbaji wa kiume mbona wapo wengi tu. Kuna Zako, Richard Leonard, Ambwene, Masanja, Sayuni Band n.k.

    ReplyDelete
  5. Acheni hizo, hakuna mashindano kwenye huduma ya Mungu, no super star in gospel.

    ReplyDelete
  6. MBONA EMANUEL MGOGO SIJAMCCHEKI

    ReplyDelete
  7. No competition in Gospel music

    ReplyDelete
  8. Hakika Waimbaji wetu wamebarikiwa

    ReplyDelete
  9. Welcome to brotherhood Illuminati where you can become
    rich famous and popular and your life story we be change
    totally my name is Dan Jerry I am here to share my
    testimony on how I join the great brotherhood Illuminati
    and my life story was change immediately . I was very poor
    no job and I has no money to even feed and take care of my
    family I was confuse in life I don’t know what to do I try all
    my possible best to get money but no one work out for me
    each day I share tears, I was just looking out my family no
    money to take care of them until one day I decided to join
    the great Illuminati , I come across them in the internet I
    never believe I said let me try I email them.all what they
    said we happen in my life just started it was like a dream to
    me they really change my story totally . They give me the
    sum of $1,200,000 and many thing. through the Illuminati I
    was able to become rich, and have many industry on my
    own and become famous and popular in my country , today
    me and my family is living happily and I am the most
    happiest man here is the opportunity for you to join the
    Illuminati and become rich and famous in life and be like
    other people and you life we be change totally.If you are
    interested in joining the great brotherhood Illuminati.then
    contact him +2348106618681 email:illuminatibrotherpowerful@
    gmail.com or you need my assistance email:danjerry04@gmail.com...

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad