TUNDU LISSU "ZITTO NA WENZAKE WATATU WAMEBAINIKA KUKIHUJUMU CHAMA"

Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimemvua nyadhifa zote Naibu Katibu mkuu wake Zitto Kabwe ambae ni mbunge wa Kigoma Kaskazini.
Mwanasheria mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu kwenye makao makuu ya chama hicho, amesema Zitto na wenzake watatu wamebainika kukihujumu chama  kwa kuanzisha kitu kinaitwa Mkakati 2013 kinacholenga kukisambaratisha chama hicho ili kuwaondoa madarakani Mwenyekiti na Katibu mkuu wake.
Nyadhifa alizovuliwa ni Unaibu katibu mkuu pamoja na Naibu kiongozi wa upinzani bungeni ambapo yeye, Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba na mwingine mmoja Makao makuu wamepewa siku kumi na nne wajieleze kimaandishi kabla ya kuchukuliwa hatua zaidi za kinidhamu ikiwemo kuvuliwa Uanachama.
Tags

Post a Comment

15 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sijawahi kumwelewa Zitto toka nimjue, its like mtu anaeweza kufanya chochote ilimradi akae juu kisiasa. Hongera CDM kwa maamuzi magumu, hio ndio demokrasia.

    ReplyDelete
  2. Ikiwa kinachoelezwa hapa ni kweli au yote tuliosikia na kusoma kwenye vyombo vya habari siku za karibuni kuhusu sakata hili la Zito Kabwe kuhujumu "CHAADEMA" ni kweli nawapongeza sana viongozi waliopo kwenye chama kwa kufanya maamuzi magumu kwa manufaa ya chama. Mimi sio mpenzi wa Siasa hasa Tanzania na Africa kwa jumla ila kwa hili nimeguswa I think with this now may be we are heading to the right direction

    ReplyDelete
  3. I support u guys keep on

    ReplyDelete
  4. Cheap politics

    ReplyDelete
  5. Tatizo la cdm haitaki watu strong kwa sababu atawaoutshine viongozi waliopo. Zitto ni mtu wa misimamo iliyojikita kwenye haki hayumbishwi. Zitto aluta continua wasikutishe wewe ni shupavu mungu atakuongoza utafika panapokufaa.

    ReplyDelete
  6. Zitto is hero msimamo ndio unatakiwa kwenye maisha yabinadam zitto juu kigoma juu

    ReplyDelete
  7. Decision nzuri xana cdm , unafiki tuache.

    ReplyDelete
  8. Hongera sana chadema hii inaonesha kweli mnajali masilahi ya wananchi. Mngemuacha angetufisadi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. wewe ni maiti inayotembea,sjui mbowe kawaroga,mpo kama misukule,hakuna mwanasiasa anaogopwa na ccm kama zito,ila nawashgaa mnamkimbia malaika mnamkubatia shetan

      Delete
  9. Kwa kweli Zito siyo kiongozi imara bali ni mwanasiasa mtafuta vyeo tangu Chuo kikuu hadi kwenye sakata la Buzwagi na hata wakati wa uchaguzi wa wenyeviti wa kamati za bunge tunajua jinsi alivyomuomba sana Kikwete amsaidie apate kiti alicho nacho sasa. Zito hajishughulishi kabisa na uongozi wala uimarishaji wa chama chake bali kila mara ni mlalamikiaji dhidi ya wenzake. Amenishangaza mara mbili akiwa naibu Katibu Mkuu anatangaza kwa vyombo vya habari kuwa amemlima barua katibu mkuu wake kama vile yeye hahusiki kabisa na ofisi ya Katibu mkuu wakati yeye ndiye namba mbili katika ofisi ile. Huyu bwana ni afadhali ahamie CCM ambako nadhani kutamfaa zaidi kwa vile upinzani hakuna vyeo. Kaburu alihamia CCM akawa mbunge wa afrika ya mashariki, inawezekana yeye akawa waziri au naibu waziri.

    ReplyDelete
    Replies
    1. no,,,,coment unakataa za mbele unapokea za mlango wa nyuma ni kwelii hafai chadema ushahidi upo kma ndio ccm walivyopanga wameshinda kwa kumhonga

      Delete
  10. Zito, I feel sorry 4 u 7bu huku soma mchezo toka mapema,wewe pale 2 ulipotangaza kutaka kugombea Urais ulikutana na vtsho gani? Ile peke yake ilionyesha chama kina wenyewe huku ona hilo? Ninachojua kwenye demokrasia upo uhuru kwa mwanachama yeyote kugombea nafac aitakayo ili mradi afuate katiba,uchaguzi peke yake ndio uliotakiwa ukuengue co mtu tu kwa kuwa yeye ndiye mwenye madaraka ya juu,huo ni udikteta,pole sana lakini wewe unakubalika uckate tamaa watakusoma tu.

    ReplyDelete
  11. sikujua kama Tindu lisu ni mshamba na asiyejitambua...shame on you

    ReplyDelete
  12. ni kweli Tundu Lissu anakurupukaga nyie hamjui, ila taratibu mtamsoma tu.

    ReplyDelete
  13. hahahahaaaaaaaaaaaaaaaaa wapiiiiiii chadema kwishney

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad