MAMA ZITTO AFUNGUKA "NILIKUWA NAOMBA KILA SIKU ZITTO AFUKUZWE CHADEMA"

Dar es Salaam. Siku moja baada ya Kamati Kuu ya Chadema kumvua uongozi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Taifa wa chama hicho, Zitto Kabwe, mama yake mzazi, Shida Salum ametoa ya moyoni akieleza kuwa kilichomkuta mwanaye kimefunika mabaya mengi yaliyopangwa afanyiwe.

“Kwa upande wangu naona kama ni ushindi kwa Zitto kutokana na jinsi ninavyojua hali ilivyo, mambo yalikuwa ni mengi mno na nikwambie tu, Zitto kuvuliwa uongozi kumefunika hayo yaliyokuwa yamekusudiwa kufanywa dhidi yake. Nilikuwa naomba Mungu  kila siku ili afukuzwe Chadema,” alisema mama huyo wakati akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake Tabata, Dar es Salaam.

Shida Salum alisema kuwa Mungu amemnusuru mwanaye na kusisitiza, “Watu walikaa na kutengeneza ripoti ya siri kuhusu Zitto na kuiweka kwenye mtandao kisha kuituma kwa wanachama wa Chadema wanaowafahamu. Mpaka wanafikia hatua hiyo maana yake ni kwamba wamejaribu njia zote za kummaliza, lakini wameshindwa.”

Alisema kutokana na hali ilivyo hivi sasa amemnyang’anya mwanaye kwa muda simu zake zote za mkononi, kompyuta mpakato (Laptop) pamoja na iPad ili asiwasiliane na watu, kwa maelezo kuwa wapo wenye nia mbaya wanaomsaka kumpa pole za kinafiki. “Kwa sasa nataka mwanangu atulize akili.”

Shida Salum, mbali na kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, pia ni  mwasisi wa  Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu (Shivyawata) na Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wenye Ulemavu wa Viungo (Chawata).

Zitto pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Dk Kitila Mkumbo juzi walivuliwa uongozi kutokana na uamuzi wa kikao cha Kamati Kuu kilichokutana kwa siku mbili, kuanzia Novemba 20 mwaka huu katika Ukumbi wa Blue Pearl jijini Dar es Salaam, wakituhumiwa  kukisaliti chama.

Mbali ya kuwavua uongozi Zitto, Dk Mkumbo pamoja na  aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho mkoani Arusha, Samson Mwigamba, pia Kamati Kuu imewapa siku 14 wajieleze kwa nini wasifukuzwe uanachama.

Kwa uamuzi huo Zitto amebaki na wadhifa wa ubunge wake wa Jimbo la Kigoma Kaskazini na Uenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

Katika ufafanuzi wake wa jana, Shida aliwataka wanachama wa Chadema kuwa watulivu kwa maelezo kuwa Zitto hajafukuzwa uanachama, “Siku nyingi walikuwa wanamwinda na hata hilo jambo ambalo Chadema wanasema amefanya, hawana uhakika nalo.”

Juzi wakati akisoma uamuzi wa Kamati Kuu,  mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu alisema wamebaini kuwapo kwa mkakati mkubwa wa watu hao kutimiza malengo hayo ambao umeandikwa katika waraka unaoitwa ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013’, ambao umeandaliwa na kikundi kinachojiita ‘Mtandao wa Ushindi’.

Alisema kikundi hicho vinara wake wapo wanne,  Zitto anajulikana kama Mhusika Mkuu (MM), Mkumbo (M1), Mwigamba (M3) na mtu mwingine wa nne ambaye alieleza kuwa hajatambulika na anatumia jina la M2.

Mama Zitto ambaye wakati akizungumza na gazeti hili alikuwa amelala kutokana na kusumbuliwa na maradhi alisema, “Kutolewa katika uongozi ni jambo la kawaida.  Zitto hajafukuzwa chama ila anaweza akafukuzwa maana kapewa siku 14 tu za kujieleza.”

Alisema kauli iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibroad Slaa, kwamba chama hicho walimwondoa Aman Kabourou (aliwahi kuwa Mbunge wa Kigoma Mjini-Chadema)  itakuwa Zitto, inaonyesha jinsi watu walivyo na chuki na mwanaye.

“Hayo ni maneno ya chuki, maana hata Zitto naye ana watu wake ambao wanaweza kutengeneza aina fulani ya chuki kwa viongozi wa chama na wanaweza kupata wakati mgumu kufanya safari au mikutano yao mikoani,” alisema.

Alisema tangu siku nyingi ndani ya Chadema kulikuwa na mpango wa kumng’oa Zitto, akifafanua kuwa hata katika kikao cha Kamati Kuu iliibuliwa hoja ya ruzuku za vyama, huku wajumbe wakimshutumu Zitto kwamba kwa nafasi yake na Naibu Katibu Mkuu alitakiwa kuitetea Chadema kuhusu ruzuku.

Katika vikao vya Kamati ya PAC, Zitto aliingia katika malumbano na chama chake baada ya kutuhumu vyama vya siasa kuwa hesabu zake hazikaguliwi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), huku akitaka ruzuku kwenye vyama hivyo isimamishwe.

“Zitto alipoingia katika kikao cha Kamati Kuu alishikilia msimamo wake kwamba kama Chadema inachukia ufisadi, nacho lazima kihakikishe kinakaguliwa,” alisema na kuongeza;

“Wao wanaona ili waweze kusalimika katika suala hili la ruzuku ni lazima wamfukuze Zitto. Chadema hawako sawa, hesabu zao haziko sawa.”

Alisema kuwa tatizo lililopo ni kuwapo kwa mkakati wa watu fulani kuiyumbisha Chadema , hivyo kila juhudi zinafanywa ili kukitingisha chama hicho kipoteze mwelekeo.

“Siwezi kusema wamemwonea au hawajamwonea, wao wametumia waraka wa Mwigamba ambao Zitto amekiri katika Kamati Kuu kwamba hajawahi kuusikia wala kuuona, tofauti na Dk Kitila ambaye amesema amewahi kuuona,” alisema na kuongeza;

“Zitto anahusishwa na kitu ambacho Chadema hawana uhakika nacho, ukiusoma ule waraka katika aya ya mwisho umeandikwa hivi, ‘Huyu mtu tunayefikiria awe mwenyekiti hajaoa,

tumshauri aoe akikataa tutafute mtu mwingine’, maana yake ni kwamba waraka huo ulikuwa haujamfikia Zitto, kama ungekuwa umemfikia Zitto watu hao wasingemwomba Zitto agombee uenyekiti.” Alipoulizwa nafasi yake ndani ya Chadema kutokana na yaliyomkuta mwanaye alisema, “Mimi hawawezi kunitengenezea jambo. Hivi Zitto anaweza kuwa mbaya mimi nikawa mzuri.”

Mama huyo alieleza kuwa tangu alipovamiwa na majambazi nyumbani kwake, Aprili 19 mwaka huu hajawahi kuhudhuria kikao chochote cha Chadema. “Wale wanaodhani Zitto kaonewa wanatakiwa kuwa wavumilivu na wapole, wasubiri kwani kila kitu kinawezekana.”

Ushauri kwa mwanaye

Alisema kuwa mwanaye ana uamuzi wake na kwamba hata kama Chadema itamfukuza uanachama, haitaweza kumnyang’anya vyeti vyake vya elimu aliyoipata.

“Zitto anaweza kufanya kazi mahali popote duniani, lakini pia ni mwalimu anaweza kuamua kufundisha. Ubunge ni mgawanyo wa madaraka. Watu wote hatuwezi kuwa wabunge,” alisisitiza.

Alisema wakati Kikao cha Kamati Kuu kikifanyika Zitto alikuwa nje ya nchi na kwamba yeye alimshauri kuhakikisha kuwa anahudhuria kikao hicho.

“Alipotua tu na ndege aliniambia kuwa kuna foleni na alitaka kukodi pikipiki ili awahi kikao, aliniambia lazima aende ili kujua hatima yake.

Aliacha gari lake na kwenda na hata mimi nilimsisitizia kwamba ni lazima aende katika kikao,” alisema. Alisema kuwa Zitto alipofika katika kikao hicho aliweza kuzima hoja zote zilizomhusu ikiwamo ya ruzuku za vyama, kwamba baadhi ya wajumbe walipoona amebadili mwelekeo wa kikao, mjumbe mmoja (akamtaja kwa jina) aliibua waraka uliomng’oa Zitto katika wadhifa wake.

“Unajua Kamati Kuu ilijadili zaidi kuhusu ruzuku. Hata ule waraka uliongezwa maneno baada ya baadhi ya wanachama kumpora Mwigamba laptop yake alipokuwa mkoani Arusha katika kikao cha Chadema,” alisema.

Huku akiwataja wanachama wa Chadema walioongeza maneno katika waraka huo (wakiwamo wabunge wawili) na viongozi wa ngazi za juu wa Chadema, mama Zitto alisema kilichomkuta mwanaye ni ushindi mkubwa, kwamba alipangiwa kufanyiwa makubwa zaidi ya yaliyomkuta.

“Hakuna amani maana ukisikia kengele inagongwa hapa nyumbani unasema hao ndiyo wamekuja kumuua Zitto nini, hivi sasa mpaka walinzi wanaolinda hapa wakisikia unakuja nyumbani kwa Zitto lazima wakuandike jina na kukufuatilia,” alisema mama huyo.
-Mwananchi
Tags

Post a Comment

25 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kelele mama wewe mtoto wako ndimi la kuwili

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huna unalo lijua kaa kimya,nyie ndo wale mkiambiwa mkeo anatembea na flan,unachukua maamuzi ya kumpiga bila kumsikiliza,subir usikilize na upande wa pili ndio utoe judgement.

      Delete
    2. Zitto is incompetent, irrelevant and dumb to say the least.
      Wachagga juuuuu

      Delete
    3. Mamayo Eti wachaga juu kumbe chama chenu ni cha kichaga tuone kwenye uchaguzi mkuu kama Tanzania nzima ni wachaga na tumeshawajua.

      Delete
  2. Ndimila kuwili ndio nn wewe Mkongo nn?

    ReplyDelete
    Replies
    1. I do not recount meeting a perfect being my friend. The issue here is the fall of our brother and his short-lived political life..

      Delete
  3. maneno ya mfamaji hayo,mpeleke mwanao ccm

    ReplyDelete
  4. Chama cha Kichaga hicho. Kwani hao watu hamuwajui? Zitto ni tishio wewe. Angechukua fomu ya kuwania urais hapo baadae mngeona Slaa na Mbowe wanavyojiharishia!!! Endeleeni na chama chenu cha ajabu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. ukabila na udini wao ndio utakao teketeza chama chao umtajutraaaaaaaaaaaaaa chaga's power

      Delete
  5. mungu atamsaidia.

    ReplyDelete
  6. Chama cha maigwena!chagas power bado sasa Slaa.itabidi arudi akahubiri injili,chama gani kisichowapa watu fursa ya kugombea uwenyekiti wa Taifa?igwena mbowe ameshika hatamu no way out yeye ndo igwena maisha.halafu wanasema wana demokrasia.ipi hawa ni kundi la maigwena wa kichaga wanaocheza na akili za wanyonge na maskini wa akili.madikteta,ukiwa chadema hutakiwi kuhoji chochote kila kitu unatakiwa useme ndio mzee.chama cha mabondia,tamaa,unafiki chuki,kuhamasisha vurugu.wameleta vita mpk bungeni eti wana machungu na nchi,machungu gani wanayo au wanaficha uovu wao.hawana mfano wa kuigwa na hawafai kuongoza taifa kama hili.nendeni mkawe maigwena wa wachaga wenzenu lakini sio jamhuri ya muungano wa Tanzania.

    ReplyDelete
  7. Tumekuelewa MAIGWENA! dash toka Jana maigwena! Maigwena ndio non jamani nisaidiweee!!

    ReplyDelete
  8. Tatizo zito alijifanya kama mungu wakati yeye cdm ameikuta..na amekuwa na haraka xana ya uongozi..na akitoka cdm ndo siasa imekwisha kwake,ndo ssm walivyo..they use you and dump forever..

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hayo wayasema ww kama Mungu kampangia itakua tuu,na si lazma afanikiwe akiwa chadema

      Delete
  9. Chadema ccm wote vyama vya wakatoriki tu wasenge wezi wakubwa kumamae zenu

    ReplyDelete
  10. Chadema ccm wote vyama vya wakatoriki tu wasenge wezi wakubwa kumamae zenu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Si uanzishe chama cha dini yako kwani umekatazwa? Inaonekana ulikuwa unafirwa wakati unaandika comments zako. Fuck you mdini mkubwa wewe

      Delete
    2. WE ndo mseenge mana waislam asili yao kwa waarabu na ndo wasenge wenyewe kuma kibuyu

      Delete
    3. unaeseama chadema na ccm ni vyama udini! Si uende chama cuf

      Delete
  11. WEWE MAMA NDO UMEMRITHISHA MDOMO NA UMBEA MWNAO ONA XAXA

    ReplyDelete
  12. Kwani nani hajui?!?!kuwa zito ni ccm?????akafie mbele atuache na chadema yeyu

    ReplyDelete
  13. hivi kwa nn na yy hajaoa mpaka leo sasa alivyotaka urais huku hata mke hana ndo nn

    ReplyDelete
  14. kila mtu anataka kula kivyake..hamna chadema wala ccm lets pray MUNGU aiweke nchi yetu sehem nzuri.maskini wazidi kuishi salama,tembo wetu wasiendelee kuuliwa,NCHI IWE NA AMAN.Thus all we want.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad