MTEI "TUTAENDELEA KUWAFUKUZA WALE WOTE AMBAO NI WASALITI CHADEMA"

Mwasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edwin Mtei amesema kuwa chama hicho kitaendelea kuwafukuza wote wanaokihujumu huku akieleza kwamba, anaunga mkono kuvuliwa uongozi kwa Zitto Kabwe na Dk Kitila Mkumbo.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili, nyumbani kwake jana, Mtei aliyewahi kuwa Gavana wa Benki Kuu (BOT) na Waziri wa Fedha katika utawala wa awamu ya kwanza wa Mwalimu Julius Nyerere, aliweka wazi kuwa daima ataunga mkono dhamira ya kukisimamia chama hicho aliyoitaja kuwa ni safi.

 “Naunga mkono uamuzi wote wa Kamati Kuu, kuwasimamisha na kuwavua uongozi Naibu Katibu Mkuu wetu Zitto Kabwe na Dk Kitila Mkumbo. Na kwa sababu Chadema inataka kusonga mbele, lazima iwafukuze mafisadi na wezi wanaoshirikiana kukihujumu chama,” alisema Mtei.

Bila kufafanua zaidi au kutaja majina, mwenyekiti huyo wa kwanza wa Chadema alisema: “Hatuwezi kuendesha chama wakati viongozi wengine wanapokea pesa na kuzihifadhi kwenye akaunti za siri.” Alisisitiza kwamba kwa nafasi yake akiwa mwasisi wa Chadema ni lazima ahakikishe anaunga mkono dhamira safi ya kukisimamia chama.

Kuhusu Arfi kujiuzulu

Akizungumzia hatua ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Saidi Arfi kujiuzulu, Mtei alisema kuwa inafaa kiongozi huyo ajitazame upya na kujisahihisha badala ya kuwa mlalamikaji kila siku.

“Aache kulalamika kwa sababu, wakati alipochaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti mimi nilisimamia uchaguzi. Kama alikuwa na ndoto kwamba siku moja atakuwa mwenyekiti wa Chadema taifa alipaswa kujichunguza kwanza,” alisema.

Mtei aliongeza kuwa iwapo kuna watu wanadhani Chadema itakufa hiyo ni dhana potovu, lakini kwa sasa chama hicho kimejipanga kuchukua dola na tayari wamejiimarisha kimkakati.

“Katika suala la kushughulikia watu wanaokihujumu chama  hakuna ‘compromise’ (mjadala),” alihitimisha Mtei.   Juzi Chadema ilitangza uamuzi wa Kamati Kuu yake kuwavua uongozi Zitto Kabwe na Dk Kitila, huku Arfi akitangaza kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tanzania Bara.

Mtei amewahi kumkemea na kumwonya Zitto katika mambo mbalimbali aliyofanya ndani ya Chadema, moja ikiwa Oktoba mwaka jana ambapo mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini, alipotangaza kuwania urais mwaka 2015.

Alisema kuwa hatua hiyo itasababisha mzozo na mpasuko ndani ya chama,  huku akiongeza kwamba amekuwa akimshauri Zitto mara kwa mara kuhusu hatua yake hiyo akimtaka kuwaunganisha wana-Chadema na siyo kuwagawa au kuwavuruga.

“Hakuna shida kuonyesha hisia, lakini unatengeneza mzozo mkubwa sana ukitangaza sasa. Mimi nimeshamshauri sana Zitto, ahakikishe anakiunganisha chama na siyo kukigawa wala kukivuruga,” alisema Mtei.

Mtei alisema hatua ya mbunge huyo kutangaza kutogombea tena ubunge na badala yake kujipanga kuwania urais mwaka 2015, imekuja mapema mno na kuonya kuwa itaibua mzozo ndani ya Chadema, akiweka wazi kuwa wakati ukifika chama hicho kitafanya uchaguzi sahihi.

“Siyo vibaya kwa Zitto kuonyesha hisia zake, lakini ndani ya Chadema kwa sasa, kuna watu mbalimbali wanaopenda kuwania urais, lakini hawajatangaza. Dk Slaa (Willbrod) anataka, Freeman (Mbowe) anataka, Zitto anataka, hata mimi huenda nikataka kugombea. Hapa hakuna upendeleo, sifa ndizo zitakazoamua,” alisema.

Hata hivyo, Zitto alipinga kauli hiyo akisema: “Demokrasia haileti mizozo kwenye vyama vya siasa hata siku moja,  bali humaliza mizozo. Udikteta, kuminya fikra huru na mawazo huru, ndivyo huleta mizozo kwenye vyama vya siasa.”

Alisema ni muhimu wazee wakawaacha vijana wawe huru kusema wanachofikiri, kwa kuwa uhuru wa fikra na mawazo ni moja ya haki za msingi na moja ya nguzo za demokrasia.

“Ninarudia, nitaomba kupeperusha bendera ya chama changu kwenye uchaguzi wa urais mwaka 2015.  Naamini kwamba ninaweza kuwezesha chama chetu kushinda na kuongoza dola na Chadema kutoa rais wakati baadhi ya waasisi wetu wakiwa hai na kuona vijana wao tunavyobadili maisha ya Watanzania na kutimiza ndoto zao,” alisema Zitto.

Alisema ana uwezo, uadilifu na uzalendo wa kutosha kuwa Amiri Jeshi Mkuu na kuunganisha Watanzania kuwa wamoja bila kujali rika, dini wala makabila yao... “Nimejiandaa kisaikolojia kukabili changamoto za ufukara wa nchi yetu.”
Tags

Post a Comment

23 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Busara na umakini ndio unaitajika

    ReplyDelete
  2. Huyu babu nae ameishiwa!

    ReplyDelete
  3. Huyu nae arudi kijijini akanywe mbege,nani kamdanganya kuwa wachaga wataiongoza tanzania,kama chama chenyewe hakitaki makabila waongoze mmeshaharibu mmejionyesha kuwa hamstahili kupewa madaraka,hamtudanganyi ng'o,watanzania tunazo akili za kututosha.

    ReplyDelete
  4. We babu kaa upumzike huko huna lolote ww

    ReplyDelete
  5. Umeisha zeeka,pumzika waachie vijana.

    ReplyDelete
  6. Then tatizo kubwa litakuwa ni utashi wa MM kugombea U-Amirijeshi! Kwamba,ili kufanikisha hilo anaweza kweli kuwa ameconspire na CCM baada ya kuona ugumu wa kulifanikisha hilo ndani ya Cdm pekee! Kama ndivyo MM alikuwa anatimiza demokrasia lakini with wrong means! Therefore I pronounce your GUILTY Mr. MM. Ila pia CDM utazameni mfumo wa kupata wagombea wa ngazi za juu haraka na kwa umakini,vinginevyo utakiua chama.

    ReplyDelete
  7. Mtei.Unatutonesha kidonda.si uwaache wanachadema waamue wenyewe?ni wasomi na ni watanzania halisi kama wewe na mbowe.Tatizo lako na mbowe ni uhusiano wenu wa baba na mkwe.Hivi unaweza kuwa na ujasiri wa kumkosoa mkweo?Hata kama uliisasisi chadema kwa sasa si mali yako tena ni kimbilio na tegemeo la watanzania wote waliolowea kwenye umaskini wa kulazimishwa kwa zaidi ya miaka hamsini!Gavana muda wenu umekwisha tunawashukuru kwa kutufikisha hapa tulipo leo waachie wengine tuone kama watatuvusha.mbowe ni msomi na ni mtu mzima mwache asimame kwa miguu yake mwenyewe.

    ReplyDelete
  8. Mi nadhan mbowe na slaa ndo wana2miwa na ccm kukivuruga chama kwa nn wafanye hv coz wanajua kua zito ni jembe!!! Yap chadema ilaikuwepo ila hakuna m2 aliyekipa na kukijengea chama umaarufu kama zto kabwe kupitia hoja zake bungen. So inashangaza kuona hl lililotokea kumuona ni msalati..pale linapokuja suala la kuambiana ukwel ndan ya chama. Hii ina2funya 2amin kuwa wewe mbowe na slaa mna2miwa na ccm ukiachilia mbal ukabila uliopo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. mm mwenyewe nashangaa hawa wazee ndio hawakitakii chema chama chao kama zitto ni kijana na anakubalika katika chama chake iweje wamzuie zitto asigombee urais wenyewe wamezeeka na ni waroho wa madaraka, kwa mantiki hiyo mtasubiri sana acha ccm isonge mbele shwain nyinyi

      Delete
  9. Huyu mzee ndo tribe legend

    ReplyDelete
  10. Sory huyu babu anataka nn jmn? Wazee wenzake wamelala, akakojoe alale achia vijana siasa

    ReplyDelete
  11. Ushauri wa bure kwa Mzee Mtei.Kasi hii haiwezi.Atake asitake siku moja Mbowe atautema uenyekiti!Mzee wetu iga mfano wa mzee Mandela,Nga'tuka.Naamini binti yako amekupatia wajukuu.Ni muda mzuri sasa kucheza na wajukuu,usogeze siku.Bado tunakuhitaji.lakini suala la kuongoza chadema kwa remoti litukupa presha na kuharakisha kifo chako.Wakati ukuta!

    ReplyDelete
  12. jamaani kumbe zitto ni wakulekule kilimanjaro ila alisahau kuandika majina yake yoootee anaitwa hivi:- ZITTO ZUBERI KABWE URIO MSHANA MASSAWE MBOWE SHIRIMA KIMARO URASSA kwa hiyo katika ile itifaki yenu ya ukabila anakubalika mrudishieni vyeo vyake tatizo si kabila tuu mbona hatujasikia mjadala wa kumjadili mchaga au mpale inamaana wao huwa awakosea ndani ya chama? kwa mtiondo huu wa tribalism na wengine wajiandae mapemaaa!!!!

    ReplyDelete
  13. Aende zake kule na mimacho kana alijua chama ni mali yake kwann hakukifanya sacoss wakopeshane wao kwa wao,basi wabaki na ukabila wao na nchi hawaipat ng'ooo

    ReplyDelete
  14. old age
    old wisdom
    older perception

    hey grand pa
    your too old to interract with the present political matters ain't as your old-systems

    relax
    you did your part
    let them do as they wish as they're in control
    despite your honor as a FOUNDER but NOT all of your opinion'll be taken into acount......Lol

    i know you're CHAGGA too
    but the trend of relegating powers from NON-Chagga persons; it shows that the PARTY is so tribal
    and if you wish to head the STATE HOUSE by 2015, please STOP that FAKE decissions

    from UG

    ReplyDelete
  15. Tusiache kuzungumza ukweli unaoonekana,chadema umaarufu wenu mkiufatilia sana kupitia ktk mikutano na maandamano ni vijana wengi ambao kwa aslilimia kubwa wameshajikatia tamaa na maisha hata ukimuuliza kuwa demokrasia ni kitu gani hajui kiufupi ni bendera zinazofuata mwelekeo wa upepo,hivyo msikae mkajidanganya kuwa tuna wafuasi kwani sisi tulio karibu na hao vijana ukimuuliza kipande cha mpiga kura hana,kadi ya uwanachama hana,mnawapandikiza maneno ya chuki wanaandamana wanavunja sheria za nchi wakivunjwa miguu mnabakia kutoa pole za midomo,kumbukeni kuwa mwenyekutafuta kitu kwa hila hatafaidi ipo siku atakamatwa,vijana tugutukeni hawa jamaa si wa kawaida wanatutafutia majanga,tusidanganyike na wanasiasa wenye uchu wa madaraka na ulafi,Mungu Ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  16. Mtei amedhihirisha wazi hiki chama cha maigwena wa kichaga.anamwambia Arif kama ana ndoto ya kugombea uwenyekiti wa taifa ajichunguze ina maana uwenyekiti wa taifa kwa chadema haruhusiwi mtu mwingine isipokuwa wachaga pekee.zito amepigania chadema mpk kimejulikana leo anaambiwa ni msaliti hawa hawana fadhila,sasa bado slaa ni bora aanze kuhubiri injili ya bwana yesu kuliko kusubiri aibu hapo.mungu amezianika malengo yao live,hawa ni madkiteta,full vurugu,na unafiki kama hali yenyewe ni hii je wangeshika dola watu wangetesekaje?poleni wana chadema mtaendelea kuwa chambo wenzenu wanapeta tu.mbona wakisema muandamane hamuandami pamoja wakisha ona polisi wanakimbia wanaacha mkiumizwa?chama kinachotegemea huruma ya wananchi,hawana chochote jipya ni yale yale.igwena mbowe oyeeee!mfalme wa chadema.

    ReplyDelete
  17. Changa team will never win . Watanzania c wapumbavu.mtei huyo mkweo mbowe ndo anayekuweka mjini Kl Ndio boss usitafute matusi humu ndani kama still unahitaji kujeshimiwa nyamaza babu ukalale.

    ReplyDelete
  18. kama mnafanya kuwa hiki ni chama cha wachaga sasa mtuambie kuliko kuanza kuwazushia na kuwafukuza viongozi wenye misimamo,.

    ReplyDelete
  19. tayizi chadema ina uroho wa madaraka sasa mtashaa

    ReplyDelete
  20. KUNA MTU MUHIMU SANA NASHANGAA ANASAHAULIKA, MTU KAMA SHIBUDA MNASUBIRI NINI KUMTOA?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad