YANGA YAPEWA MASHARTI KUMSAJILI MCHEZAJI OKWI

YANGA na Azam kama zinamtaka straika wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi ni fedha yao tu, lakini kuna sharti lazima walifanye.

Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) limetoa masharti na muongozo wa klabu zinazomtamani mchezaji huyo aliyesitisha mkataba na Etoile du Sahel ya Tunisia.

Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba aliiambia Mwanaspoti kuwa: “Hakuna kinachoizuia klabu kutaka kumsajili Okwi, cha muhimu wanatakiwa kuongea na Etoile du Sahel ya Tunisia, wakimalizana nao basi watamchukua, hivyo ni ruksa cha muhimu ni kufuata sheria na haki.”

Okwi ameidhinishwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kuichezea SC Villa ya Uganda kwa muda wa miezi sita huku sakata lake la Etoile likifanyiwa ufumbuzi.

Mchezaji huyo anaidai Etoile malimbikizo ya mishahara pamoja na dau lake la usajili huku Simba iliyomuuza kwa Waarabu hao nayo ikidai dau lake Sh 480 milioni.

Suala hilo lipo Fifa na Kawemba amewahakikishia Simba kwamba wasiwe na wasiwasi watapata haki yao.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Yanga oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  2. Kashuka kiwango

    ReplyDelete
  3. hovyoooooooo! Kama limejinyea vile lione bichwa kama tikiti maji

    ReplyDelete
  4. Huyo ni simba damu mzee wa 5-0

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad