Mfanyabiashara wa magari, Gabriel Munisi (35), jana alijiua baada ya kumuua mtu mmoja na kujeruhi wengine watatu jijini Dar es Salaam katika tukio linalohusishwa na wivu wa mapenzi.
Munisi, ambaye alikuwa mkazi wa Mwanza, aliwapiga risasi watu watatu akiwamo mchumba wake, Christina Alfred katika Mtaa wa Bungoni Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.
Baada ya kumpiga risasi mchumba wake huyo na kudhania kwamba amemuua, inadaiwa kwamba Munisi aliendelea kuwamiminia risasi watu wengine na kumuua mdogo wake Christina, Alpha (22).
Katika tukio hilo, Christina na mtu anayedaiwa kuwa mchumba wake mpya, Francis Shumila wamelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kujeruhiwa. Mama yake Christina, Helen Alfred amelazwa katika Hospitali ya Amana baada ya kujeruhiwa pia.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marieta Minangi alisema Munisi alikutwa na bastola moja, magazini mbili na yalikutwa maganda 14 ya risasi zilizotumika na risasi mbili ambazo zilikuwa hazijatumika.
Tukio hili limetokea mwezi mmoja baada ya mwandishi wa habari wa ITV, Ufoo Saro kujeruhiwa kwa risasi na mzazi mwenzake, Anthery Mushi.
Katika tukio hilo, Mushi alijiua baada ya kumuua mama mzazi wa Ufoo na inaaminika pia tukio hilo lilisababishwa na masuala ya mapenzi.
Lilivyotokea
Mashuhuda waliokuwapo katika tukio hilo walisema mauaji hayo yalitokea saa 1.15 asubuhi baada ya Munisi kufika Ilala Bungoni na kwenda katika Klabu ya Wazee iliyo jirani na eneo yalipotokea mauaji na kunywa supu kabla ya kusogea karibu na lango la nyumba anakoishi mchumba wake.
Mmoja wa majirani, Noel Gerald alisema alimuona Munisi akiwa amesimama karibu na lango la nyumbani kwa kina Christina.
Alisema baadaye waliona gari aina ya Toyota Hilux, Surf, likitoka katika lango la nyumba hiyo na mara walimuona Munisi akimwamuru dereva ashushe kioo lakini alikataa na kudai kwamba ndipo alipoamua kuwapiga risasi waliokuwamo kwenye gari hilo.
Alidai kuwa Munisi alipiga risasi nane mfululizo huku akiwa analizunguka gari hilo na kwamba alimpiga dereva ambaye baadaye alifahamika kuwa ni Shimula. Imeelezwa kuwa majeruhi huyo ni raia wa Kenya na ni rubani wa ndege.
MASHUHUDA WAELEZEA JINSI MUUWAJI ALIVYOUA KWA RISASI NA YEYE KUJIUA NI KAMA MOVIE
16
November 20, 2013
Tags
Haya sasa dada zetu mtatumaliza kwa tamaa zenu za kipumbavu.
ReplyDeletesio tamaa na nyie wanaume ni vinganganizi ukiambiwa sikutaki uelewe sasa ukilazimisha mapenzi mwisho wake nini? haya ona umekufa walengwa bado wako hai na watafunga ndoa na wataishi maisha yao ya furaha wewe utaishia kuchomwa moto wa jehanamu mapenzi sio kulazimisha mjifunze kukubali matokeo
DeleteTamaaa mby wadd wa kichaga jirekebishen kila siku nyie tuuu,mnatuharibia na sisi
ReplyDeletemwanaume akimuacha mdada kwenye mataa mnatoa maneno machafu yule muhuni kaachwa kenda muoa mwenye adabu mbona mkifanyiwa nyinyi wanaume mnakua wakali?
DeleteInauma sana. Huyo dada alikuwa hajiwezi na hata kuvaa alikuwa hajui huyo jamaa alikuwa analea. Halafu leo hii amependeza eti anamwacha anaenda kwa pilot. Ona sasa umepoteza maisha ya watu wasio na hatia
ReplyDeleteshosti kulea unalelewa na wazazi wako sio mtu mwingine kumbe kulikua hakuna penzi kama mtu anakulea maana yake ni mzazi wako sio mpenzi wako na alipomaliza kumlea binti amepata ampendaye shida iko wapi? unadhani kumlea mwanamke ndio uchukua advantage ya matatizo yake na shida zake ndio ulazimishe mapenzi? ukweli ndio huo aliemlea alichukua jukumu la ulezi na uzazi shoga umetusaidia kujua huyu dada hakukosea kwenye maamuzi yake ya kupata mchumba anayempenda sio mchumba kwa ajili anakulea tofautisha mapenzi na matunzo
DeleteAisee kutokana na maelezo yako, yani we hata kama unapambana na nyoka haki ya mungu mimi nikishika fimbo ni heri nikuchape wewe ili nyoka aende zake kwa amani
DeleteMwandishi, Francis Shumira ni baharia na sio rubani.
ReplyDeletemi naumia sana ninaposikia et wamepona,wangekufa tu hawa wote
ReplyDeletendio uone kama mtu hajakukosea mungu hawezi kuwahukumu na ndio maana wamepona na watafunga ndoa yao na wataishi kwa amani na furaha na upendo na mwenye makosa ameshaingia kwenye moto wa jehanamu anakostaili, mapenzi ya bwana yametimia aliekipanga mungu binadamu hawezi kukitenganisha hata uje na bunduki
DeleteAnonymous 9:11 am naona umeshapewa nguvu za kimungu tayari na unaanza kuhukumu eti emeshaingia kwenye moto....kwanza ni Mungu wa aina gani mkatili hvyo anayechoma watu moto?akili/mawazo ya Mungu sio kama yako.Pili mabaharia ni Malaya kwa taarifa yako huwa hawaoi, uzuri mmoja tu ni kwamba wanajua kum-handle mwanamke kipindi wanapomhitaji tu
DeleteWe jidanganye. Kama unabisha na wewe fanya ubabaishaji wa penzi uone kama utapona. Unajipa matumaini kwenye mali za watu. Kama wewe huna kipato ridhika na hali yako siyo kijipeleka kwenye mali za watu. Afu leo hii useme eti umelelewa na wazazi wako. Pigana upate vyakwako siyo kula vya watu. Pumbavu
ReplyDeleteukweli unarudi pale pale alikipanga mungu binadamu hawezi kukitenganisha
DeleteWewe 9:09 mwehu kweli. Mimi nakufahamu unakula pesa za watu halafu unateleza. Yatakukuta
ReplyDeletepumbav sana huyu muuaji,ivo akuwaona wanawake wote walio jaa vichocholoni wanauza kuma bei poa tu,leo kaenda kujitoa kafala bure kisa malaya
ReplyDeletewe hujui machungu ya kuachwa
Delete