HABARI KAMILI KUHUSU BABU SEYA NA PAPII KUENDELEA NA KIFUNGO CHA MAISHA..SOMA WALICHOSEMA HAPA


Ni dhahiri kwamba huu ndio mwisho wa harakati za Mwanamuziki maarufu wa muziki wa dansi Tanzania mwenye asili ya Congo DRC Nguza Viking na mtoto wake Johnson Nguza (Papii kocha) kujinasua kwenye kifungo cha maisha gerezani.
Kwa mara nyingine tena harakati zao za kujitoa kwenye adhabu hiyo zimegonga mwamba baada ya Mahakama ya Rufani kupigia msumari wa mwisho uliozima harakati zao kujinasua baada ya kutupilia mbali maombi yao ya marejeo ya hukumu ya rufaa yake.
hii ni mara ya tatu kwa wafungwa hawa kugonga mwamba baada ya Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam na Mahakama ya Rufani kutupilia mbali rufaa zao kupinga hukumu ya Mahakama ya hakimu mkazi  kisutu iliyowahukumu kifungo cha maisha.
Wafungwa hawa kupitia kwa Wakili Mabere Marando walikua wakiiomba Mahakama ya Rufani ifanye marejeo ya hukumu yake ya February 11 2010 iliyothibitisha adhabu hiyo waliyohukumiwa na Mahakama ya chini na badala yake iwaachie huru lakini Mahakama ya Rufani katika uamuzi wake uliotolewa na Majaji watatu, Nathalia Kimaro, Salum Massati na Mbarouk Mbarouk ilitupilia mbali maombi hayo hivyo waendelee kutumikia kifungo cha maisha gerezani.
Ni uamuzi ambao uliibua machungu sio tu kwa Wafungwa na ndugu zao lakini hata kwa Wakili wao mwingine Gabriel Mnyele aliesema ‘hakuna namna nyingine ya kuwachomoa kwenye adhabu hii isipokua miujiza’
Ndugu na watu wengine waliohudhuria Mahakamani waliendelea kutokwa na machozi ya huzuni pale Wafungwa hawa walipokua wakipandishwa kwenye gari la Magereza kurudishwa kuendelea kutumikia adhabu yao.
Kauli ya Mahakama baada ya kutupilia mbali maombi yao ni ‘Waomba Marejeo hao hawakuwa na hoja ya msingi kwa sababu hoja zilizotolewa sio tu hazikidhi kuifanya Mahakama irejee hukumu hiyo bali pia zilishatolewa wakati wa usikilizwaji wa rufaa na kutolewa uamuzi na kwamba waomba Marejeo hawakuweza kubainisha makosa waliyodai yalijitokeza kwenye hukumu iliyowatia hatiani na hawakuweza kueleza ni jinsi gani yalisababisha haki kutotendeka’
Mahakama hiyo imesema ‘kuhusu upande wa mashtaka kushindwa kuwaita Mahakamani mashahidi wanaoonekana kuwa muhimu kuunga mkono ushahidi wa Watoto, tunasema hoja hiyo haina msingi…. suala la shahidi gani aitwe Mahakamani kuthibitisha kesi ya upande wa mashtaka liko mikononi mwa upande wa mashtaka, zaidi ya yote idadi ya Mashahidi sio hoja ya msingi bali kuaminika kwao’
Wakili Mnyele amesema ‘huu ndio mwisho wa mchakato, kulinganisha na hukumu ilivyokua ni kwamba kunahitajika kuwepo na Mahakama ya juu zaidi ya hii, kungekuwepo na Supreme Court ingeweza kusikiliza na kufikia maamuzi ya haki’
Kwa upande wake, Babu Seya wakati akipelekwa na askari kwenye gari la Magereza alitoa kauli ambayo hakuipa ufafanuzi wowote baada ya kuisema kwamba ‘kwa binadamu ni makosa lakini kwa Mungu hakuna makosa’
Papii Kocha nae wakati anapelekwa kupanda gari arudishwe Magereza alisema ‘sasa tunamuachia tu Rais ndie anaweza kutoa uamuzi wa mwisho’
Babu Seya na wanawe watatu walihukumiwa adhabu ya maisha gerezani na Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu June 25 2004 baada ya kupatikana na hatia ya kuwabaka na kuwalawiti watoto kumi wa kike wenye umri chini ya miaka 10.

Post a Comment

20 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. poleni sana ila duniani sheria mbinguni haki

    ReplyDelete
    Replies
    1. acheni ujinga Babu Seya amelawiti watoto mnataka atoke aje kulawiti wengine zaidi? hivi hao majaji watatu waliokaa na kuamua mnafikiri hawajaona makosa yake? msilete ujinga wenu amefanya kosa unalipa madhambi uliyowafanyia watoto malaika jela ndio panawastahili, wakuonewa huruma ni wale watoto walioharibiwa maisha yao

      Delete
    2. Acha roho mbaya wewe

      Delete
  2. eeh andhar kanoon

    ReplyDelete
  3. mahakama kipofu.

    ReplyDelete
  4. U kyala wanaka tumulekele fyoshi

    ReplyDelete
  5. Hv hii sheria himuoni kapuya au jamani sheria si msumeno hukata kwa mafukara peke yake lmao

    ReplyDelete
  6. Noma hayo yote tumuachie Rais ndie uamuzi wa mwisho

    mahakama kipofu

    ReplyDelete
  7. Kuna mkono wa mtu hapo ila kwa mungu wote sawa hakuna rais, mbunge, hakimu askari wala mfungwa wote kifo kwanza kitakachofuata malipo kwa yale tuliyoyatenda hapa duniani, CHEO NI DHAMANA BANDUGU

    ReplyDelete
  8. Sorry wadau naomba mnijuze maana ya hilo neno lmao

    ReplyDelete
  9. "Kwa binadamu makosa, ka mungu s makosa"

    ReplyDelete
  10. Yote heri papi kocha na babu seya kama kweli hamjafanya ilo kosa jua kwamba Mungu amtupi mjaa wake. Tambua kwamba malipo hapahapa duniani na wala cio mbinguni kokote muendapo Mwenyezi Mungu awasaidie

    ReplyDelete
  11. hivi inawezeka kweli kesi ikahukumiwa bila hata shahidi moja, i cant belive ma eyes, hii tz bwana hakuna haki hata kidogo, imeniuma sanaa kwa nn shahidi wa upande wa pili wasiitwe.

    ReplyDelete
    Replies
    1. nyie mnacholilia ni muziki wao na wala sio kingine....panel iliyo wahaoji wale watot iliridhika kuwa hawa akina nguza walifanya kosa. kuna njia nyingi za kuwahoji hawa watot hata kama walikuwa wametumwa ingejuliakana.Umaarufu ni mbaya sana jamani kama ww ni maarufu mwombe Mungu akupe hekima maana unaweza kulewa sifa ukafanya mambo ambayo hata dunia ikisikia hawataweza kuamini

      Delete
    2. Wewe Zena Juma unataka ushahidi gani?daktari alithibitisha kuwa watot walifanyiwa hvyo vitendo, watoto nao walikiri kufanyiwa hvivyo vitendo na waliotajwa unataka ushahidi gani zaidi?Fuatilia kesi nyingi za ubakaji wa watoto siku hizi tz, mtoto analawitiwa anamwambia mzazi, mzazi anakwenda polisi, baada ya hapo anapimwa na daktari.Daktari akithibitisha tu kwamba mtot kafaniwa hicho mtuhumiwa lazima afungwe miaka 30 na kuendelea, hakuna ushahidi mwingine unaohitajika hapa.Mbona kesi kama hizi hamzilalamikii?kesi kama hizi zikipata shahidi jua mtoto aliokolewa

      Delete
  12. Jamani amna hata kesi hapo they hve samething kinarol tu hapo watanzania tumefanywa mazuzu.. hvi kweli baba atoke nä watoto wake wa kuwazaa wakabake vitoto vya miaka nane kweli.. nipo me nakataa waliowafanyia hvyo Sijui kama wataiona mbingu..ni wauwaji. Mungu atawalaani sana. Mungu awatie nguvu akina babu seya.

    ReplyDelete
  13. Msure kasema over!!

    ReplyDelete
  14. hawa jamaa inawezekana wametenda kosa,mana wa congo ndio zao kuamini ushirikina,yaweza kuwa waliambiwa na mganga,sema tu jamaa wameshatubu wanapaswa kusamehewa,coz kama mungu anasamehe kwanin nasisi wanaadam tusisameh,hao majudge wanakuwa na roho sijui za namna gani

    ReplyDelete
  15. Angefanyiwa mtoto wako bila shaka ingekuuma sana lakini watoto wawatu haiumi. Hii inatoa fundisho kwa anaetaka kufanya hivyo afikirie mara mbili. Nawaonea huruma lakini walivyofanya kwa mungu ndio kuna uamuzi wa haki aidha kuongezewa adhabu au kusamehewa

    ReplyDelete
  16. kama kweli waliwalawiti watoto wafie jela na kama wamebambiziwa kesii hii lazima irrudiwe upya kwenye serikali mpya ya chadema na tukija baina wamefungwa kwa ila nyie majaji na huyo mhe wenu adhabu yenu ni kunyongwa

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad