UFOO SARO "NILIOKOKA KUFA KUTOKANA NA MIUJIZA YA MUNGU"

Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufoo Saro ambaye alijeruhiwa kwa kupigwa risasi na mzazi mwenzake, Anthery Mushi, amefanya ibada na kusema: “Namshukuru Mungu kwa kumponya.”

Ni mara ya kwanza Saro kuzungumza tukio hilo tangu aliporuhusiwa kutoka Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu, MOI ya Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa.

Katika ibada hiyo iliyofanyika katika Kanisa la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Kibamba, Jimbo la Magharibi, Ufoo huku akitokwa na machozi na wakati mwingine kushindwa kuzungumza alisema: “Ni miujiza tu ya Mungu yeye kunifanya mimi kuwa hai leo.”

Mtangazaji huyo ambaye alilazwa kwa zaidi ya wiki mbili, aliwashukuru watu wote waliomtia moyo, kumsaidia kipindi chote alichokuwa mgonjwa.

“Sina cha kuwalipa, ninawashukuru sana kwa wema wenu, pia kwa kuniombea. Mungu ni mkubwa na amenipigania, naendelea vizuri kwa sasa,” alisema na kuongeza:

“Mungu alinisimamia na nyinyi pia mliniombea, hakika sina budi kushukuru kwa kila jambo. Nitasoma zaburi ya 146 katika Biblia Takatifu ili kumshukuru Mungu kwa kunisaidia.”

Ufoo alisema kuwa ameamua kumshukuru Mungu kwa sababu siyo watu wote wanaopata matatizo kama yake wanapona.

Mchungaji aliyeongoza misa hiyo iliyoanza saa 4 asubuhi hadi saa 7 mchana, Joseph Maseghe alisema Mungu hakupanga Ufoo afariki dunia kwa kupigwa risasi.

“Mungu bado anakuhitaji, hakupanga ndiyo maana upo nasi leo. Hautakiwi kulia huu ni mwanzo wa maisha yako mengine, usilie unachotakiwa ni kumshukuru Mungu kwa kila jambo,” alisema.

Misa hiyo ilihudhuliwa na watu mbalimbali wakiwamo wafanyakazi wa ITV pamoja na Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Grace Kihwelu, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), John Heche.

Baada ya kumalizika kwa misa hiyo, ndugu na marafiki wa karibu wa Ufoo walialikwa na mtangazaji huyo katika hafla fupi ya chakula cha mchana.

Akizungumza wakati akiwakaribisha wageni katika chakula cha mchana, alisema: “Nimepata pigo kubwa katika maisha yangu, familia yetu sasa haina baba wala mama, kweli namshukuru Mungu na nawaombea kwa Mungu wote walioniombea na kunitakia mema, sijui nimpe nini Mungu, sijui kwa kweli.”
-Mwananchi
---------
Bonyeza like hapa chini kama umeipenda habari

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Baadae utueleze basi mpendwa kulikoni Mushi atoke Dafur nakuja kuwaporomoshea marisasi ovyo ovyo na kujiua mwenyewe wakati haluwa kichaa. Tafadhali funguka hapo tu, kumshukuru Mungu, chakula nanini na nini haitoshi, Mungu yeye anajua mkosaji nani hapo sasa cc wanadamu ili tusihukumu mtu kimakosa basi baelezeee!

    ReplyDelete
    Replies
    1. kosa lingekuwa la mushi angefunguka sana tu lkn kosa lake mwenyewe atafungukaje, yarabi nafsi

      Delete
  2. Mungu yupo pamoja nawe dada ufoo inatakiwa utoe na sadaka kweli mungu anakupenda sana

    ReplyDelete
  3. mungu amekupa nafas ya kutubu na kuachana na huo ushetan wako maan mtu akifa hua hana nafasi ya kutubu tena

    ReplyDelete
  4. Tunaomba atueleze jinsi alivyotapeli zile hela za jamaaa

    ReplyDelete
  5. Haina haja kutueleza chochote maana mwisho atatenda dhambi ya uongo. Mtumikie Mungu kwa moyo wote kwa maisha yako sasa.

    ReplyDelete
  6. Acha umbea sasa we akuelezee nini

    ReplyDelete
  7. Ufoo!kwanza utubu kwa moyo wako wote ukiri makosa yako yote maana ww ndio unajua yaliyotokea na chanzo ni nini,maana kwa hali ya kawaida mtu hawezi kuchukua maamuzi mazito kama yale,kuna unachokijua moyoni mwako na usipotubu kwa imani hiyo dhambi haitakuacha kamwe,take care xsana umeshatafsiriwa vibaya mno kwa sababu ya ww kutowaelza watanzania ukweli,japo naamini huwezi sema ni siri yako.

    ReplyDelete
  8. Ingekuwa vzr pia kama ungekwenda kwanza kwenye kaburi la mamayako na kufanya Ibada kubwa kwa sababu wee umekuwa njia ya kifo cha mamako. Ukweli unaujua mwenyewe but 4 me its your second chance, tubu mara saba sabini kipo ulichomkosea Anthery Mushi (R.I.P)

    ReplyDelete
  9. pole sana ufooo tubu dhambi zako.

    ReplyDelete
  10. Diablo mkubwa wee you deserve to die

    ReplyDelete
  11. Asiye na dhambi na awe wa kwanza kumuhkumu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad