Leo wakati nakuja hapa nilipo muda huu nilikuwa nimeongozana na wadada kama wa-4 hivi inaonekana wanaishi jirani na wanakofanyia kazi au kuishi ni kumoja
Wadada hawa walikua na story iliyovuta masikio yangu na kunifanya nipunguze spidi ili niendelee kuwasikiliza kwa kuwa tulipokuwa pana ka umbali kidogo hadi ufikie kituo cha usafiri wetu wa umma[Hiace/daladala/vifordi]
Wadada hawa walikuwa wanamzungumzia mwenzao ambae inaonekana siku za karibuni ataolewa
Tatizo halikuwa kuolewa bali anaemuoa
Inasemekana kuwa huyo mume mtarajiwa wa rafiki wa hao akina dada hajawahi kufanya ngono,yaani ni bikra wa kiume
Wadada wale walikuwa wanamlaumu mwenzao kwa kutokusikiliza maelekezo yao kwa kukataa kuolewa na huyo jamaa kwakuwa ni "mshamba" yaani hayajui mapenzi kitendo kitakachomfanya rafiki yao aanze kutembeza shule kwa huyo mume namna ya kugegeda kitendo ambacho wale wadada hawakukubaliana nacho
Walionekana kukerwa sana na walikuwa wanasema wao hawawezi kuja kuolewa au kuwa na mahusiano na mwanaume wa aina hiyo
Story hiyo ikanikumbusha miezi kadhaa iliyopita nilikuwa nazungumza na jamaa zangu kuhusiana na suala hili ambapo kuna jamaa alikuja kutulalamikia kuhusiana na mkewe kutokujua mapenzi kwa sababu alimkuta bikra
Jamaa yetu yule alionekana kukereka sana na alifikia kusema kama angejua asingemuoa
Kati ya vijana tuliokuwa pale watatu walikubaliana na yule jamaa
Nilishangaa!
Nilidhani kuwa kama ukimkuta mwanamke sio used basi unafurahi kumbe sio
Sasa nikiunganisha na hili tukio la leo naona hili jambo kama linakua flani hivi,yaani huenda hili suala hapo siku za nyuma lilikuwepo lakini inaonekana linachukua kasi mbaya
Nimeamua kulileta hapa ili nijue Wanaume wa hapa wanalichukuliaje suala hili
Pia wanawake nao wanalichukuliaje hili
Yaani kama kuna watu wawili ambao unatakiwa uchague kati ya huyo mmoja awe mwenzi wako na mmoja ni used na mwingine sio,ungependa yupi awe mwenzi wako na kwanini?
Watu wa siku hizi inaonekana hawapendi masuala ya kuanza kufundishana,wanataka watu ambao ni waalimu tayari
Inaonekana sisi mabikra tutaipata mwaka huu....lol!
Naomba mchango wako tafadhali!
Mdau-
Usizini. Hilo ni agizo la Mungu muweza na anayejua yote. Bikira ndiyo mwenyewe haswa. Matatizo aliyonayo bikira ni afadhali zaidi mara 100 kuliko gumegume.
ReplyDeleteBasi tu niuoga kwan mtu anajua bikra akishajua utamu humkamati kwaiyo wengi wanaogopa
ReplyDeleteMabikra ni wazuri, ila kumleta mchezoni ni shughuli nzito,kikubwa hapa ni furaha ya nafsi,binafsi Siwapendi mabikra.
ReplyDeleteWw ujawai kuwa bikra
DeleteBikra sawa kwa mila zetu.ila binafsi hapana bora used.
ReplyDeleteTatizo sio Bikra tatizo nying feki
ReplyDeleteKarne hii watu weng swala hilo hatulizingatii coz ni ucmbufu !
ReplyDeleteUKISIKIA MAPAPA YA MJINI NDO HAO WANAWAKE WA 4. MAPENZI NI SANAA KAMA ZILIVYO SANAA ZINGINE AMBAZO UFANYAJI NA UFANISI WAKE HUTEGEMEA NA KIPAJI CHA MFANYAJI. WANGAPI NI MALAYA MBWA NA WALIOKUBUHU LAKINI KITANDANI NI WAMEJAA KERO (HAWAJUI MAMBO)? UBIKRA THAMANI YAKE ITABAKIA MILELE NA INA HESHIMA KUBWA HASA KWA MWANAMKE NDIO MAANA WALIOZIPOTEZA WANAJUTA NA KUTAFUTA ZA KUTENGENEZA NA BADO HAZIFIKII KIWANGO.
ReplyDeleteHAO WANAWAKE WALIKUA WANASEMA HIVYO KWA KUMUONEA WIVU MWENZAO NA KUMKOSA MWENZAO KWENYE UMBEA WAO PINDI ATAKAPO OLEWA.
VIJANA WAKIKE NA WAKIUME LINDENI UTU WENU MSISIKIRIZE UPOTOFU WA HAO WALIOPOTEA KIMAADILI.
HONGERA , MUNGU NAMUOMBA AKUZIDISHIE ELIMU YENYE MANUFAAA NA UZIDI KUWAELIMISHA, MUNGU AKUBARIK , HONGERA SANA KWA KUONGEA UKWELI
Deletemh mnapenda shotkat
ReplyDeleteMimi kama fundi haina maana hata kama nikimkuta bikra nitamfunza ili mradi akubali kufundishika na awe anafundika. I hire someone who can be trained and work for a job and not professional who can denite a jot
ReplyDeleteYote sawa ni maenzi ya mtu ila ukweli ni kwamba Bikra bado ni heshima na ina thamani kubwa (haswa kwa mwanamke)....kwani hamjasikia mara kuna demu kauza bikra yake bilioni kadhaa hela za madafu..... Uoga kwamba akiyajua mambo baadae atataka kwenda nje... itasababishwa na watu wanavyoishi na wenza wao.....
ReplyDeleteTatizo kwenye mapenzi tunakuwaga na list ndefu ya matakwa kwa wenza wetu... but i think all one needs is Love and understanding...... ukimpata mwenye mapenzi na muelewa ..... mengine yote yanabaki matamanio madogo madogo ambayo unaweza hata kuyaepuka yasikufanye kuenda nje ya ndoa....
Du kaazi mnayo
ReplyDeleteHeshima itabaki Heshima na Uhuni utabaki Uhuni. Moja ya vitu pekee na thamani utaeza map mtu wako katika mahusiano yenye malengo ni UTU wako. I THINK I WILL GO KWA MTU ALIE JIHIFADHIA UTU WAKE, na TUSIPOTOSHANE kama hukuweza fanya hivyo kuna mengine pengine unaeza fanya kuheshimu utu wako.
ReplyDeleteHuu ni lazima ushuhudia usomaji na kila mtu, nipo hapa kuruhusu ulimwengu wote kujua kuhusu mtu aliyeokoa uhusiano wangu na mtu huyu mkuu anaitwa Dr IZOYA. Hakika alifanya kazi nzuri kwangu kwa kumrudisha mpenzi wangu wa zamani ambaye aliniacha na kuahidi kamwe kurudi kwangu tena. Kwa hili, nimekuja kutambua kuwa kutoa maelezo ya Dk IZOYA kwa ulimwengu utafanya mengi mazuri kwa wale walio na nyumba zilizovunja au uhusiano kwa ajili yake ili kukusaidia kurekebisha uhusiano huo uliovunjika au ndoa yako. Unaweza kumfikia kupitia anwani yake ya barua pepe: drizayaomosolution@gmail.com au kumwita moja kwa moja kwenye [+12098373537]. Kuwasiliana naye na kuona jinsi tatizo lako litatatuliwa ndani ya 24hours. Pia mtaalamu katika mambo yafuatayo ...
ReplyDelete(1) Unataka kurudi nyuma yako.
(2) Unataka kukuzwa katika ofisi yako.
(3) Unataka wanaume / wanawake kukufuate.
(4) Unataka mtoto.
(5) Wewe ni mjasiriamali na unataka kushinda mikataba
(6) Unataka mume wako awe wako milele
(7) Unahitaji msaada wa kiroho.
(8) Umeshambuliwa na unataka kupona fedha zilizopotea.
(9) Weka talaka
(10) Kualika kwa mila ya fedha
(11) Chagua uchaguzi