BLOGS ZINAVYO MKERA RAIS KIKWETE"TETEENI NCHI NA SI KUIPONDA KWENYE BLOGS"

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Jakaya Mrisho Kikwete ameonyesha kukerwa na tabia ya baadhi ya watanzania wanaotmia muda wao mwingine kwenye mitandao ya kijamii Blogs kuiponda nchi yao, Akizungumza na Watanzania waishio nchini Pland alisema kwamba, "Teteeni nchi badala ya kuiponda kwenye mablogu", Rais Kikwete amesema wajibu mkuu wa Watanzania wanaoishi nje ya nchi ni kuisemea vizuri, kuihangaikia na kuitetea nchi badala ya kushinda kwenye mablogu wakiiponda, kuibeza na kulalamika.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa kuishi kwa Watanzania nje ya nchi kutaonekana jambo la maana zaidi ikiwa watatumia rasilimali na fursa wanazozipata ugenini kusaidia kubadilisha hali na maisha ya ndugu zao waliobakia Tanzania. Rais Kikwete pia amewaonya Watanzania hao wasije kuchanganyikiwa na kujichanganya wenyewe kwa kuiga tamaduni za kigeni kupita kiasi. Rais Kikwete alikuwa anazungumza na Watanzania waishio nchini Poland usiku wa jana, Alhamisi, Novemba 21, 2013, kwenye Hoteli ya Bristol mjini Warsaw ambako alifikia wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku nne katika Poland.

Aliwaambia Watanzania hao na familia zao: “Matumaini na matarajio yetu sisi tuliobakia nyumbani ni kwamba mtaisemea vizuri nchi yetu, mtaitetea nchi yenu, mtaihangaikia nchi na kuleta faida nyumbani. Ni jambo haliingii akilini kuwa baadhi yenu mnaweza kuishi hapa na kazi yenu ikawa ni kushinda kwenye mablogu mkilaumu nchi yenu wenyewe. Nchi mbaya, viongozi hawafai..mnapata faida 

gani. Mnazo nchi ngapi?”Rais Jakaya Kikwete akitafakari jambo juu ya utawala wake

Aliongeza Rais Kikwete: “Kuhangaikia nchi yetu ni wajibu wenu ambao hamwezi kuukwepa. Matumaini yetu ni kwamba mtasukuma mbele maslahi ya nchi yenu, mtatetea ustawi wa nchi yenu na ndugu zenu.

Fursa zilizoko hapa mnazijua wenyewe, sisi hatuzijui. Nyie ndio mnaishi hapa, sisi tuko mbali na hatuwezi sisi kutegemewa na kutarajiwa tufanye mambo ya hapa ambayo hatuyajui.”

Alisisitiza Rais Kikwete: “Mbona kazi za ma-Ngo’s mnazifanya vizuri bila kusukumwa ama kushawishiwa lakini kazi za kusaidia ndugu zenu hamfanyi? Kama hata hamwezi kusaidia ndugu zenu mnachangia nini nchi yenu?.

” Rais amesema kuwa kwa Watanzania waishio nje kuonekana wanajali na kutetea nchi yao kutasaidia kujenga hoja ya msingi kuhusu umuhimu wa kuanzishwa kwa uraia pacha (dual citizenship) ambao Watanzania waishio nje wanaulilia. “Mnaweza kuhalalisha hoja ya uraia pacha kwa kuwa watu wenye faida kwa nchi.”

Kuhusu ombi lao la uraia pacha, Rais Kikwete amesema kuwa ni wajibu wa Watanzania waishio nje kuongeza kasi ya kuchangia mjadala kuhusu suala hilo ili likubaliwe kuingizwa kwenye Katiba Mpya. “Rasimu ya kwanza ya Katiba ililikataa jambo hilo kwa sababu hili ni jambo lisilokuwa na ushabiki na upenzi mwingi nyumbani.

"Ujumbe wangu kwenu ni jipangeni vizuri kutetea hoja yenu hii. Saidieni mjadala wa jambo hilo badala ya kushinda kwenye mablogu mkijadili siasa na hivyo kusahau yenye maslahi kwenu.”

Kuhusu kuiga tamaduni za nchi nyingine na kusahau za nyumbani, Rais Kikwete aliwaambia kuwa inaelekea kuwa baadhi wachache wanaoishi nje ya nchi, wamejichanganya na kuchanganyikiwa kiasi cha kusahau mambo ya kwao. 
 Rais Kikwete alitoa kauli hiyo baada ya mmoja wa Watanzania kudai kuwa suala zima la mahari limepitwa na wakati na kuwa kutoa mahari ni sawa ni kuwauza watoto wa kike. Rais ambaye alionyesha kushangazwa na kauli hiyo, alijibu: “Msiige mambo ya kigeni kiasi cha kuanza kuchanganyikiwa.”
Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. nimeipenda ya kutolewa mahar kwa mabint.

    ReplyDelete
  2. Mahari ni kuendekeza dhiki tu kwa wanafamilia wachache tena wengi wao ni wale ambao hawakushiriki chochote katika malezi bora ya binti wala kutoa hata chapa ya kumsomesha. Ajabu wao ndo visebengo wakubwa wa kudai na kupanga kiasi cha i mahari huku wazazi waliohangaika wanaangalia Kwa mshangao. Yes huko ni Kama kuuza mtoto wako na hata hivyo visenti vya mahari havifikii hata robo ya matunzo ya binti wazazi walovyomtunza na wapumbavu wengine wanajitia kutoa mahari ili watese watoto wa watu kutwa kiwasimanga kuwapiga kuwaletea vimada ndani on the name of mahari how stupid is that?!

    ReplyDelete
  3. Na Raisi asituzingue mara ngapi wasomi wanahangaika kusoma nje wanapata elimu bora wakirudi huko ni balaa hawathaminiwi kisa tu hawana connection na wanasiasa wa ngazi za juu. Serikalini msijidanganye kurud eti kuboresha nchi Kama viongozi wenyewe walioko madarakani wameshindwa kuboresha nchi kwa kutumia vizuri madaraka na nafasi zao serikalini sie wachache tulioko nje tutaweza wapi wakija wasomi hao hao viongozi wanawapiga majungu mpaka wanakoma na nafasi za wasomi zinazibwa na mabongo lala watoto wa vigogo. So mr president if you don't have anything nice to say just say nothing at all give us a break and enjoy your visit and make it your private affair nobody will blame you for not talking to Tanzanians during your visit

    ReplyDelete
  4. Oh and before I forget hOw in the world does the president even gave time to read blogs that are bashing politicians???!!! Really??? Seriously???? So weird Is he running out of the responsibilitiintro run the government?! Or is he running out of important things to read and no he is blaming us for doing what he is exactly doing kushinda kwenye mablog tofauti mi ni mwananchi wa kawaida with bad economy I got nothing much going on so I got plenty of time to spend online but the president????!!!!! I find this so wierd and strange and he should be quite about this bit at least now we know what our president the dearest is doing and where he invest his time but this is disturbing

    ReplyDelete
    Replies
    1. ongea kiswahili kizuri kuma ww!!!!

      Delete
    2. A freak like you must be having learning disability so go fuck yourself your retarded freak na utakoma na hivi huko bongo hakuna madarasa ya learning disability people like you utaishia kuita watu kuma you low life trash bag

      Delete
  5. 6:48 am safi saaaana.

    ReplyDelete
  6. dokta msafiri kwenye hili nimekukubal sana.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad