DIAMOND: WEMA ASITEGEMEE KUOLEWA NA MIMI

Stori: Musa Mateja    
RAIS wa Wasafi Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’, juzikati alifunguka kuwa kwenye maisha yake ya ndoa atakayoingia siku chache zijazo, aliyekuwa mchumba wake wakamwagana na kurejeana hivi karibuni, Wema Sepetu asitegemee kuolewa naye.

Diamond ambaye ni staa wa Bongo Fleva aliyasema hayo mbele ya paparazi wetu Novemba 7, mwaka huu jijini Dar kufuatia kuulizwa anamchagua nani wa kumuoa kati ya Wema Sepetu na mchumba wake wa sasa, Penniel Mungilwa ‘Penny’.

Swali kwa Diamond liliibuka baada ya kuzagaa kwa tetesi kwenye mitandao ya kijamii kwamba yu mbioni kumvisha pete ya uchumba mmoja wa mademu zake.

Swali hilo lilimfanya Diamond afunguke kwa kusema kwamba anachokijua yeye na ambacho kipo kwenye mikakati yake, mke wake mtarajiwa ni Penny.

“Najua wengi wanahisi mimi ninaweza kuoa mwanamke zaidi ya mmoja kutokana na dini yangu kuruhusu lakini jambo hilo mimi silifikirii hata kidogo kwa kuwa kwenye maisha yangu nilishapanga nitaoa mke mmoja tu,” alisema Diamond.

Akaendelea: “Watu wanasema mengi juu yangu na Wema, wengi wao hawajui nafsi yangu inataka mwanamke yupi, ninachoweza kusema na watu wakasikia na kunielewa basi wajue kwamba Penny ndiye mke wangu, Wema asitegemee kuolewa na mimi.”

Diamond alikwenda mbele zaidi kwa kumwanika Penny kwamba ana sifa ya kuwa mke kwani ni mvumilivu sana na anaonesha upendo wa dhati kwake.

“Kwa maana hii basi hakuna mwanamke mwenye jina  kubwa wala sura nzuri zaidi ya Penny ninayeweza kumwita mke wangu. Najua kila mtu ana namna yake ya kuchagua ampendaye, ndiyo maana utaona watu wanasema hili mara lile, lakini hawajui nafsi yangu inataka mwanamke wa aina gani,” alisema Diamond na kuongeza:

Kama kuna demu anayejipa matumaini hayo basi asitegemee hata siku moja kwa sababu kuoa kwangu kutazingatia mke mwema na si bora mke, Penny pekee ndiye mwenye sifa za kuwa mke wangu,” alisema Diamond.

Juzi Ijumaa Wikienda lilimpigia simu Penny ili kutaka kupata maoni yake kuhusu tamko la Diamond, lakini muda mrefu simu hiyo ilikuwa ikiita bila kupokelewa.

Baada ya kumkosa Penny, Ijumaa Wikienda lilimtwangia simu Wema, naye kama Penny, simu yake iliita mara kadhaa lakini haikupokelewa.
Chanzo:Global Publishers

Post a Comment

20 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. eheheee u turn kimenuka mange mchokozi jamani ..anachokoza watu halafu wakimjibu anadai ni sinta au linda!
    nilikuwa fan wako mange ila leo sikuamini tena! unawachambaje wadada wa watu ? ni wivu au nini?

    ReplyDelete
    Replies
    1. halafu anajicommentia mwenyewe anadai ni mafans wake.sasa kama mtu kaenda south so what! na bado watu wanasonga mbele na kupaa utabaki hapo hapo .kana roho mbaya sana haka kadada.
      ila nilijua tu ile birthday party lazima aandamane.

      Delete
    2. Yeye mange Analea MUZUNGU kwa kuuza nguo barabarani .mpeni pole kutwa kupiga Picha barabarani kwake no way .mmebanana 2 bedroom

      Delete
    3. MANGE anakaa mbali na Beverly hills ila mumewe anatengeneza bustani Beverly hill na head quarter ya ofisi ipo Beverly hills .sasa Wana share gari yeye na mumewe .Mumewe anafanya kazi na wifi yangu .Wanakaa 2 bedroom na nasikia tiny apartment mumewe analala nika very expensive kazini .Income 3500 kwa Mwezi ndio maana mange anahangaika na nguo .sasaanajishaua nini?

      Delete
  2. dogo unafanya umalaya unawafanyia dada zetu ushenzi unataka kwa kutumia rungu ustaa wako,kwa tarifa yako ukitaka kujua kua mwanamke ni mvumilivu kiasi gan muonyeshe pesa,hata ukimletea mwanamke mwingine ndani hatoki,hata umpe kichapo cha mbwa mwizi habanduki,na hata ukimtimua atakugomea na kukwambia bora umwue tu,,huyo pen hajakupenda,,kinacho mng'ang'aniza hapo ni pesa na ustaa wako mbuzi pori wewe,amka ucingizin

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mwacheni alale,mi ningekuwa yeye ningewapotezea woooteeee nikaoa Demu ambae si famous

      Delete
  3. *WEMA *+ DIAMOND* =FOREVER and *FOR ALWAYS* WALA DOMO AJASEMA LOLOTE. UYO MANGE NI MUONGO ANATAKA COMT ZIWE NYINGI

    ReplyDelete
  4. kwan inakuaje nyie musiokua na la kufanya munamchagulia m2 mke?,ukiona hvo amegundua k2 kzur kutoka kwa penny,munachekesha xana kuacha yenu na kulazmisha upuuz,kwan akimuoa huyo wema nyie mutapata nn?,achen ufala coz munakera,shiiit!!!

    ReplyDelete
  5. Kwann Wema alisema anataka kuolewa na Diamond?embu tumuache mtoto wa watu apumzike bado anamachungu yakufiwa.Diamond oa mwaya mke wakukufulia,kupika nakukufanyis usafi.Pakumaliza nyege zako unapajua

    ReplyDelete
  6. WAJINGA NDIO WALIWAO KUTWA PENNY ALIKUWA ANAMNANGA DIAMOND KUWA NI MBAYA,MSWAHILI HAENDANI NA WEMA.LAKIN WEMA WA WATU HAKUJALI HAYO ALIMPENDA DIAMOND KWA MOYO WOTE.KWELI PESA SABUNI YA ROHO LEO HII DIAMOND KAGEUKA DHAHABU KWA PENNY.PENNY NAFSI INAKUSUTA JINSI ULIVYOKUWA UNAMCHIKIA DIAMOND.KUJA KUFANYA NAE MAHOJIANO KTK KIPINDI UKAJITONGOZESHA MPAKA DIAMOND AKAKUGONGA.NAKUMBUKA SIKU ILE ULIVAA KINGUO KIFUPI ILI UMTEGE NA MAPAJA YAKO ULIYOYACHIBUA KAMA KIIDONDA CHA MOTO.KWRLI NIMEAMINI SIZITAKI MBICHI HIZI

    ReplyDelete
  7. WAJINGA NDIO WALIWAO KUTWA PENNY ALIKUWA ANAMNANGA DIAMOND KUWA NI MBAYA,MSWAHILI HAENDANI NA WEMA.LAKIN WEMA WA WATU HAKUJALI HAYO ALIMPENDA DIAMOND KWA MOYO WOTE.KWELI PESA SABUNI YA ROHO LEO HII DIAMOND KAGEUKA DHAHABU KWA PENNY.PENNY NAFSI INAKUSUTA JINSI ULIVYOKUWA UNAMCHIKIA DIAMOND.KUJA KUFANYA NAE MAHOJIANO KTK KIPINDI UKAJITONGOZESHA MPAKA DIAMOND AKAKUGONGA.NAKUMBUKA SIKU ILE ULIVAA KINGUO KIFUPI ILI UMTEGE NA MAPAJA YAKO ULIYOYACHIBUA KAMA KIIDONDA CHA MOTO.KWRLI NIMEAMINI SIZITAKI MBICHI HIZI

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unakusumbuka heee Ooh diamond havutiii or kakaa kiswazi Swazi AMA kweli ukiwa na hela ukosi wa kuoa.hata Mimi Kama mwanaume wangu anafweza nitamyenyekeaaa Kama penseli anavyomnyenyekea nasibu,weraaaaaaa

      Delete
  8. Once a cheater always a cheater so penny jiweke tayari.

    ReplyDelete
  9. Porojo tu za bwana madomo mfalme wa zinaa na uzinzi wa hali juu na kujiweka hewani asikose kwenye headlines kumsema wema kwenye nyimbo eti kila siku magazeti sasa na yeye hapa na hii cheap publicity ni nini?! Si bora ya Wema yeye she is admitting she like spotlight kuliko wanafiki Kama huyu domo ka kiboko. Penny ameshajipigia hesabu za kuchuma Mali na so far so good hapo hatoki hata kwa winchi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nanyama za limbwata anamlisha nasikia.na keshawaambia sinzA mori atoki ngoooooo mtSubiri sanaaaa kashafika anasubiri ndoa.

      Delete
  10. Peeny hawez muacha diamond,gari yenyewe anayotumia ni ya Dai kupanda daladala mchezo?hahaaa lazima ang'ang'ane yeeey....Wema wil always be Wema no matter wat.mwenyewe yupo kimyaaaaaa nyie mnaweweseka tu..i lov her to d moon en back

    ReplyDelete
  11. wewe diamond hilo lipenny likafiri halijui hata uislam la nini mchukue wema muislam mwenzio hilo lipeni linavumilia hujalioa ngoja ulioe utaona cha moto

    ReplyDelete
  12. Nyie vipi nani kawaambia mapenzi yanajali dini wala kabila kafiri tygo yako mbavuuuuuuu lmao

    ReplyDelete
  13. Diamond siku hizi Hana dini,amejiunga na dini ya wavaa suti.kwahiyo uislam kwishney.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad