HII NDIO STORI KAMILI KUHUSU KUTEKWA KWA MSANII MATONYA HAPO JANA.

Mwanamuziki nyota wa muziki wa kizazi kipya usiku wa kuamkia Jumatatu alionja joto ya kiwe baada ya kutekwa na kusurubiwa kisha kunyang'anywa kila kitu pamoja na gari yake.

Mwanamuziki huyo akiwa kwenye viunga vya Club ya usiku ya Kibo iliyopo Tegeta Jijini Dar pamoja masisita du wakila bata ghafra kundi la watu watano lilimvamia na kumkamta msobe msobe hadi nje ya ukumbi pamoja na kumrukisha kichurachura huku wakina dada waliokuwa wamendamana nao wakilia kwa uchungu kwa kumuonea huruma.

Habari zaidi toka kwa chanzo chetu kilichoshuhudia timbwiri hilo kilisema kuwa chanzo cha tukio hilo ni kudaiwa kwa Matonya na mtoto wa mjini aliyefahamika kwa jina la Evance" Huyu Evance ni mtoto wa mjini na huwa anawakopesha pesa wanamuziki mbalimbali pamoja na wasanii wa bongo movie hivyo miezi ya hivi karibuni alimkopesha shilingi laki nne msanii huyo kwa madai kuwa hakuwa na pesa ya kula bata wikiendi ambapo baada ya kumkopesha msanii alianza kuzungusha kurudisha hali iliyomfanya Evance kuchukua hatua za kumfanyia unyambilisi huo" Kilisema chanzo chetu

Hata hivyo baada ya kumkamata msanii huyo Evance alimpelekwa Oysterbay ambapo aliiacha gari na simu kwa makubaliano atakapoleta pesa hiyo atapewa gari yake.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Aibu sn.wasanii tengenezeni saccos yenu

    ReplyDelete
  2. Auibujeee mbele ya warembo unadaiwa lol ukute ulikuwa unatanua balaa hpo ili uonekane unazo matokea yake polsiiii hahaha mnatia aibu wasanii wetu..kwan ela za sembe zimeishaje?

    ReplyDelete
  3. Auibujeee mbele ya warembo unadaiwa lol ukute ulikuwa unatanua balaa hpo ili uonekane unazo matokea yake polsiiii hahaha mnatia aibu wasanii wetu..kwan ela za sembe zimeishaje?

    ReplyDelete
  4. Hawajamla ndogo hao washenzi..??

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad