HUYU NDIO MTANGAZAJI WA REDIO MWENYE USHAWISHI MKUBWA KULIKO WOTE TANZANIA


Millard Ayo
Habari hii Imeandikwa na Bongo5.com
-------------------------------------------------
Jana tuliitisha kura za maoni Facebook na Twitter kutaka kufahamu kutoka kwa wasomaji wetu kuwa ni mtangazaji gani wa radio nchini mwenye ushawishi mkubwa na anayesikilizwa zaidi kuliko wengine.

Tanzania imeongea, na tunamtambulisha mtangazaji anayependwa zaidi, mwenye ushawishi kuliko wengine na ambaye kipindi chake husikilizwa zaidi, kuwa ni Millard Ayo aka ‘Mtu wa Nguvu’, wa Clouds FM.

Japo si kituo chake cha kwanza kuanza kazi, jina la Millard lilianza kufahamika nchini kupitia kipindi cha Milazo 101 cha Radio One. Sauti yake yenye mamlaka na ubunifu hewani, ulikifanya kipindi hicho kuwa maarufu kuliko vingine vya burudani katika radio hiyo inayomilikiwa na kampuni ya IPP.

Kuondoka kwake Radio One kulikuwa ni pigo kubwa lakini lenye neema kwa Clouds FM. Alihamia Clouds FM na kuanzisha kipindi kipya kiitwacho Amplifanya ambacho kilichukua nafasi ya kipindi cha nyimbo za kiafrika, Bambataa. Haikuchukua muda kipindi cha Amplifanya kikawa miongoni mwa vipindi bora kabisa Clouds FM. Kipindi hicho pia ni miongoni mwa vipindi vinavyoiingizia fedha nyingi redio hiyo na kumfanya Millard kuwa miongoni mwa watangazaji wa kituo hicho wanaolipwa mshahara mkubwa zaidi.

Leo hii Millard ni miongoni mwa watangazaji bora Tanzania na wanaosikilizwa zaidi. Si maarufu tu redioni bali pia ndiye mtangazaji wa Tanzania mwenye mashabiki wengi zaidi kwenye mitandao ya kijamii. Ana zaidi ya followers 67,000 kwenye Twitter huku Facebook akiwa na likes zaidi ya 145,530.

Umaarufu wake kwenye mitandao ya kijamii umemfanya ageuke brand na kuyavutia makampuni makubwa kama CRDB Bank, Fast Jet na mengine kudhamini kile anachotweet. Tweets zake tu zinamuingizia fedha huku akimiliki pia website yake binafsi yenye wasomaji lukuki na yenye matangazo mengi.

Kwa mshahara anaoupata, kazi ya uripota wa DSTV, ubalozi wa Fastjet, website yake, deal za voice-overs na mambo mengine, Millard anaingiza takriban ama zaidi ya shilingi milioni 10 kila mwezi.

Millard ni zaidi ya mtangazaji, bali ni mwandishi mwenye ‘pua ya habari’ (nose for news) huku akiongoza kwa kuja na angle za kipekee za habari zenye mvuto kwa watu (human interest stories) zinazokifanya kipindi chake cha Amplifaya kuteka matangazo ya jioni siku za wiki.

Pamoja na kupata mafanikio hayo, Millard ameendelea kuwa mchapakazi, simple, mtu anayejituma kutafuta habari hata sehemu za mbali kabisa, mcheshi na mtu wa watu.

Hakuna shaka kuwa, Millard ana mustakabali wa nguvu kwenye fani hiyo. Ni mfano wa kuigwa kwa watangazaji wengine na hazina kubwa kwa wazazi wake, Clouds Media Group na hata taifa kwa ujumla.
-Bongo5

Post a Comment

24 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Katika cku zote leo ndo umecopy point.

    ReplyDelete
  2. Eeeeeh ni bwana wa jokate huyo , wanafanya siri

    ReplyDelete
  3. umeulizwa!!? Acha umbea, au inakuhusu nini?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Aisee kama wameulizwa? Badala ya kukoment kilichoandikwa wanacomment mengineee. Naipenda sana sauti ya Millard yaani saaana

      Delete
  4. Kisabengo ka bao la kwanza...khaaaaaaa......! Anyway asante kwakutujuza.....

    ReplyDelete
  5. Me nampenda sana huyu kaka yani natamani kama angekuwa mpnz wangu, sema tu umri nimempita nina 34

    ReplyDelete
  6. Umri sio tatizo mpe agonge tu

    ReplyDelete
  7. big up ayoooooooooooooooooo

    ReplyDelete
  8. NAKUBALIANA NA HABARI HII ILA CLOUDSFM HAWASIKIKI HEWANI KUPITIA MTANDAONI ILI KUWAPA FURSA WASIKILIZAJI WA KITANZANIA WALIOKO NCHI ZA NJE. UONGOZI/MANAGEMENT YA CLOUDSFM NI WAZEMBE KIASI CHA KUACHIA WAPINZANI WAO KUSHIKILIA WASILIZAJI WA KIMATAIFA. TUNAISHI ULIMWENGU WA TECHNOLOGY YA KISASA LAKINI HAPA RUGE NA TEAM NZIMA YA UONGOZI WA CLOUDSFM NAMPA ALAMA YA UFAULU YA DIVISION 5

    ReplyDelete
    Replies
    1. mbona sisi tuko nje ya Africa lakini tunawapata au huna link?

      Delete
    2. NILIKUWA NAWAPATA KUPITIA WEBSITE YAO NA PIA KUPITIA USTREAM LAKINI SIKU HIZI HUA WANAPATAIKANA KWA NADRA SANA NA UKIBAHATIKA KUWAPATA THEN WITHIN FEW MINUTES WANAKUA OFFLINE... JE WEWE MDAU (07:13 AM) HAPO JUU UNAWAPATA KUPITIA LINK GANI MANAKE KWANGU NI TATIZO SUGU LA MUDA MREFU

      Delete
  9. huyu jamaa anaweze sio sir zile n level zingine

    ReplyDelete
  10. Cloudsfm mna-bore mnashindwa hata na Radio za Mtwara let alone EastAfricaRadio ambao ni wapinzani wenu wakubwa. Wanasikika Crystal Clear kupitia mtandaoni that's means mngekua level nyingine kama mngewadaka fans wenu walioko nje ya Tanzania lakini hapa mmeziba macho na masikio.

    ReplyDelete
  11. Mbona me nipo sweédén napata kwa online. Pengine computer zenu za viwango vya china

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kazi kwelikwel,we utakuwa mhaya.

      Delete
    2. WEWE MDAU @04:44 SWEEDEN UNAONEKANA MBULULA.... walewale division 5 wanaozunguziwa huko nyumbani... DO YOU KNOW WHAT SORT OF COMPUTER I USE OR FOR THIS CASE WHAT INTERNERT SPEED I'VE GOT? FOR YOUR INFORMATION 90% OF ALL COMPUTER COMPONENTS IN THE WORLD ARE MADE FROM CHINA THE ONLY DIFFERECE IS WHERE ARE THESE COMPUTERS ARE GOING TO BE SOLD. JE UNAJUA NIKO WAPI? TATIZO HAPA NI KWAMBA CLOUDS FM NI WAZEMBE KUTOA HUDOMA ZAO KWA NJIA YA MTANDAO ....

      Delete
  12. sikushangazwa na hizo taarifa yule jamaa noma.

    ReplyDelete
  13. nimeshangazwa na hizo taarifa kwani nilijua kuwa u ndugunaizeshen utachukua nafasi so nawakubali

    ReplyDelete
  14. anastahili kwakweli.

    ReplyDelete
  15. Me chijui nchwahli vijiuuri ntafachie kisweedish

    ReplyDelete
  16. weupokijijini then unasema sweden!wembulula kweli

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad