JAMAA ASHINDWA KUVUMILIA AMWANDIKIA BARUA DEMU ANAE MPAGA LIFT KILA SIKU NA KUITUNDIKA JAMII FORUMS

Huu ni waraka wangu kwako wewe mdada ninaekupaga lifti asubuhi. Nimevumilia sana mpaka nimechoka aisee maana imekua ni kero sana. Toka tuanze biashara ya kupeana lift imekua tatizo sana mpaka najuta kukufahamu. Sina uhakika sana kama wewe ni member humu Jf,
But hata kama sio member, najua hukosi kufanya kazi na Member wa humu ambae sina shaka atakufikishia ujumbe.

1) Kwanza kabisa mimi ni mume wa mtu. Biashara ya wewe mke wa mtu kunipigiaga simu asubuhi asubuhi na kuniamsha siitaki. Mimi ninaamka kwa ratiba zangu, simu unazinipigiaga kuniamsha hua zinanipa wakati mgumu sana kujitetea kwa my wife wangu.

2) Sipendi kabisa tabia ya mimi kukusubiri wewe getini kwako. Mimi sio dereva wako, hujaniajiri wala kwa lifti ninayokupa sifaidiki chochote zaidi ya kua tu wewe ni jirani yangu, nakuonea huruma ukigombea daladala asubuhi. Wewe unatakiwa uwe umeshajiandaa asubuhi na nikukute getini. Cha ajabu siku hizi nikishafika getini mpaka nikupigie simu ndio utoke. Jana umeniuzi sana eti ulishajiandaa ila ukawa unasubiri nikupigie simu.


3) Kunichagulia nyimbo za kusikiliza kwenye gari sipendi. Mimi ni mpenzi mkubwa wa Bongo Flava, hizo R&B zako kama unazipenda sana basi ka-dowload ukasikilize nyumbani kwako/kwenu.

4) Inaendana na namba (3) pale juu. Hua napenda sana kusikiliza Magazeti redioni asubuhi. Sipendi kabisa tabia ya wewe kujifanya ndio controller wa radio ya gari langu. Kupitia Magazeti radioni ndio najua mambo mbalimbali yahusuyo Siasa, Mchezo n.k. kabla sijafungua JF.

5) Mimi sio mpenzi sana wa AC kwenye gari, napendelea kitu Natural Air. Sijui kwanini hujalifahamu hili. Eti ukiingia tu unaanza kupandisha Vioo na kuwasha AC, huangalii kama kio changu pia kimepanda ama vipi. Wewe unatakiwa unifuatishe mimi na sio kujifanyia mambo utakavyo.

6) Kuna mafuta mengine unapaka yananikera kwelikweli harufu yake. Nafikiri hata huko kazini kwenu wanaipata fresh.

7) Unaongea mno aisee, yaani kama umemeza kanda. Yaani njia nzima unaongea wewe tu. Binadamu tumepewa mdomo mmoja na masikioo mawili ili tuongee kidogo lakini tusikilize sana, lakini kwa wewe mdada sio hivyo aisee. Unahdithia mastory ya kazini kwenu ambayo hayanihusu, mi ya nini?? 

8) Ukiwa na mimi ujue ni straight to Mjini. Mambo ya kuniambia eti tupitie sijui Steers au Jamaa fast Food kuchukua vitafunwa mi siiizimkii aisee. Pengine wewe umezoea kuchelewa kazini, basi tusicheleweshane. Sometimes nakua na viporo kibao kazini nahitaji kuwahi kuvimalizia, we unaanza kuzusha safari zako za asubuhi asubuhi, why we mwanamke??

9) Hivi gari umejifunzia wapi?? Sijawahi kukuona ukiendesha na wala hujawahi kunionyesha hata leseni yako, leo unaniambia siku moja moja niwe nakuachia uwe unaendesha wewe, ili iweje?? Unataka kujifunzia gari kwangu? 

10) Mimi ndio dereva, najua wapi ni-over take na wapi nipite wapi. Cha ajabu hata speed unanipangia wapi nikimbize na wapi niendeshe slow, wewe umeomba lifti tu, kaa subiri ufikishwe kazini kwako, biashara ya njiani naijua mimi. Mimi nimeanza kuendesha gari toka unasoma shule ya msingi so sipendi ujifanye mwalimu wangu wakati naeendesha.

11) Gari yangu sio saluni kwenu. Eti unaweka miguu juu, mara sijui unakata kucha, halafu hizo kucha zinaporukia wala hujishughulishi kuzitafuta. Matokeo yake tunataka kuvunjiana ndoa. Halafu ukifungua kioo cha kujiangalia cha "kizuia jua" uwe unakirudishia baada ya kukitumia. Pia sipendi ukae kwa kulaza siti kwa nyuma. We asubuhi asubuhi umeamka bado una energy za kutosha halafu unakaa kwa kulaza siti, hizo kazi zitafanyika kweli??

12) Tena sipendi uwe unaongea kwa kunipiga piga begani au mkononi, hua naumia na pia naweza kupoteza control ya sterling. 

Haya ni baadhi tu ya ambayo unayafanyaga wewe abiria wangu naekupaga lifti ambayo yananikera sana asubuhi. Nashindwa tu kujua nianzie wapi kukuambia ukweli navyokereka.

Chanzo:Jamii Forums

Post a Comment

35 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. yaaan wewe kaka nimtu mzuriii mnooo nakuambia .una huruma ila huruma ita kuja kuvunja ndoa yako.mpite au mpe kubwa mkeo hataki mwambie ukwelii na mwenyewe mwingine ukindika humu at ona utanii ila ume nifurahisha sasa wadada mkipewa lift loh muwe na kiasi kwa kila kitu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yeah kaka wa wstu anahuruma na upendo alikua akimuonea huruma wanatoka mtaa mmoja na wt wanaenda town.anamuhurumia asipate shida ya madaladala na ndo ukute wanakaa gongola mboto au mbagala au kimara uwiiiii.lkn mdada kashindwa kua muungwana na kakosa heshima kbs.kwanza angetaka lift idum angekua anakaa seat ya nyuma kwa adabu.anaamka mapema anakutwa njee.apunguze mdomo kujishaua na ujuaji mwingi.apige kimya iwe ni swali jibu stop.wsla brother asingeboreka looool lkn kwa hp akuuuuvkska kaa mbali na uache kutoa lift kwa faida yk.byeeeeee.

      Delete
  2. Mbavu zangu hahah. .uwii. mm lift no. Siwez jua ratiba ya mwenye gari. Lakin hata mamen nao ukiwapa lift wanaongea mno. Sometimes mtu hata huji skii kuongea inabidi utoe fake smile tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. nakufa kwa kucheka yaani nimecheka hii stori mpaka basi kaka unayataka mwenyewe kwani ukiamka asubuhi na kuwasha gari lako moto kwenda unakokwenda atakuuliza nani? unayataka mwenyewe kwanza na mume wake naye yuko wapi? kuna mijanaume mingine nayo fala kweli mke wako anapewa lift kila siku asubuhi jamaa liko wapi sijui? au ndio limeridhika mke wake kupelekwa na mwanaume mwingine kazini? ukitombewa mkeo utalia au utacheka? bongo ina mambo

      Delete
  3. Kaaaaaazi
    Kwelikweli,.huu ujumbe unawahusu wengi jamani,bila Shaka watajirekebisha,

    ReplyDelete
  4. Mwambie ukweli sasa au unamwogopa je asipoupata huu ujumbe

    ReplyDelete
  5. watu wanakera kweli. Bora umemwambia. Na isiishie jf tu. Mwambie hata ana kwa ana

    ReplyDelete
  6. Mambo hayo yapo hapahapa bongo ila kwa7bu ujumbe umefika watajilekebisha

    ReplyDelete
  7. Ni kwel wanapenda mteremko

    ReplyDelete
  8. kama vp mtombe tu

    ReplyDelete
  9. usimpitie,usimpigie simu,wala usimtafute,hakuweki mjini,just follow mambo yako jua wewe ni mume wa mtu.mimi nakupa ushauri ni kiwa km mwanamke mwenye ndoa pia.alafu wewe ni mwanume bwana mbona domo zege mpe live khs yote hayo kuwa upendi kabisa.

    pole

    ReplyDelete
  10. jamani pole yake

    ReplyDelete
  11. Hicho kidada kitahira kwel

    ReplyDelete
  12. Kizungu cha wabongo cha "my wife wangu" hahahahahahahaa. Hii inamaanisha "mke wangu wangu" alafu jamaa shoga, kwanini yeye hakumwambia demu uso kwa uso kama dume au kumwambia wakati huyo demu anampigia simu? Bwege.

    ReplyDelete
  13. Madada duu wabongo hao kazi kwl kwl dah ni nomah aisee...but message sent atajirekebisha

    ReplyDelete
  14. nadhan mwanaume wa kweli anamweleza wazi bila kuuma maneno. sio kutuletea sisi hapa!!

    ReplyDelete
  15. STORY YA KUTUNGA HII SI KWELI ALTHOUGH UNAWEZA KUPATA MTU ANA TABIA KATI YA HIZO SI ZOTE.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hii ni stor ya kutunga haswaa ila ina ujumbe coz watu wa aina hii wapo ingawa hakuna mtu anaweza kuwa na tabia zote hizi tajwa. dawa c kulalamika ni kuacha kutoa lift basi kwani lazima?

      Delete
    2. hii story ni ya kutunga ila kuna watu wanatabia kama hizi inakera usipime mimi naishi maflat tunagari moja asubuhi hubby ananishusha anaenda na gari jioni tunapitiana ndio ratiba yetu kuna hilo limama jirani yetu linakera hatari kwanza utalikuta chini kasimama pembeni ya gari anatusubiri tukishuka wenyewe na vicheko vyetu na watoto wetu wanatusindikiza ataanza hapo hapo kuongea maneno yake yote anayoongea ni negative ataanza nyie foleni barabarani mbona mnachelewa, tukiagana na watoto wetu na yeye anaingilia maongezi yetu na wanetu na dada, hata tukipanda kwenye gari mimi na mume wangu tuko mbele tunaongea habari zetu ataingilia na kujifanya mshauri anajua ushauri wa kila jambo tutakalo sema yeye na mume wake wameshachakazana na ndoa yao huko sisi wenyewe bado tunamalovidavi ndoa yetu changa basi litaleta stori za mume wake jinsi gani walivyokwaruzana akatufanya tukawahatuongei tena mimi na hubby tukiingia kwenye gari tunasikiliza radio na kusmiliana tu ikawa inatunyima raha ikabidi tulifanyie mkakati wa kuliambia tunapita njia nyingine samahani hatukupi lift likatununia ikawa ugomvi sasa hivi hata salamu halinipi likafie huko usininyime raha na mume wangu kapande daladala na mzee wako ishii

      Delete
    3. Hata we yk yakutunga kbsaaa bora ya hy kaka ni yakweli na kashauriwa vzr.

      Delete
  16. Ningekuwa mimi ningembakilia mbali tena humo humo kwenye gari

    ReplyDelete
    Replies
    1. hii kali kwii kwii kwii nimechekaje sasa

      Delete
    2. Kaka pooole.ww mwanaume bhanaaa chagua ndoa yk kua na amani au kumpiga chini hy mama.unapata shida ya nn washa gari chapa mwendo.........akiona kimya ck 2 atakufuata gate kwako mwambie siendi mjini now na family issues.mwendo huo huo.kila ck akipiga potezea usipokee.msg ucjibu.huo ni ujumbe tosha ataaacha kukufuatafuata bhanaaaa.be serious.wala haina haja ya kupoteza muda kumweleza kitu.mtajibishana vibaya bure hp au akaongea mambo meeeengi mtaani kwenu ikakuvunjia heshima.na huo utaratibu wa ratiba za lift kila ck kwa hy mwanamke kwann uliilea.hk njian watu c watajua ndo mkeo atii!!!!.km na leo umempa bc iwe mwiiiiiishoooooo.tusikusikie tn unaleta suala hili humu ndani.tuletee matokeo ya kupiga chini sawa kaka.na wala usikubali uzinzi na hy dada ht km anajirahisisha.muheshimu mkeo,pia heshim watoto wk.zaidi ya yoooote usimtende MUNGU wk dhambi.am a married woman.hope umeelewa.kazi njema.

      Delete
  17. Story yakutunga.kama huna chakuandika acha illusions.

    ReplyDelete
  18. kama vp mpotezee hana akil mshenzi kabisa kata hata vibao hilo dada

    ReplyDelete
  19. mimi ushauri wangu kwa huyo kaka hii iwe ni story ya kutunga au la! mm sijui ni hivi kaka huruma yakao isizidi kiasi maana ni dhambi pia, wewe usipokee tena sm yk pia mweleze mkeo ukweli juu ya lift unayompa huyu mama na kero zake.Usimfiche chochote mkeo kwani siku zote ukweli utakuweka huru,mkatie huyu mama mawasiliano kabisa.Usimwogope maana yeye sio anayekupa pumzi na yeye sio barabara useme utakosa mahali pakupita,usiendekekeze matatizo heri lawama kuliko karaa, ni hayo tu eti unampitia unampigi honi au unampigia sm ni bosi wako nini!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ukute home kwako ck ukitoka na mkeo akichelewa kdg kutoka unammind sn.lkn hy mwanamke unaenda kumsubiria gate kwake stoke aaaaaaaghhhhhhh hy c sawa bhanaa wifi wk anahaki ya kuchukia bhanaaa badilika pls km nilivyokushauri hp juu mpoteze akikufuata unamwambia hauendi mjini una family issues.ungekua ni mkaka hauna mke na hy dada hajaolewa walauuuu lkn kwa status yk noooooooooo man.badilika faster.

      Delete
  20. Kwi Kwi! Kwi! .........inanihusu kinoma. Kuna jamaa mmoja tunakaa naye kutwa. Lakini tunasoma pamoja chuo Fulani hapa dar yaani ni classmate, jamaa huwa anatoka kwenye lecture dk5 kabla haijaisha, kisa eti asinipe lift msela wake, kinachoniudhi akifika home anaanza maswali ooh, vipi lecturer katangaza test? Na mengine kibao ya kisenge tu! Alafu ananiomba summary zangu eti amalizie! Jamani huyu msenge si Anatoumbwa mkunduni huyu? Kuma lamamaake! Kirav4 chenyewe kinakohoa mimoshi lukuki! Kama kimepigwa na bomu! Mi maskini lakini Jeuri kinoma mbwa nyie!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwann umtukane jamaa wa watu???.yawezekana na ww ulikua KERO SANA kwe lift yk hakutaka kukwambia kwa maneno lkn uisome no.kwa vitendo.akikuuliza hbr za class km hautak kumpa c unamwambia haujui yann matusi bhaaanaaaa.acha hizo tusikosee MUNGU kwa vinywa vyetu kiasi hicho.potezeyaa km yy bc.matusi hayajengi.

      Delete
  21. kiukweli kaka hv sio vizuri hata mm nakuunga mkono sisi wasichana sijui tukoje tena hasa hao wanaojifanya matawi ya juu unatudhalilisha dada mawanawake wenzio na pia ushauri wangu mm kaka bora nusu shari kuliko shari kamili ww muimu usimpitie wala kumpigia simu akigombania basi atakuwa na adamu huruma isije ikakumboza kaka angu achanchana nae

    ReplyDelete
  22. Mnaosema story ya Kutunga mna vigezo gani? Ye jamaa kasema huyu mdada yupo, nyinyi mnasema hayupo wala hii issue hai-exist, kwani mnawajua watu wote humu duniani??

    ReplyDelete
  23. Bhanaaaa dada asikukere mume wa mtu babu eeee ngoja akapande dala daladala ili konda na dereva wampeleke steers hahaaaaaa.

    ReplyDelete
  24. Huu ni lazima ushuhudia usomaji na kila mtu, nipo hapa kuruhusu ulimwengu wote kujua kuhusu mtu aliyeokoa uhusiano wangu na mtu huyu mkuu anaitwa Dr IZOYA. Hakika alifanya kazi nzuri kwangu kwa kumrudisha mpenzi wangu wa zamani ambaye aliniacha na kuahidi kamwe kurudi kwangu tena. Kwa hili, nimekuja kutambua kuwa kutoa maelezo ya Dk IZOYA kwa ulimwengu utafanya mengi mazuri kwa wale walio na nyumba zilizovunja au uhusiano kwa ajili yake ili kukusaidia kurekebisha uhusiano huo uliovunjika au ndoa yako. Unaweza kumfikia kupitia anwani yake ya barua pepe: drizayaomosolution@gmail.com au kumwita moja kwa moja kwenye [+12098373537]. Kuwasiliana naye na kuona jinsi tatizo lako litatatuliwa ndani ya 24hours. Pia mtaalamu katika mambo yafuatayo ...
    (1) Unataka kurudi nyuma yako.
    (2) Unataka kukuzwa katika ofisi yako.
    (3) Unataka wanaume / wanawake kukufuate.
    (4) Unataka mtoto.
    (5) Wewe ni mjasiriamali na unataka kushinda mikataba
    (6) Unataka mume wako awe wako milele
    (7) Unahitaji msaada wa kiroho.
    (8) Umeshambuliwa na unataka kupona fedha zilizopotea.
    (9) Weka talaka
    (10) Kualika kwa mila ya fedha
    (11) Chagua uchaguzi

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad