JUMA KASEJA ASAINI MKATABA WA MIAKA MILILI YANGA KWA MILIONI 40

Golikipa hodari nchini, Juma Kaseja jana(Novemba 08,2013) amesaini Mkataba wa miaka miwili na klabu ya Yanga SC  kwa Shilingi Milioni 40.Kaseja amesainshwa na vigogo wa Usajili wa Yanga, Abdallah Ahmed Bin Kleb na Seif Ahmed ‘Magari’ mbele ya Meneja wake, Abdulfatah Salim Saleh Ilala mjini Dar es Salaam.

Kaseja sasa anakwenda kuungana na makipa wawili aliowahi kufanya nao kazi Simba SC, Ally Mustafa ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’.

Hii inakuwa mara ya pili Kaseja kusajiliwa Yanga, baada ya awali kusajiliwa mwaka 2009 akitokea Simba SC ambako baada ya msimu mmoja wa Mkataba wake kumalizika akaachwa na kurejea Msimbazi.

Kaseja aliachwa Simba SC mwishoni mwa msimu kwa madai kiwango chake kimeshuka na amelazimika kuukosa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Bara, ingawa sasa baada ya kumwaga wino Yanga anarudi kazini Januari.

Kikubwa kilichoisukuma Yanga SC kumsajili kipa huyo ni uzoefu wake katika michezo ya kimataifa na inataka inufaike naye katika Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.

Juma Kaseja aliibukia sekondari ya Makongo, Dar es Salaam ambako aliitwa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys mwaka 2001 chini ya kocha Mnigeria, Ernest Mokake aliyekuwa akisaidiwa na mzalendo, Juma Matokeyo, wote sasa marehemu.

Mwaka huo huo alisajiliwa na Moro United aliyoichezea hadi mwaka 2003 alipohamia Simba alipopiga kazi hadi 2009 akaenda Yanga na kurejea mwaka mmoja baadaye ambako alifanya kazi hadi mwishoni mwa msimu uliopita alipotupiwa virago.


Read more: http://peruzibongohabari.blogspot.com/2013/11/juma-kaseja-asaini-mkataba-wa-miaka.html#ixzz2kAr1ANsO
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad