KIBADENI:NATENGENEZA SIMBA YA MWAKANI ..ACHENI LAWAMA

Dar es Salaam. Kocha mkuu wa Simba, Abdallah Kibadeni amewashangaa wanaomtupia lawama sasa wakati jukumu lake lilikuwa kutegeneza kikosi bora cha msimu ujao.
Kauli hiyo ya Kibadeni imekuja baada ya hivi karibuni baadhi ya viongozi na mashabiki kumshutumu yeye na benchi lake la ufundi kufuatia timu hiyo kunyukwa na Azam 2-1 na kutoka sare 1-1 na Kagera Sugar na kushuka hadi nafasi ya nne katika msimamo.
Matokeo hayo yamesababisha baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu ya klabu hiyo, hivi karibuni  kuanza mazungumzo na kocha wa Gor Mahia ya Kenya, Bobby Wiliamson kuja kuchukua jukumu lake.
Akizungumza na gazeti hili jana Kibadeni alisema, “wote wanaolitupia lawama wanapaswa kukumbuka malengo na mikakati niliyotoa wakati nachukua jukumu hili mbele ya viongozi wote wakiwamo viongozi wa matawi.
“Mikakati yangu ilikuwa ni kutengeneza kikosi kwa ajili ya Ligi Kuu msimu ujao, lakini pamoja na yote hayo namshukuru Mungu, pia tumeweza kufanya vizuri katika mechi za mzunguko huu ambapo hadi sasa tupo katika nafasi nzuri ya kuwania ubingwa.
“Wale wote wanaotushutumu kuwa tumeshindwa kazi wanapaswa kulitambua hilo, mikakati na malengo yetu yanalenga ubingwa msimu ujao, pia tunataka mafanikio msimu huu,” alisema Kibadeni ambaye alitua Simba akitokea Kagera Sugar.
Simba wavunja viti 195
Thathimini iliyofanywa na Serikali imeonyesha mashabiki wanaodhaniwa wa Simba waling’o viti 195 kwenye Uwanja wa Taifa wakati wa vurugu zilizotokea wakati timu hiyo ilipolazimishwa sare 1-1na Kagera Sugar uwanjani hapo wiki iliyopita.
Vurugu hizo zilisababisha askari kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya mashabiki waliyohudhuria uwanjani hapo.
Habari za ndani kutoka kwa mmoja wa viongozi wa Serikali ambaye hakupenda kuandikwa gazetini zinaeleza kuwa ukarabati wa kiti kimoja uwanjani hapo unagharimu dola 100 (sawa Sh 160, 000) hivyo hadi kukamilika ukarabati wa viti 195 vilivyong’olewa itagharimu dola 19,500 sawa na zaidi ya (Sh 31. 2 milioni).
Kaimu katibu mkuu wa TFF, Boniface Wambura alisema tayari Bodi ya Ligi (TPL) imeanza kushughulikia suala hilo sambamba na kupitia ripoti ya mechi hiyo kwani wao ndiyo wanahusika na ligi na itakapokuwa tayari hatua zitachukuliwa dhidi ya wahusika.
_Mwananchi

Click like below to Win as fan of the Day.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad