KIGUGUMIZI cha serikali ya Rais Jakaya Kikwete katika kuchukua uamuzi mgumu kwenye masuala mazito kimemwibua Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, akisema nchi inakosa viongozi jasiri wenye kusimamia utekelezaji wa mambo waliyoamua katika sekta mbalimbali.
Alisema nchi ina tatizo kubwa la uswahili mwingi wa kukaa kutekeleza kile kinachotakiwa kufanyika kiasi cha kuwafanya kila mtu kuanza kulalamika.
“Hapa mnaamua bila kutekeleza, watu hawana ujasiri wa kufanya maamuzi magumu, ni lazima awepo mtu mmoja wa kuamua si wote kulalamika lalamika.
“Tukishakubaliana mambo ni lazima yafanyike. Ni lazima tuondokane kuwa nchi ya kulalamika kuanzia kiongozi wa juu mpaka mwananchi,” alisema.
Lowassa aliyasema hayo jana bungeni wakati Bunge lilipokaa kama Kamati ya Mipango ili kujadili Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2014/16.
Lowasa ambaye ni mbunge wa Monduli (CCM) alisema kuwa ni vema serikali ingekuwa na mipango michache yenye kutekelezeka na tija kwa taifa.
Aliongeza kuwa kama angekuwa kiongozi wa serikali angejikita kwenye vipaumbele vitatu ambavyo ni ajira, Reli ya Kati na elimu kuliko kuwa na vipaumbele vingi visivyotekelezeka.
Alibainisha kuwa tatizo kubwa linaloifanya serikali ishindwe kufanya vizuri kwenye maeneo mbalimbali ni kujiwekea vipaumbele vingi huku rasilimali zake zikiwa chache na wakati mwingine zile zinazopatikana hazitumiwi vizuri.
“Vipaumbele vingi mno utekelezaji wake ni tatizo, tungechagua vichache, tukavisimamia na tuvitekeleze. Tukiwa navyo vingi kwa wakati mmoja hatuwezi kuvitekeleza vyote, tuanze na vichache tukivimaliza tunavifuata vingine.
Ajira
Alisema kama angekuwa kiongozi wa serikali angeanza na kipengele cha ajira ambacho kinakwenda sambamba na mipango.
“Huwezi kupanga bila kuzungumza habari za ajira, tukiri kuna Watanzania wengi wamemaliza kidato nne, sita, chuo kikuu, vyuo, darasa la saba walioko mitaani hawana ajira.
“Tusipowashughulikia, watakula sahani moja na sisi, tusipoangalia yatatufika yale ya wenzetu ya Afrika Kaskazini, si lazima yatufike lakini hawa wasio na ajira watakula sahani moja na sisi,” alisema.
Lowassa aliongeza kuwa wanapaswa kuangalia suala la ajira kwa umakini sana, kwamba inawezekana sana kila mmoja akifanya wajibu wake.
Alibainisha kuwa nchi ya Hispania ilikuwa na tatizo kubwa la ajira mara baada ya kutokea kwa mdororo wa uchumi duniani lakini walikaa chini na kuamua kulitafutia ufumbuzi.
“Wale wenzetu waliamua kila mwekezaji anayekwenda kwao sharti kubwa ni lazima atoe ajira kwa vijana, baada ya miaka miwili walipiga hatua kubwa sana, lazima tuliangalie suala hilo kwa umakini mkubwa sana,” alisema.
Lowassa aliwapongeza Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatuma Mwasa na Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Elibariki Kingu kwa kuamua kuangalia suala la ajira kwa vijana.
Alisema viongozi hao wamethubutu kwa kuwachukua vijana waliomaliza chuo kikuu na kuwapa matrekta na kuwatafutia ardhi ya kilimo ambapo hivi sasa wanaendesha shughuli zao vizuri.
Aliongeza kuwa Benki ya CRDB nayo imeanza kutoa mikopo kwa vijana wanaomaliza vyuo vikuu kwa kuchukua vyeti vyao kama dhamana.
“Wizara, watendaji na viongozi mbalimbali kila mtu angetimiza wajibu wake katika hili jambo nina hakika tatizo la ajira lingepungua kwa kiasi kikubwa,” alisema.
Elimu
Alisema mjadala wa elimu usipuuzwe kwa kuwa lipo tatizo la msingi katika elimu ya Tanzania na hatua zinazochukuliwa hazitoshi.
Aliongeza kuwa alitegemea ripoti ya tume iliyoundwa na Waziri Mkuu kuchunguza matatizo ya elimu hapa nchini ingetolewa bungeni na ikajadiliwa ili wabunge wajue matatizo yaliyopo na namna ya kuyatatua.
“Haitoshi kuchukua wanafunzi wengi kumaliza chuo kikuu wakati akienda kwenye soko digrii anayoipata haifai, hawezi kupata kazi kwa kuwa aina ya elimu aliyoipata haimuwezeshi kuajiriwa.
“Wenzetu Ujerumani wanagawa digrii nusu inatokana na ujuzi wa kitu fulani na nusu iliyobakia inatokana na elimu aliyoipata hivyo kila kundi hapa lina uhakika wa ajira,” alisema.
Alisema kelele zinazopigwa na wananchi juu ya matatizo ya elimu zinapaswa zisikilizwe na uitishwe mjadala wa jambo hilo ili Tanzania isiachwe na jumuiya mbalimbali ikiwemo ile ya Afrika Mashariki.
“Tukiacha mambo haya yaendelee kwenye elimu yetu tutakuwa wababaishaji na tutaachwa katika soko la ajira duniani,” alisema.
Reli ya Kati
Alisema kipaumbele chake kingine ni kuboresha reli ya kati ambayo itachangia kupunguza uharibifu wa barabara zinazojengwa kwa gharama kubwa na serikali.
Lowassa alimpongeza Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli kwa jitihada zake za kusimamia ujenzi wa barabara ambazo hivi sasa zimekuwa zikiharibika kwa kiwango kikubwa kutokana na magari kupitisha mizigo mikubwa.
“Maroli yaliyopaswa kusafirishwa kwa treni hivi sasa yanasafirishwa kwa magari, hapa ni lazima barabara ziharibike, naomba muangalie kwa haraka sana Reli ya Kati,” alisema.
Lowassa pia alimpongeza Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harisson Mwakyembe, kwa jitihada za kutafuta ufumbuzi wa foleni za jijini Dar es Salaam ambazo zinachangia kuzorotesha ukuaji wa uchumi.
“Foleni Dar es Salaam it’s a nightmare (jinamizi), muda tunaokaa katika foleni ukiujulimsha ni mrefu sana serikali ni lazima mchukue hatua sasa, si suala la kusubiri,” alisema.
Afrika Mashariki
Lowassa aliitaka serikali kuacha kugombana na marais wa Rwanda, Paul Kagame, Uhuru Kenyatta (Kenya), Yoweri Museveni (Uganda) ambao wameamua kushirikiana na Sudan katika masuala mbalimbali.
Asema Tanzania ijielekeze zaidi kuimarisha ushirikiano na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Congo ambako kuna manufaa makubwa zaidi.
Sumaye kufunguka
Wakati huo huo, Waziri Mkuu mstaafu wa Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye, ambaye ni mmoja wa watu wanaotajwa kuutaka urais mwaka 2015, leo anakutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuanika kile kinachoelezwa kuwa ni mchezo mchafu unaofanywa na mahasimu wake.
Hatua ya kada huyo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), inafuatia tukio la hivi karibuni akidai kuhujumiwa katika mwaliko aliopewa na vijana wa asasi isiyo ya kiserikali inayojihusisha kuelimisha jamii kuhusu usalama na amani (Public Terrorism Awareness Trust Fund and Human Welfare (PTA-HW).
Asasi hiyo iliandaa tamasha Jumapili iliyopita jijini Dar es Salaam na kumwalika Sumaye kuwa mgeni rasmi lakini katika mazingira ya kutatanisha saa chache kabla ya shughuli hiyo iliyofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanza, aliarifiwa kuwa imeahirishwa na kwamba atataarifiwa tarehe nyingine itakayopangwa.
Hata hivyo, katika hali isiyoelezeka muda mfupi baadaye maandamano ya vijana hao yaliwasili katika viwanja vya Mnazi Mmoja na kupokewa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kutoka Wilaya ya Bukoba Vijijini, Nazir Karamagi.
Dalili za waziwazi za mgawanyiko miongoni mwa waandaji zilijitokeza baada ya kuwasili kwa Karamagi ambaye hakuwa ametarajiwa na waandaaji pamoja na washiriki wa tamasha hilo.
Kwa muda mrefu sasa Sumaye amekuwa akidai kuhujumiwa na wapinzani wake wanaomhofia katika mbio za urais mwaka 2015 ambapo katika Uchaguzi Mkuu wa CCM mwaka jana alidai kuchezewa rafu ya rushwa.
Tanzania Daima
Lowassa anafaa kuwa rais 2015 maana anajua maeneo nyeti na korofi katika nchi yetu ambayo akiyashughulikia naamini imani inaweza kurudi kwa CCM hasa katika suala la AJIRA na ELIMU huyo jamaa mwingine hafai kuwa rais kwa sioni alichokifanya alipokuwa w/mkuu ktk serikali ya awamu ya tatu-suala la elimu mh Lowassa analivalia njuga tangu alipokuwa PM na mpaka sasa,eg shule za kata kuwepo ni juhudi zake binafsi lakini waziri wa sasa hajaona umuhimu wa kuendeleza alichokiacha Lowassa,wali hawalipwi vizuri,mazingira magumu ya kufundishia,shule hazina vitabu,maabara,walimu wa kutosha,maktaba,hii kitu naamini Lowassa inamsumbua sana akilini na naamini akipewa urais mwaka 2015 vyote hivi vitakuwa solved hata kama sio asilimia mia atlest itakuwa better than now.by Malanga A N
ReplyDeleteLowasa anamaamuzi, upeo, sauti yenye kusikika na kusikilizwa na hana mzaha aa 2015 nampa kura yangu kwa asilimia 100
DeleteHapana na wala hafai kuwa kiongozi, kwani kaongea haya katika kujisafisha na kujisafishia nia ya kuutaka URAIS. Kumbuka huyu ni mwana CCM na mpango huu wa maendeleo ni dira kwa CCM na mpaka unafikia bungeni (kuletwa bungeni) umepitia katika vikao, kamati na mikutano mbalimbali ndani ya CCM. Yeye alikuwa wapi kutoa mapendekezo haya katika kamati, kaacha huko leo kaibukia bungeni, Je, kama sio kuutaka URAIS ni nini? Lakini kumbuka amekaa serikali kwa muda mrefu, alifanya nini katika UONGOZI wake? Kuwag'oa vigogo/wawekezaji/wakala wa maji wa Dar es Salaam kipindi hicho, mengine je? Huyu ni muongo na mnafiki anautaka URAIS kwa udi na uvumba.
DeleteWewe anonym 8:57pm acha kuwa mjinga au kibaraka! Utamsifiaje Jambazi? Mapesa aliyoiba 'Lowassa' amefsnyia nini mbali ya kujitajirisha na kununu suti tu. Admin. usi-publish kampeni humu ndani, please.
Deletelowassa kiukweli anafaa kuwa rais wa Tanzania 2015.
ReplyDeletehivi mesahau ufisadi wake wa richmond akiwa rais vita vitatokea
Deletewatu hatuna data, nani kakuambia lowassa ndo alifanya ufisadi wa richmond??? yeye aliwajibika kwa nafasi yake ila sio kwamba yeye ndo kahusika. inaonyesha bado watu wana hili jinamizi la kuona lowassa ndo mwenye richmond. hivi leo mauaji yakifanyika na waziri wa mambo ya ndani akajiuzulu utasema yeye ndo kawaua??? acheni kufikiria karibu. mwinyi alijiuzulu akiwa waziri kwa kosa lililotokea ofisini kwake. hili ni swala la uwajibikaji tu sio kwamba ndo yeye kafanya. amkeni. mtu mwenye busara akiona kosa limefanyika ofisini kwake anatakiwa ajiuzulu ila viongozi wengi wa Tz hawataki wanagomea madarakani hata kama wamefanya makosa. kama hujui ndo mana unasikia waziri fulani jiuzulu, it does nt kwamba yeye ndo amefanya tukio. sa hivi tunamsakama waziri wa mali asili kwa swala la pembe za ndovu ili ajiuzulu, sio kwamba yeye ndo anasafirisha pembe hizo. AMKENI
Deletemtu pekee anaefaa kua rais wa tz ni KABWE ZITTO. PEKE YAKE KWA SASA...........
ReplyDeleteI Salute anony.10:06pm Zitto hakupewa au kurithishwa uongozi kama 'Januari Makamba' na wengine wengi, yeye alizaliwa Kiongozi kutokana na busara zake za kuona au kuvisoma vitu kama karne ya 21 inavyoendelea.
DeleteSwala la afya ni muhimu sana, huduma bora za afya inapaswa ziwepo za uhakika wilaya zote.
ReplyDeletekweli wa tz wasahaulifu na viongozi wanajua hilo na hamtokaa mkapata kiongozi anae wataka bali mnae taka maana aliyo yafanya lowassa mmeyasahau yote na sasa mnataka kumpa nchi ndio mumtajirishe vizuri sasa za richmond zimekwisha? kwa ccm mpeni mzee SITTA na waziri mkuu wake MWAKYEMBE otherwise nchi itauzwa.............mi napita tu watz wenzangu na ninawakumbusha tu.
ReplyDeletejamani watazania ni maburaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa hao na jk ni mtu na shoga yake nchi apewe zito.
DeleteUmeniwahi mdau nilikuwa nataluandika hivyo lowassa na kikwete,na rostam aziz ni mabestiiiii mpaka kupitiliza,nchi apewe zitto Kabwe ,mitanzania akili zao Fupiii,Richmond wameshasahau,mnampa nchi fisi
DeleteHaoni hata haya kuongea bungeni kwa yale aloyafanya kuila nchi mpaka amehakikisha ameimaliza ama kweli mtajilisheni tena mmpe nchi sasa ndo ataques kama mwenzangu hapo juuu alivyosema. Mara kumi hata Zito Kabwe kuliko huyo jambazi Lowasa
ReplyDeleteZito anafaa kuongoza nchi hii
ReplyDeleteKwa kweli naona baadhi wa ya watoa maoni wanaomponda Mh.Lowassa bado wamo gizani,na laana za mizimu ya umaskini inayolitesa taifa imewajaa kabisa. Nasema acheni majungu na fikra potofu,sio wakati wa kucheza tena michezo ya kipuuzi ya siasa zisizoleta maendeleo,YALIYOPITA SI NDWELE,TUYAGANGE YALIYOPO NA YAJAYO! Rais wa TZ hii iliyochakaa namna hii ni Lowassa tu aifufue toka mautini au ICU ili liitwe taifa la wenye akili. Swali; Ni nani mwenye ubavu wa kutekeleza hayo ya msingi aliyoshauri Rais wetu ajaye Lowassa?
ReplyDeleteRais anayefaa kuchaguliwa 2015 anatakiwa kuwa na UDIKTETA 50%
ReplyDeleteAunde mahakama maalum kwa ajili ya mafisadi,majangili,wauza unga,wala rushwa kama matrafiki wanaotusumbua barabarani na kwenye maofisi za umma,nk
Bila hiyo TZ itabakia ni ufisadi uliopindukia na maovu mengi. Kesi zinakaa miaka mingi bila hukumu hii inawapa kiburi mafisadi na wa-tz wengi wenye pesa zao kwa sababu kuna mapungufu makubwa sana ktk mahakama zetu hizi. Rais anayeweza kutoa maamuzi mazito ambayo hata kimtizamo utadhani haiwezekani!
Endeleeni kumtajirisha lowassa Kwa kumpa nchi 2015.poleni sana.
ReplyDeleteHAHAHAAAAAAAAAAAAAAAAAAA NAOMBA KUULIZA HIVI TUPO SERIES YA NGAPI VILE KWENYE HII SEASON? NGOJA S.SITA NAE ATAKUJA NA SEASON FIVE YAKE
ReplyDeleteAcheni maneno yasiyokuwa na msingi mwenye uhakika kuwa LOWWASA kaiba ni nani?acheni kuongea msivyovifahamu MTAKE MSITAKE LOWWASA NDIYE RAIS WENU,ana maamuzi na anajiamini nani wa kufananishwa nae,hapa hatupo kwa ajili ya vyama tunamtaka mtu makini,si mbwabwaji wa maneno yasiotekelezeka na ww uliyesema akishinda kutakuwa na vita,pengine uende mirembe ukapime uwezo wa akili zako,zina kasoro Lowwasa ni jembe.
ReplyDeletebora tuendelee kusaka makaratasi ulaya kwa style hii Lowasa kuwa rais hali ya nyumban itazidi kuwa tete
ReplyDeleteOmbeni kwa MUNGU awape raisi kwani atakaekuja atafanana na jinsi tulivyo. Ila tukimwomba MUNGU tutapewa atakaetutoa tulivyo na kutupeleka tunavyotakiwa kuwa. Hakuna utawala wowote duniani usiokuja kwa kusudi fulani ,kusudi Lima MOLA ,kama watu hamjawahi kujaribu sasa jaribuni Kuomba MUNGU inalipa,usiombe sana sema tu. "EE MUNGU MKUU TUPE RAIS ATAKAETUVUSHA NG'AMBO . AAMIN" HIVYO tu,wote tukifanya hivyo,tutajibiwa hakika maana MUNGU Ndiye anajua moyo wa kila mtu maneno ya mdomoni si ndo mwisho yapo mengine tusiyoyajua ambayo ndo chanzo cha manung'uniko yetu. b blsd Tz and her people.
ReplyDelete