MANCHESTER UNITED VS ARSENAL: JE ARSENAL ITAMALIZA UTEJA KWA UNITED???

Red Devils vs. Gunners ni mechi ambayo imekuwa ikitupa karibia kila kitu kuhusu soka katika miaka mingi iliyopita na siku ya leo tutapata kuona mengine zaidi. 
Mchezo wa leo kwa upande mwekundu wa jiji la Manchester unaweza ukatoa picha nzuri ya hatma ya United katika msimu huu. 
Arsenal wamedondosha point mbili tu katika mechi zao tisa zilizopita za ligi na wapo juu ya United kwa pointi nane, ambao wapo nafasi ya 8 kwenye ligi.
The Gunners wamewanyamazisha watu waliokuwa na mashaka nao kila wiki inayopita na watakuwa na hali kubwa ya kujiamini wakati wakiwasili Old Trafford baadae leo. 
Gary Neville tayari ameshaonyesha kwamba Arsenal wana nafasi ya kushinda leo kwa fomu nzuri waliyonayo - aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuhusu ubora wa Arsenal katikati ya wiki baada ya ushindi dhidi ya Borussia Dortmund katika Champions League.

Lakini jambo moja ambalo Gunners hawajafanikiwa kufanya msimu huu ni kutoka nyuma na kwenda kushinda mechi hiyo. 
Inaweza sababu ikawa kwamba wamekuwa wakitangulia kufunga, lakini pia dhidi ya Aston Villa katika mechi ya ufunguzi wa msimu, dhidi ya Chelsea katika Capital One Cup na Dortmund katika Champions League ndani ya Emirates, walifungwa kwa goli moja na wakashindwa kujibu mapigo. 
Ikiwa United wataweza kuanza kufunga katika mechi ya leo, then leo tutaona namna ubora wa Arsenal katika level ya juu kabisa.

Udhaifu na Ubora wa timu - Gunners wana matatizo katika mashavu ya ukuta wake. Sagna na Gibbs wamekuwa wakicheza vizuri msimu huu lakini wanapokutana na timu zenye mawinga wazuri wamekuwa wakipotea. Wasipokuwa makini wanaweza kuigharimu timu. Ushindi wa Arsenal leo unaweza ukaamuliwa na safu ya kiungo chao ambayo imeimarika vilivyo msimu huu baada ya kuongezwa kwa Mesut Ozil na kuimarika kwa kiwango cha Ramsey.
Man United bado wana udhaifu katika safu ya kiungo kitu ambacho kimekuwa kikiwasumbua kwa kipindi kirefu. Maroune Fellaini bado hajakaa sawa ndani ya timu na hivyo kuna uwezekano akaanzia benchi. United wamekuwa wakiboreka katika safu ya ushambuliaji kadri siku zinavyokwenda msimu huu. Wakiongezewa nguvu na ubora wa fomu ya Wayne Rooney, na kinda Adnan Januzaj. Endapo Rooney na Van Persie watacheza vizuri kama ilivyokuwa dhidi ya Fulham mambo yawawia vigumu safu ya ulinzi ya Arsenal.


TAKWIMU
United wamepoteza mechi moja tu kati ya 12 zilizopita za ligi na Capital One dhidi ya Gunners.

Huu utakuwa mchezo 50 wa Arsenal Wenger dhidi ya United tangu awe kocha wa Arsenal. Ameshina mechi 15 katika 49 zilizopita  (ukitoa zilizoisha kwa mikwaju ya penati).


Magoli 14 kati ya 19 ya ligi yamefungwa au kusaidiwa na aidha Robin van Persie au Wayne Rooney.

Ushindi wa leo utaipa Arsenal rekodi ya kuwa na pointi nyingi zaidi baada ya mechi 11 za ligi.

Arsenal ndio timu pekee ya Premier League kufunga katika mchezo wa ligi msimu huu.

Ramsey amefunga mabao 11 katika mechi 17 lza ligi na kombe la ligi akiwa na Arsenal msimu huu, na mabao 13 katika mechi 21 za klabu na nchi yake. 

Arsene Wenger ana rekodi ya kushinda mara 14 katika mechi za premier league dhidi ya David Moyes - idadi kubwa kuliko dhidi ya kocha yoyote wa ligi hiyo hivi sasa.

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mume mume tu hata akitangulia chin hatabaki palepale

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad