MASOUD MASOUD "DIAMOND HAWEZI KUMFIKIA ALI KIBA KATIKA UIMBAJI HATA KIDOGO"

Wiki iliyopita katika kipindi cha Mkasi ambacho hurushwa kupitia EATV na kuendeshwa na mtangazaji Salama Jabir, mgeni alikuwa Masoud Masoud, mtangazaji mahiri wa muda mrefu ambaye ni miongoni mwa watangazaji wa Radio wanaoheshimika sana Tanzania kutokana na upeo mkubwa alionao na kufahamu mambo mengi.

Moja ya swali aliloulizwa ni “Labda kuna tamasha wewe ndio muandaaji au wamekwambia uchague mwanamuziki ambaye ataenda kuburudisha kwenye hilo tamasha Tanzania utamchagua mwanamuziki gani?”

Masoud ambaye anasifa ya kuongea kwa uwazi bila kupindisha maneno alimtaja Alikiba kuwa ndiye msanii pekee wa bongo fleva anayemkubali kuliko mwingine yeyote.

“Mimi wa kwanza nitakayempendekeza aaah nani huyu, nampenda sana katika wasanii wote wa bongo fleva, Alikiba, Alikiba nampenda sana. Alikiba kama umemsikiliza, Rhyme zake zile katikati ya zile bars anavyoimba ni mwanamuziki kama angekuwa nje ya nchi asingekamatika. Angepata producer mzuri wa kumfahamisha nini cha kuimba beat gani atumie, Alikiba yuko juu sana.” Alijibu Masoud

Aliendelea na kuongeza kuwa Diamond anaweza kuwa anafanya vizuri sokoni lakini hawezi kumfikia hata kidogo Kiba katika uimbaji.

“Nyota imeng’aa kwa Diamond Platnumz lakini Diamond Platnumz siwezi kumlinganisha hata kidogo na Alikiba, kwenye kuuza huwezi kumlaumu anaweza kuwa Diamond akauza sana au akampandisha na si Tanzania tu, hata Hollywood wanafanya hivyo hata CBS wanafanya hivyo, hata US music industry wanfanya hivyo. Sasa mpaka wakiwepo watu wataalam wanaoweza kusema huyu anaimba sawa huyu haimbi sawa lakini kwenye mauzo hakuna mtu anajali hilo.”

Masoud kwa sasa ni mtangazaji wa TBC Taifa.

Mtazame hapa kupitia Mkasi (sogeza hadi dakika 17:45 alipozungumzia kuhusu Alikiba na Diamond)

Imeandikwa na Bongo5.com


Tags

Post a Comment

16 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mjomba nikwel kwan hakuna anacho imba cha maana ila tuu mashabiki.

    ReplyDelete
  2. Mziki biashara watu awaangalii uimbaji watu wanaangalia mkwanja mzee

    ReplyDelete
  3. Ali K habadiliki

    ReplyDelete
  4. Toa pesa ili uingize pesa mwelekezeni huyo alikiba!!!

    ReplyDelete
  5. Kwel ali kuimba. Diamond sokon

    ReplyDelete
  6. dIAMOND HODARI WA KUKATA MAUNO TU HUYO NA KUNYOA KIDUKU

    ReplyDelete
  7. sahihi kabisa, Kiba anaimba vizuri hata akiwa live sauti imetulia ila Diamond ni mkali studio kuliko live.Sokoni Diamond hakamatiki

    ReplyDelete
  8. Ally anajua. Boss Masoud watoto cku hizi hawajitambui ona suruali zao zinonesha makalio ova wanataka kubomolewa. Masoud ww unaujua muziki lkn wengi leo hii wanashabikia wasichokijua.

    ReplyDelete
  9. Ally anajua. Boss Masoud watoto cku hizi hawajitambui ona suruali zao zinonesha makalio ova wanataka kubomolewa. Masoud ww unaujua muziki lkn wengi leo hii wanashabikia wasichokijua.

    ReplyDelete
  10. Ally anajua. Boss Masoud watoto cku hizi hawajitambui ona suruali zao zinonesha makalio ova wanataka kubomolewa. Masoud ww unaujua muziki lkn wengi leo hii wanashabikia wasichokijua.

    ReplyDelete
  11. Ally anajua. Boss Masoud watoto cku hizi hawajitambui ona suruali zao zinonesha makalio ova wanataka kubomolewa. Masoud ww unaujua muziki lkn wengi leo hii wanashabikia wasichokijua.

    ReplyDelete
  12. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  13. Tushachokaaaaaaaaaaaaaaaa topic zinazohusu domo nene plseeeeeeee hakuna wanamuziki wengine?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wanamuziki wengine si ndio hao akina Ali K utaandika nini kuhusu yeye? Na hata sijui yuko wapi na anafanya nini D ukiachana na scandal lazima ataandikwa anafanya kazi zinaonekana.

      Delete
  14. I support you 100%, true said .

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad