MAUMIVU "NILIYE MFUMANIA NA MPENZI WANGU KANIANGUSHIA KIPIGO CHA MBWA"

Nina mpenzi wangu ambaye yuko chuo fulani hapa Dar lakini kutokana na maamuzi yetu tuliamua aishi mtaani badala ya Hostel. Huyu msichana nilianza nae mahusiano kwa kipindi kirefu sana na hata tumefikia kuvalishana pete na nyumbani kwao nafahamika pia.

Kutokana na shughuli zangu nyingi kua mikoani hua tunakutana kwa baadhi ya wikiendi tu ninapokuja hapa Dar.

Basi Ijumaa hii nikaona sio vibaya kum-surprise my wife to be. Nikatoka zangu mkoani na shauku ya kujiandaa kwenda kwa P-square na mamaa.

Nilipofika pale Geto kwake hali sikuielewa. Nikaona sio mbaya kubisha hodi. Niligonga kidogo tu sauti yenye hasira na mikwaruzo ikatoka ndani. "Wewe Nani"???

Nikajibu kwa kujiamini nikijua wako discussion na wenzake.. "Mimi ni Edwin"

Ndani nikasikia kama wanabishana kidogo.

Ghafla jamaa akafungua mlango na kuniuliza huku amekasirika wewe nani? Nikajibu kwa kujiamini. "Kama Grace yupo ndani muulize Edwin ni nani?"

Basi Grace alipoulizwa akakana kunifahamu. Hapo jamaa akaanza kunishushia kipigo. Kutokana na mwili mdogo nilionao jamaa alinipga kwa kweli huku akitishia kunipigia kelele za mwizi.

Basi baada ya pale nikaenda hospital kupata matibabu. Nikaamua kumtaarifu mama yake Grace. Mama Grace alishangaa sana na kudai mbona Grace alimtaarifu tumeachana kwa Mwezi sasa?

Nikachanganyikiwa zaidi. Nilipopeleleza zaidi kwa rafiki yake mmoja, nikagundua jamaa ndio anamgharamia Grace kila kitu na kias nilichotoa kwa Grace ilikua hela ya chumvi tu..

Hapa nilipo nina maplasta usoni na sehemu nyingine.

Nisaidieni nichukue hatua Gani kisheria juu ya huyu jamaa? Je akisema nilitaka kuiba nitajitetea vipi? Ushauri wenu ni muhimu sana

Note
Nimetumia majina ya kweli ili kama Grace yupo humu ndani ujumbe umfikie na ajue ameniumiza sana moyoni kwa usaliti aliouonyesha mchana kweupe.

Asanteni
Tags

Post a Comment

40 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Chapa lapa tafuta mwingine hata ukimshitaki huyo aliyekupiga kama ana mkwanja bado itakula kwako na utazidi ku umiza nafsi yako,omba mungu akusaidie upate mwingine asije kuwa kama grece.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tafuta bastola mfanyie ufoo saro style au Gabriel munusi WA ilala. Hawa mademu wamezidi kutuchanganya.

      Delete
  2. Replies
    1. Tena amroge kubleed mbele na nyuma

      Delete
  3. Tafuta mwingine coz huyo sio mwaminifu

    ReplyDelete
  4. Jaman hya mapenz 2napoelekea n kubaya hamuwez amn wenzang mm pia nimeumizwa xana n mke wa m2 na nimegundua mume wng amenisalit tena mbaya zaid amezaa na hyo m2 wake kiukwel moyo wng umekufa ganzi celew ht cha kufanya na mume wng bdo nampenda mapenz yanaumiza xana k2 nnchotalajia kufanya mtapata hbr 2 kwenye mpekuz

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mtumeeeeeee usitumie bastola we dada!!!

      Delete
  5. Aaaah kaka! pesa huna, nguvu huna sawa lakini hata mikwara nayo pia huna?
    pole sana ndugu yangu ndio mademu wa bongo hao, harafu siku anakuja kupigia magoti umsamehe unalegeza na unasahau mashuti ulipigwa hiyo ni mbaya sana unamkana mpenzi wako kisa pesa?

    ReplyDelete
  6. Pole ndugu ndo maisha hayo, Ila ucfe moyo kwan hiv viumbe vina tamaa sana kuwa care ktk utafuta, unaweza ukalivagaa laghai kuliko hata huyo grec! Ila yote maisha!....

    ReplyDelete
  7. Mim takusaidia Bastora bro' awa madem wamezidi sasa

    ReplyDelete
  8. Achana nae huyo demu mzee anga
    lia maisha yako wanawake sio watu kabisa

    ReplyDelete
  9. ...sasa hivi hawa wasaliti wasipigwe risasi kwanza wanaowapiga risasi wenyewe hawana shabaha kila siku wanaishia kuwajeruhi tu aagh! dawa yao ni kuwaharibu masula yao na mtindi mkali ili yahalibike masula kabisa tuone kama kuna mtu atayatamani na masula mabaya.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe una akili sana, hizi bastola wala hazifai shabaha ni ngumu, mpango mzima tindikali tu tena hio haina gharama halafu unasepa kwenye kigiza kiulainii unamwangalia sasa atamuuzia nani sura baada ya hapo. Bastola utanyea debe mpaka ufe sasa faida gani au eti ujiue halafu huku umekosea shabaha mwenzio amalazwa wki mbili anatoka kuponda raha kama kawa. Jamani mimi sisemi mtindi mkali ni kitu kizuri ila wasichana na wanawake kwa wanaume acheni kutujeruhi na kutuchuna kwenye mapenzi then mnatubwaga, tunaumia jameni, kama hunipendi nikatae mapaaa sio nimelipa ada miaka, nimenunua gari, nimejenga nyumba mpaka umenona na kupendeza then mnatubwaga.

      Delete
    2. Yote ya nn ndugu yangu, huo ni udikteta wa mapenzi.mapenzi ni uamuzi wa mtu hayalazimishwi bro

      Delete
    3. Mbona hata sisi tunawafanyia madem hivyo?tena cases zetu ni kubwa zaidi.Afu yakitokea kwetu tunalalamikaaa...anyway pole sana kamanda, Mungu amekuepushia coz huyo demu anatamaa na hakufai

      Delete
    4. eh, tindikali tena? mnanitisha japo mimi si msaliti. ukisingiziwa itakuwaje?

      Delete
  10. Mapenz yanatesa jaman,achana nae

    ReplyDelete
  11. Kama vipi mtungie wimbo itauza

    ReplyDelete
  12. Nitafute nitakusaidia mm mganga napatika Liwale Lindi kaz ndogo sana hyo utakavyotaka ww hata kuua

    ReplyDelete
  13. Unge mfr kwanza uwezi mmjua jamaa kama alikuwa anasababisha njoo taon madem wa kutosha men

    ReplyDelete
  14. hapo hakuna cha sheria jembe ni shaba tu we huon wachaga wanafanyaje!

    ReplyDelete
  15. achana nae kwanza kitendo cha kukukana tu ni tosha hakuhitaji, achana nae mungu atakulipa tena mara dufu, utakuja uone,

    ReplyDelete
  16. Bora umemgundua mapema,sahau yaliyopita,jenga maisha yako na tafuta mwingine ambaye utaona anafaa, usikate tamaa wanawake wenye mapenzi ya kweli wapo japo wachache!

    ReplyDelete
  17. Mwanangu Kaza But 2 Mbona Madem Wapo Tena Wa Kumwaga 2.

    ReplyDelete
  18. Unang'ang`ana nin mshikaji wangu,achana naye braza!!

    ReplyDelete
  19. Unang'ang`ana nin mshikaji wangu,achana naye braza!!

    ReplyDelete
  20. MBONA JIBU UMEPATA [ T I N D I K A L I ]

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tusitumie tindiiali kwenye mambo ya mapenzi jamani. bora bastora kuna kufa au kupona, tindikali ni kilema cha kudumu

      Delete
  21. Njoo kwang utasahau yote

    ReplyDelete
  22. Njoo kwang utasahau yote

    ReplyDelete
  23. weweee acha upumbavu ulishindwa kusoma alama za nyakati huyo demu mipango ya kukupiga chini ilikuwepo siku nyingi awezi akafanya uamuzi wa ghafla ila ww unatudanganya sisi HIVI ww ni mchagga nn? maana yake nyinyi MALIMBUKENI wanawake.

    ReplyDelete
  24. Oya Big Kama Vp Kaushia 2 Ngachu Ni Wengi Sana Na Utampata Mwengne Mwenye Upendo Wa Dhat Na Wewe Co Huyo Mwenye Tamaa!But Be Care Brooo.

    ReplyDelete
  25. Mapenzi niuuweeee%&@%@&@%@

    ReplyDelete
  26. mpotezee kwa muda jifanye kama bwege vile harafu mwisho wa siku mtafute jifanye kama umesahau omba penzi kama kawaida akikubali tuu nikumtembezea kifilo mwanzo mwisho harafu piga chini jumla yeye si mshenzi

    ReplyDelete
  27. Pole sana ndugu yangu ya dunia njoo ivyo. Lakini mimi nakushauri sahau uyo. Demu hafai tafuta mwengine na kweli utapata anaye kufaa nakumushitaki jamaa yanii wewe hauna sheria mwanamke atakukana kama alivyo.kukana mbele ya uyo jamaa

    ReplyDelete
  28. kama wewe siyo mchaga hata rafiki wa kichaga huna? kama huna tafuta mmoja wao wanaijua shughuli hiyo vyema!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  29. pole sana kweli mapenz yanaua jamani

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad