MCHUNGAJI MWINGIRA NDANI YA SKENDO NZITO YA KUZAA NA MKE WA MTU

TUHUMA nzito dhidi ya kiongozi wa Kanisa la Efatha, Nabii Josephat Mwingira, zimefunguliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central), Kibaha, Pwani. 

Dk. William T. Morris ambaye ni daktari anayetambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN), ndiye aliyeshusha tuhuma hizo, akidai kwamba Mwingira amezaa na mke wake, Dk. Philis Nyimbi.
Morris ambaye wasifu wake unaeleza namna sifa zake zinavyojipambanua ndani ya Shirika la Afya Duniani (WHO), aliwasilisha madai hayo mwaka 2011, akitaka jeshi la polisi limsaidie kupata haki zake.


Dk. Philis Nyimbi anayedaiwa kuzaa na Nabii Mwingira.


UWAZI LANASA JALADA LA UCHUNGUZI
Mtandao mpana wa mitego ya habari katika Gazeti la Uwazi, uliwezesha kunasa uwepo wa jalada la uchunguzi, likiwa na nambari KBA/ PE/23/2011 ambalo mhusika wake ni Mwingira.
Shauri hilo linasomeka kwenye kumbukumbu za jeshi la polisi KBA/ PE/23/2011 JALADA LA UCHUNGUZI.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, ACP Unrich Matei, alilithibitishia gazeti hili kwamba kweli jalada hilo lilifunguliwa na tuhuma zake ni hizo za Morris kudai Mwingira amezaa na mkewe.



UTHIBITISHO WA BARUA YA POLISI
Habari zinasema kuwa Morris alipofungua shauri hilo, haikuchukua muda mrefu alirudishiwa majibu kwamba tuhuma zake azipeleke mahakamani kwa sababu hazina mashiko katika jinai.
Awali, tuhuma zake zilijipambanua kwamba Mwingira amekuwa na uhusiano usiofaa na mkewe (Philis) mpaka kumpa ujauzito na hatimaye mtoto akazaliwa.
Katika barua hiyo, iliyosainiwa na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Jinai (RCO), Mkoa wa Pwani, SSP E.H. Mwijage, ilimwelekeza Morris kutafuta haki katika mkondo mwingine wa sheria, hususan mahakamani.
Barua hiyo ilikuwa na kichwa; YAH: KBA/PE/23/2011, KOSA: JALADA LA UCHUNGUZI, MTUHUMIWA: JOSEPHAT MWINGIRA.
Vilevile barua hiyo, ilikuwa na kumbukumbu nambari PWA/CID/130/VOL XXV11/211 na ilikuwa ni majibu ya ile ambayo Morris alimwandikia RCO, Desemba Mosi, 2011.
Barua hiyo ya RCO, iliandikwa Januari 25, 2012 ikiwa na maelezo yafuatayo;
“Baada ya uchunguzi makini juu ya malalamiko yako, uchunguzi umebaini kuwa kosa lililofanyika ni adultery (kuzini) au defamation (udhalilishaji) ambapo katika sheria za makosa ya jinai, makosa hayo hayapo.
“Kutokana na sababu hizo hapo juu, tunakushauri uchukue hatua nyingine za kupata haki yao au ufungue kesi ya madai mahakamani dhidi ya mtuhumiwa.”
MORRIS ANASEMAJE?
Morris alitafutwa na waandishi wetu na alipopatikana, alikiri kila kitu lakini alidai kwamba amekuwa akipata shida kufungua kesi ya madai mahakamani kutokana na misukosuko mbalimbali anayopewa.
Alisema, yeye siyo Mtanzania na kutokana na hilo, amekuwa akisumbuliwa na hata kutishiwa kurudishwa kwao.
Aliongeza kwamba ameendelea kushughulikia hili suala lake kwa utulivu bila papara ili asipoteze haki zake za msingi.
UMOJA WA MATAIFA
Kwa upande mwingine, zipo nyaraka ambazo Morris inadaiwa alizituma Umoja wa Mataifa kwa barua pepe (tunayo nakala yake) aliyoielekeza kwa katibu mkuu wa shirika hilo, Ban Ki Moon, Januari 11, 2011.
Hata hivyo, ndani ya barua hiyo, Morris ameeleza tuhuma nyingine mbalimbali kuhusu Mwingira lakini zinahifadhiwa kwa sasa.
Katika barua hiyo, Morris aliomba ulinzi kwa sababu tayari Ubalozi wa Marekani nchini, Umoja wa Ulaya, Shirika la Kimataifa la Haki za Binadamu (Amnesty International), Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na taasisi ya haki za binadamu nchini, ameshazipa taarifa.
Aidha, Morris alimsisitizia Ki Moon ombi lake la kusaidiwa kupata haki zake na mkewe pamoja na madai mengine aliyoyaandika katika waraka huo.

CHETI CHA NDOA
Kwa mujibu wa Morris, Philis ni mke wake halali, aliyefunga naye ndoa takatifu katika Kanisa la St. Alban jijini Dar es Salaam, Desemba 23, 2001, akiwa na umri wa miaka 39 na mkewe wakati huo alikuwa na miaka 30 na kupewa cheti cha ndoa namba B. 0638572 na ilifungishwa na Padri Canon William Kambanga.
Uwazi linayo nakala ya cheti hicho cha ndoa.
MKE NAYE AZUNGUMZA
Kuhusu tuhuma hizo, Philis alisema kuwa Mwingira hahusiki kwenye matatizo yao.
“Yule alinitelekeza, siyo mume wangu,” alisema Philis na kuongeza: “Angekuwa mume kweli asingenitelekeza na kunisaliti mpaka kwa mtoto wa kike ambaye tunaweza kumzaa.”
Aliongeza kuwa alimvumilia Morris kwa mambo mengi na hawezi kumsamehe kwa sababu alimuumiza sana.
MWANDISHI: Kwa maana hiyo unakiri kwamba ulizaa na mwanaume mwingine?
PHILIS: Ni kweli, nilifanya hivyo baada ya yeye kunitelekeza na hakuwa na uwezo wa kunizalisha.
MWANDISHI: Huyo mwanaume ni nani? Ni Mwingira?
PHILIS: Hilo swali siwezi kujibu, iwe Mwingira au mwanaume mwingine yeyote, labda kwa wakili wangu au mahakamani.
MWANDISHI: Unafahamiana na Mwingira kwa ukaribu?
PHILIS: Ndiyo nafahamiana naye, ni ndugu yangu.
MWANDISHI: Ndugu yako kivipi? Labda kaka, mjomba au?
PHILIS: Wewe elewa ni ndugu yangu, ila kuhusu ndugu yangu kivipi, hilo swali siwezi kukujibu.
MWANDISHI: Umewahi kuwa muumini wa Mwingira?
PHILIS: Iwe nasali RC, KKKT au vyovyote vile, wewe inakuhusu nini?
MWANDISHI: Kama utasuluhishwa na Morris, unaweza kuishi naye tena?
PHILIS: Wewe kaka, hivi unajua jinsi yule mwanaume alivyoniumiza? Siwezi kabisa.

KUMPATA MWINGIRA SHUGHULI
Waandishi wetu walifanya jitihada za kuzungumza na Mwingira mara tatu bila mafanikio.
Mara ya kwanza, waandishi wetu walikutana na walinzi ambao walisema, hawataonana na Mwingira, isipokuwa wakutane na msaidizi wake ambaye anaitwa Mchungaji Urasa.
Mara ya pili, waandishi wetu walikutana na Urasa ambaye alisema ili kumuona Mwingira inabidi kuandika nambari ya simu, jina na mahali ambako wanatoka.
Mmoja wa waandishi wetu aliacha jina, nambari ya simu na maelezo mengine yaliyohitajika lakini hakupata majibu yoyote.
Jumapili iliyopita, waandishi wetu walirudi kanisani Efatha kwa mara ya tatu na kukutana na mtu anayeitwa Samuel Peter ambaye alijitambulisha kama mtumishi.
Waandishi wetu walipomuomba Samuel awape muongozo wa kuonana na Mwingira, alijibu: “Siyo rahisi kumuona nabii.”
Hata waandishi wetu walipoomba nafasi ya kuonana na Urasa ili kukumbusha ahadi ya mwanzo, Samuel alijibu: “Hata Urasa hamuwezi kumuona, mbona huwa hamji kuripoti habari za ukombozi kama misukule? Hamuwezi kuwaona wote hao.”
KAMANDA WA POLISI
Jumapili iliyopita, Kamanda Matei, alipoulizwa kuhusu maendeleo ya kesi hiyo ya Morris na Mwingira, alisema anahitaji mlalamikaji aende ofisini kwake.
“Ni kweli tukio hilo lipo kituoni lakini jalada lake likafungwa. Naona mazingira ya kulifunga lile jalada hayakuwa sahihi, nahitaji aje ofisini kwangu tuone nini hasa kilisababisha lile jalada la uchunguzi likafungwa,” alisema Matei.
Alifafanua kuwa kesi hiyo ilifunguliwa wakati Pwani ikiwa na kamanda mwingine, kwa hiyo yeye amelikuta shauri hilo.
“Unajua yale ni madai tu, inabidi mlalamikaji aje atupe ushirikiano, mtoto apimwe damu kwa ajili ya DNA, vile vinasaba ndivyo vitatoa jibu yule mtoto ni wa nani,” alisema Kamanda Matei.

Chanzo:Global Publishers
--------------
Please Click Like Button Below

Post a Comment

20 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu mwingira ni fuska wakutupwa,alinitapeli karibu mafao yote niliyoyapata nilipopunguzwa kazi CRDB morogoro na pia alitaka kubaka.Ni nabii wa uwongo.

    ReplyDelete
  2. Nyie hamshtuki jamani.......Wachungaji na manabii feki ni wa kumwaga Mungu atunusuru maana cku za mwisho zimekaribia,so wengi wako after money,ni matapeli na wanzinzi si kila king'aacho ni dhahabu jamani zingine chupa.

    ReplyDelete
  3. Nyie hamshtuki jamani.......Wachungaji na manabii feki ni wa kumwaga Mungu atunusuru maana cku za mwisho zimekaribia,so wengi wako after money,ni matapeli na wanzinzi si kila king'aacho ni dhahabu jamani zingine chupa.

    ReplyDelete
  4. Hapo haki itendeke bila kujali utaifa wa mlalamikaji@Malanga A N

    ReplyDelete
  5. mungu hz ndoa za sasa hv mbona hatar kachala kwa kachala hawaelewan mwenye pesa kwa mwenye pesa hola! aliyesoma na asiyesoma shughuli msom kwa msom tabuu.ee jmn mtoto hajatendewa haki kuwekwa humu

    ReplyDelete
  6. neno.la.nabii lilifanya kazi likatoa na mtoto!!!! mwee nyie waumini kusoma hamuwezi.basi hata picha hamuoni?

    ReplyDelete
  7. sintosahau siku nimetoka safari nikamkuta huyu mtumishi akimtomasa mke wangu mbele ya mtoto wangu wa miaka 4 sikuwahi kufika hata kanisani kwake tena. najuta na misaada niliyokupa malaya mkubwa wewe. sidhani kama nitaenda kanisani ktk maisha yangu tena.

    ReplyDelete
  8. weee anon. wa kwanza hebu tuelezee vizuri ilikuaje na wewe mpka ukatia mafao yako!!!!! tunyooshee maneno

    ReplyDelete
  9. anon.9:31 ilikuaje jamani hebu fichueni hayo maovu tujue ukweli

    ReplyDelete
  10. Kwa ufupi mi nilikuwa muumini mzuri wa kanisa lake na mtu aliyenishawishi kwenda kusali kwa mwingira alikuwa ni rafiki yangu ambaye ni wakili maarufu hapa dsm, tumekuwa tukijitolea sana kusaidia kanisa kwa hali na mali kwani tulimuamini sana huyu mchungaji, tumeenda hivyo mpaka akatumbua fadhilia zetu hivyo akawa anakuja kutuombea nyumbani, ktk mazingira hayo si rahisi mtu anayoitwa mchungaji na unayemuamini ukamuwekea mipaka ya kuja kutoa huduma ya maombi nyumbani kwangu, hivyo alizoea mpaka akawa karibu sana na familia, wakati mwingine aliweza kuja hata kuongea tu. binafsi nafanya kazi kwenye shirika moja ambalo lipo chini ya UN hivyo huwa nakazi nyingi za kusafiri. kuna siku nikiwa safarini niliamua kirudi mara moja wikiendi haikuwa kwenye ratiba.nilifanya hivyo nikiwa nimewakumbuka sana mke wangu na watoto wangu wawili.nikapanda ndege na kwa bahati nilifika salama uwanja wa ndege dar saa kumi na mbili na nusu. nikachukua tax mpaka maskai ilikuwa saa moja plus..nilipofika tu nilichungulia kwa pizia kwa nia ya kumtania tu wife, sikufikiri jambo baya hata kidogo. chakushangaza nilikutana na mchungaji kamkumbatia mke wangu na wapo kwenye mapenzi kabisa.mbaya zaidi mtoto wangu alikuwa yupo hapo sebuleni anawaaona wanachokifanya. sikuamini nilitafakari kabla ya kuingia. niliona ni jambo la aibu hata kupiga kelele. nilipoingia walishtuka sana kwa sababu hawakutarajia na sikuwasemesha. na hapo ndipo nilipoyambua kuwa Mwingira ni mtu muovu anayehubiri unafiki. kwa hakika ni jambo baya kwani alishindwa aondoke au abaki na mim sikutoka chumbani mpaka saa5 usiku. baada ya kutamani kuongea na watoto wangu..nilikuwa nampenda sana mke wangu.lakini ukweli simpendi tena na nipo naye kwasababu ya watoto. hivyo ndiyo actual stor kwa ufupi

    ReplyDelete
  11. DUH POLE SANA ILA MSAMEHE MKE WAKO SHETANI ALIMZIDI NGUVU

    ReplyDelete
  12. pole sana ila kwanini hukumpiga nondo ya kichwa? bro we siyo hakuna busara kwa jambazi kama huyo

    ReplyDelete
  13. Acheni kuwazushia watumishi wa mungu mambo yasiyo na ushahidi wowote, hata mimi leo naweza toka na kusema chochote as long as kuna uhuru wa kusema. Ingekuwa ni DNA imethibitisha hapo sawa. Pili nyie mnaoongeza hadithi za uongo ooo nilikuwa safari, nafanya UN, UN huna hata gate au gari unafika moja kwa moja dirishani unakaa Manzese nini! Acheni kusema watumishi wa Mungu mtaangamia. DONT JUDGE YOU WILL B JUDGED.

    ReplyDelete
  14. mwingira anakesi nyingi za uzinifu usimtetee. mbona wengine hawasingiziwi toa utando kwenye akili yako..anakesi na mbuna kama unaifuatilia katembea na mke wake

    ReplyDelete
  15. we anoy unaemtetea mwingra fala kweli hata me nilishapataga story yake ana tabia ya kutongoza wake za watu na alaaniwe na wake c ajabu wanamfanyia hvyo hvyo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyo mwanamke nä yy ni kahaba vilevile kwa nini akubali kuzaa nä mwingira wakati alijijua ni mke wa mtu.. mwanaume yeyote ukimlegezea anakula mchongo Bila kujali ni mke wa mtu..

      Delete
  16. imekuwa kama America waeneza ukimwi ni wachungaji

    ReplyDelete
  17. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  18. Kwa kwel cjui tukimbilie wap ka wachungaj ndo hvoo trnaa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad