Shindano la Epiq Bongo Star Search 2013 linafikia ukingoni
leo usiku (November 30), ambapo mmoja kati ya washiriki watano
walioingia fainali atatangazwa kuwa mshindi.
Kila mshiriki ana sifa za pekee ambazo zinamtofautisha na washiriki wengine na huenda ikamsaidia kuibuka mshindi.
Jina moja kati ya majina haya litapamba vichwa vya habari kesho.
Emmanuel Msuya:
Ni mshiriki namba 21 anaewakilisha kanda ya ziwa. Ndiye mshiriki
pekee wa kiume ambaye ameingia fainali akiwa na uwezo mkubwa wa kuimba,
lakini kitu kikubwa kinachomtofautisha na wenzake ni uwezo mkubwa
alionao wa kupiga vyombo vya muziki kama kinanda na gitaa.
Msuya amerekodi wimbo unaoitwa ‘Leo Leo’ ambao ameufanya na Producer Sheddy Clever.
Elizabeth Mwakijambile:
Sifa moja kubwa aliyonayo inayomtofautisha na wenzake ni uwezo wake
mkubwa wa kubadili sauti nakuimba vizuri sauti ya base (ya kiume), mbali
na vocal ya nguvu ya kike aliyonayo.
Mara kwa mara anapoimba unaweza kuifananisha sauti yake na ya mwanamuziki mkongwe Stara Thomas.
Elizabeth amerekodi wimbo unaoitwa ‘Nifanyeje’ uliotayarishwa na producer Lamar wa Fish Crab.
Maina Thadei:
Uwezo mkubwa alionao wa kuimba nyimbo za taarab na miduara umemfanya
kuwa na ladha tofauti na wenzake na kujikombea fans wengi wanaopenda
aiana hiyo ya muziki.
Sio tu aina ya muziki anaochagua, lakini performance yake awapo
jukwaani na mbwembwe za aina yake ni kitu ambacho kitakufanya umuangalie
hadi anaposhuka jukwaani.
Maina amefanya wimbo wa mduara unaitwa ‘Panya Buku’, na ukisikiliza
utahisi unasikiliza wimbo wa msanii mzoefu kwenye miondoko hiyo.
Saa ngapi?
ReplyDeleteHamna msanii hapo ktk mwaka mliochemka bss ndo huu.ata yule wa kushtua hakuna.labda mkata mauno yule na tunavutiwa mauno tu kuangalia kuimba ovyoooooooo kbs.
ReplyDeletekula tano mdau
Delete