Stori: Imelda Mtema
NDOA ya mastaa wa filamu Bongo, George Tyson na Yvonney Chery ‘Monalisa’ iliyovunjika kitambo, ilirejewa na uhai wa saa kadhaa katika shughuli ya kumpongeza binti yao mpendwa Sonia baada ya kupata kipaimara.
Mwandishi wetu aliwashuhudia wawili hao wakionekana dhahiri kuweka tofauti zao pembeni na kujali shughuli ya binti yao iliyofanyika Jumapili iliyopita nyumbani kwa mama mzazi wa Monalisa, Suzan Lewis ‘Natasha’, Yombo –Buza, Dar.
Muda wote walionekana wenye furaha na waliketi kwenye meza moja huku Monalisa akionesha heshima wakati wa kumlisha keki Tyson kwa kupiga magoti.
“Hawa jamani wanapendezana sana wakiwa pamoja. Jamani... mtoto wao amerudisha penzi lao. Ingefaa wakafikiria upya na kuona kuna umuhimu wa kurudiana na kumlea pamoja mtoto wao,” mmoja wa wageni waalikwa alisikika akisema.
Katika kuonesha kuwa kweli hawana bifu, Mona aliamua kumtunza mzazi mwenzake noti nyingi za elfu kumikumi zilizokadiriwa kuwa zaidi ya 200,000 ambapo alisema: “Huwa nawashangaa watu wengi wakiwatuza akina mama kwa kuwalea vyema watoto lakini wanawasahau akina baba. Sasa mimi namzawadia baba Sonia kwa sababu bila yeye, mtoto wetu asingekuwepo.”
Tukio hilo lilivuta hisia za watu na kusababisha shangwe kubwa kuibuka katika sherehe hiyo.
-Globalpublishers
safi.
ReplyDeleteLIKE IT JAMAN
ReplyDeleteInapendeza sana
ReplyDeleteKwani walitengana kwa nini? Nijibuni wadau
ReplyDeleteSababu kubwa ya kutengana kwa hawa jamaa ni kwamba mmoja ama wote wawili walikuwa wabinafsi. Walikuwa wabinafsi kwa maana kwamba hawakujali kwamba mtoto anawahitaji wote wawili ktk kumlea hata kama mmojawao ana mapungufu makubwa kiasi gani. Na wameshindwa kupingana na wimbi la kusambaratika kwa ndoa kwa sababu mbalimbali. Na watakuja kujutia maamuzi yao,VINGINEVYO WATAFAKARI UPYA MAAMUZI YAO. NA MIMI BINAFSI NATAMANI SANA WARUDIANE,KWA FAIDA YA MTOTO WAO NA JAMII NZIMA YA TANZANIA. NAWAPENDA SANA HAWA JAMAA WAKIWA PAMOJA KTK NDOA!
ReplyDeletedemu keshafulia ataenda wapi unafikiri, kila mwanaume anayekuwa anaachana, si lazima arudie makombo. Na jamaa nafikiri si mtanzania ndio maana anamwonea.
ReplyDeleteCheki hata nguo aliyovaa huyo demu yani kafuliiiaaaaaa.
ReplyDeleteUlitaka avae nusu uchi km wngne??km hujui fashion piga kimya.....kitenge kipo sokon kwa ss na Monalisa anajiheshmu cku zoote
ReplyDelete