Mimi ni mama nimeolewa miaka mingi tu(zaidi ya kumi sasa), na Mungu katujaalia watoto,
hapo nyuma tulifungua biashara kadhaa na mume wangu lakini biashara zote hizo zilikufa kutokana na yeye kuchukua pesa kutumia akisema atarudisha halafu harudishi..hili lilisababisha biashara zikafa kwani mitaji ilikufa kutokana na yeye kuchukua pesa halafu harudishi.. basi mchezo ndio ulikuwa huo kwa biashara zote mwishowe nikaamua kukaa bila biashara kwani kwa kiasi kikubwa ni kama vile tulikuwa tunamfanyia yeye..pamoja na hivo vibiashara mimi na yeye wote ni waajiriwa..
Sasa baada ya kuacha biashara za familia mimi nikaanza biashara yangu mwenyewe pasina kumwambia mume wangu, nimefanya kwa siri hiyo biashara na kwa kweli namshukuru Mungu inaenda vizuri kwani nilianza na mtaji mdogo lkn sasa nina turnover nzuri tu, kwa kweli namshukuru Mungu..
Sasa biashara imekua na wakati mwingine inanibidi kusafiri nje ya nchi kwa ajili ya hiyo biashara yangu...nimeshafanya mara kadhaa lakni namdanganya naenda kikazi (nimeajiriwa pia) while in fact nasafiri kwa mambo yangu tu..
na hapo hapo nimeweza kununua plot 3 na nyingine moja nimeanza kujenga sijamwambia, kwani pesa hizo napata kwenye biashara yangu na yeye haijui hiyo biashara..na zenyewe hizo plot na nyumba nayojenga sijamwambia sababu naogopa nikimwambia ataanza kunihoji umepata wapi hela wakati nafanya biashara ambayo namshukuru Mungu kwa kweli inanilipa kdg, nilianza kama utani tu lakini inaenda vizuri..(sio sembe jamani) ni biashara ya kawaida tu ya kununua bidhaa na kuuza..
pia nilinunua gari ambayo nilimdanganya nimekopa kazini lakni ukweli sijakopa popote, nimenunua tu kwa vihela vya mshahara pamoja na faida kutokana na hiyo biashara nayofanya..
sasa nifanyeje ndugu zangu, nimwambie mume wangu au niendelee kuuchuna tu? naogopa nikimwambia ataanza yale yale ya kukopa hela halafu harudishi...kwa ujumla hana discpline na hela, ana matumizi mabaya na huwa anaishiwa na kuanza kukopakopa watu, kitu ambacho nimemdhibiti lkn nimeshindwa..
naogopa nikifa leo sijui itakuwaje, huyu ninayefanya nae biashara hatanidhulumu? (kuna mtu nimemuajiri, tunaelewana sana, lkn hajui km mume wangu hajui kwani sijamwambia hayo,)...watoto wangu sio wakubwa wa kuwashirikisha vitu km hivyo kwa hivo hawajui..
lakini nimemwambia kaka yangu na nimeandika usia, na pia kaka yangu anajua hizo plot zote nilizonunua na nyumba nayojenga, nimemuonyesha na nimemwambia kabisa kuwa shemeji yako(yaani mume wangu) hajui...nina dada yangu ambaye ningeweza kumwambia na yeye lkn si mtu mwenye kutunza siri anaweza akaropoka ikawa tabu kwa hivo sijamwambia..
jamani wadau niko sawa au? hebu nisaidieni mawazo
-Jamii Forums
Kama kweli unafanya biashara halali anza kumwambia taratibu ila mwambie pesa umekopa japo ni zako,usimshirikishe katika biashara zako zote kwani unajua hana displine,iwapo utakufa hata ukipoteza utapoteza kidogo,hongera kwa kuisogeza akili yako!
ReplyDeleteNimekupenda...ni vizuri umemshirikisha kaka yako..na usia pia...
ReplyDeleteUsiliambie, kula buyu mama fanya yako, nyumba ikiisha, mwambie akizingua muame uendelee na yako!
ReplyDeleteusimwambie piga kimya kwa kua kaka anajua
ReplyDeleteHongera yako
ReplyDeleteHiyo ni biashara ya ngono tu kumamae wewe kilichokufanya ubinue mkia nini ?hooo biashara yangu heeeee nasafiri halafuuuuu nanhiiiiii mme wangu hajui kumbe unatomba
ReplyDeletewewe nina wasiwasi ndodizaini ya jamaa mume wa mleta mada...asante kwa kuniongezea siku za kuishi nimechekaje? nikirudi kwnye maada naungana na waliosema mshirikishe taratibu. na ni vizuri majina ya plots yawe ya watoto na wemwenyewe angalau moja mana ndugu nao wakiamua hawakawii...kama mama mzazi pia yupo mweke pia kama mmiliki kwa ajili ya wajuu zake in case of anything (msimamazi) otherwise BRAVO MY FELLOW LADY!
DeleteMaelezo yako.mazuri na hongera sana.mbona picha haifanani na story me nilianza kuwazia biashara nyngne.hongera dada.uko sawa
ReplyDeleteAchana nae!
ReplyDeleteMaelezo yako yako vzur but hujaainisha ni biashara gan ingependeza sana km ungeainisha. ila 4to yako ina2tia was x2. na biashara yako ambayo huja2ambia!
ReplyDeleteusimwambie biashara hiyo ni yako na unamjua mtu mwenyewe ni matumizi mabaya atakurudisha kulekule
ReplyDeleteUNAJIJU.
ReplyDeletehv mmilik wa hii blog ni msichana or mwanaume ?
ReplyDeletehongera natamani lingekuwa ni demu langu lichapa kaz hvyo
ReplyDeleteNaona nchi za afrika ndiko kuna matatizo haya,Amerika na Ulaya haya matatizo hayapo na shida umejia shida ya mume wako na humfundishi ,abadilike hakuna Baraka hapo ,uwe wazi tangu mwanzo angekuwa amebadilika,pia unaonyesha mama sio mwaminifu japo ni ujasiri wa kizamani,ni kheri usinge shirikisha mtu yeyote ,hata kaka yako kwa sababu mwisho wa siku anaweza kukujeuka japo ni kaka yako na ndoa yako ikawa hatarini ni ngumu kukushauri ,na angekuwa mume wako kafanya hivyo ungejisikiaje?
ReplyDeleteso umemuamini kaka yako kuliko mumeo? huoni umeruka mkojo umekanyaga mavi!!
ReplyDeletemwambie
ReplyDeleteHutaki mwambia mumeo just bcoz biashara uifanyayo haitompendeza possibly ukahaba . Kama ni biashara halari mueleze na ili asiingilie sana Cash mueleze upo share even na hiyo bro wako
ReplyDelete