NAPE AMWAGIZA MSAJILI WA VYAMA TANZANIA AIFUTE CHADEMA

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye amemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kukifuta Chadema kwa madai kuwa, kimeshindwa kusimamia katiba yake kwa kutofanya uchaguzi wa ndani zaidi ya miaka zaidi ya kumi.
  
Nape alisema chama hicho kimejaa viongozi waongo, wapenda vurugu na wanaotaka kuvuruga amani ya nchi kwa kisingizio cha Katiba Mpya na kwamba, wamesahau katiba iliyopo imedumu kwa miaka 50 na haijawahikuwagombanisha wananchi wala kuwavuruga.
Hata hivyo, jitihada za kumpata Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chadema, John Mnyika kuzungumzia tuhuma hizo jana jioni kwa simu yake haikufanikiwa.
Akihutubia wakazi wa Manispaa ya Songea jana, Nape alimtaka Msajili wa Vyama vya Siasa kukiagiza chama hicho kufanya mkutano wa uchaguzi haraka kikigoma akifute na kwamba, asipofanya hivyo wao wataendelea kumsema na kumchukulia hatua.
SOU
Aliongeza CCM kilifanya uchaguzi wake 2012 na kupata viongozi wapya, lakini Chadema imeshindwa kusimamia katiba yake ambayo ilipeleka kwa msajili wa vyama na kuisajili kwa kuivunja wao wenyewe kwa kuendesha chama isivyo.
Nape alisema chama hicho hakifai kuongoza nchi, kwani kimeshindwa kusimamia katiba yake na kuifuata hakiwezi kuongoza wananchi.
“Kwa sababu Msajili wa Siasa ni mlezi wa vyama vyote vya siasa ikiwamo Chadema, namuomba akiagize chama hicho kifanye uchaguzi kwani wao wanajiita wanademokrasia wakati wanashindwa kufuata demokrasia kwa vitendo,” alisema Nape.
Kuhusu malalamiko ya wananchi, Nape alisema wananchi wamekuwa wakilalamikia utendaji mbovu wa viongozi wa Serikali na kwamba, yana msingi kwani inasikitisha licha ya Ruvuma kuwa ni mkoa unaolisha nchi, hakuna mawazili wa kilimo ambao wamefika mkoani hapa.

---MWANANCHI
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwa maelezo yako muh Nape mi naona chama cha kwanza kufutwa ingekuwa CCM kwani wezi,Mafisadi na wala rushwa wamejazana huko ccm

    ReplyDelete
  2. Ni kweli kabisa kwa maelezo ya Mheshimiwa Nauye. Chama ambacho kinapigania Katiba ya Nchi wakati Chama chenyewe kimeshindwa kusimamia na kuifuata Katiba yake, hicho ni Chama cha aina gani????......Ni kweli kabisa hicho Chama kikipewe majukumu ya kuendesha Nchi kitaweza kuifuata Katiba ya Nchi??????

    ReplyDelete
  3. Siasa,siasa,siasa.....Bado kabisa wapinzani wa kweli nchi hii hakuna ni maneno tu na uchonganishi usiokuwa na tija wapo kimaslahi zaidi hata ya hiyo ccm,wachagueni muone kufanya tu uchaguzi ndani ya chama kupata viongozi wengine ni mizengwe,waliopo hawataki kuachia ngazi kuna nini hapo kwenye hivyo viti?ukijaribu kusema hawakawii kusema huyu ni mamluki anatumwa na ccm,wapii wezi wote hao,na wala kisifutwe kitakufa taratibu hakuna lolote,hao wanaosema ccm mafisadi watoto wao ndio wanasoma shule za kata bila malipo,hao hao wameteremshiwa kuunganishiwa umeme,hao hao wanasafiri leo vizuri ktk barabara zilizojengwa chini ya serikali ya chama cha mapinduzi,hawayaoni ni mengi tu kama kuna mafisadi si wote wapo viongozi safi na mpaka leo bado wanawaongoza,kama sivyo wasingechaguliwa na wananchi,ila anaonekana wanafaa na kwa hali hii CCM hawatatoka madarakani kwani upinzani unaonyesha udhaifu 2015.ccm watapita kwa kishindo kikubwa someni alama za nyakati,wapinzani jipangeni mje na hoja zinazotekelezeka na si vinginevy

    ReplyDelete
  4. Duh!!!!hili nalo neno!tutajipanga unapatikana wapi tukupe kazi uwe msemaji wa chama?

    ReplyDelete
  5. nape acha ujinga hata cc tuna macho na tunaona ujinga wenu unaemfanya mjinga nani? elimu yako haijakukomboa bado!

    ReplyDelete
  6. Sasa wewe nape ni kama nani,wakutamka eti chama flani kifutwe,unataka kufundisha watu kazi,ama ccm ndo kaz yenu huwa mnasajili vyama vya siasa,acha ujinga wewe nauye

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad