RIHANNA NA DRAKE SASA NI ZAIDI YA KAKA NA DADA...MASHABIKI WASEMA KUNA JAMBO
0
November 17, 2013
Inavyoonekana Rihanna ni ‘team drake’ na Drake ni ‘team Riri’ na hilo tu linatosha kuwafanya wawe zaidi ya marafiki, kwasababu inavyoonekana ‘urafiki’ wa wawili hao unazidi kuimarika kadri siku zinavyozidi kwenda.
Ikiwa ni siku chache toka Drake aonekane katika tour ya Rihanna huko Dallas, alamisi wiki hii Rihanna naye amerudisha fadhila kwa kuhudhuria show ya Drake huko Houston, Marekani.
Baada ya show hiyo wawili hao ambao walikana kuwa na uhusiano wa kimapenzi japo zipo dalili nyingi zinazoashiria kuna kitu kikubwa kinaendelea kati yao, walielekea katika club moja ya strippers ambako kwa mujibu wa TMZ walimwaga mvua ya pesa $12,000 kwa ujumla kwa kinadada wanaocheza nusu uchi (strippers), na chanzo kimoja kiliiambia TMZ kuwa baadae Drake na Rihanna waliondoka pamoja mishale ya saa 11 alfajiri.
Bongo5
Tags