SAKATA LA UBAKAJI LAENDELEA, PROFESA JUMA KAPUYA ABURUZWA POLISI KWA TUHUMA ZA KUBAKA.

HATIMAYE binti anayedaiwa kubakwa na Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), amefungua jalada Polisi dhidi ya mbunge huyo.

Habari za kipolisi ambazo Tanzania Dama limezipata, zinasema kuwa binti huyo ambaye anadai kubakwa na kisha kutishiwa kuuawa na Profesa Kapuya, amefungua jalada namba OB/RB/21124/13 katika Kituo cha Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.

Harakati za kufungua jalada hilo zilianza juzi jioni na kuendelea hadi jana ambapo polisi walitumia zaidi ya saa 12 kumhoji binti huyo anayedaiwa kubakwa ili kupata ukweli wa sakata hilo.

Akiwa kituoni hapo, binti huyo alikutana na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi ya Oysterbay (OCD) na OC-CID wake na kutoa maelezo ya awali kabla ya viongozi hao kumruhusu ayaweke malalamiko yake katika maandishi kwa ajili ya kufunguliwa mashitaka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius  Wambura, alikiri polisi kufungua jalada hilo na kuongeza kwamba hivi sasa wanafanya uchunguzi kubaini kama ujumbe ulio katika simu ya binti anayedai kubakwa na kutishiwa maisha unatoka katika simu ya  mbunge huyo.

“Tumefungua jalada, lipo kwa ajili ya uchunguzi na tukibaini kuwa ni nani anahusika na tuhuma hizo tutamsaka na kumkamata popote alipo,” alisema Wambura.

Habari zaidi zinasema polisi wamechukua namba ya Kapuya inayodaiwa kutumika mara kwa mara kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa binti huyo, akitishiwa kuuawa.

Simu hiyo namba 0784993930 inayodaiwa kumilikiwa na Profesa Kapuya, mbali ya kutuma ujumbe mfupi wa maneno ya kutishia kuua, pia ndiyo inayodaiwa kutumika kutuma pesa kwa njia ya mtandao kwenda kwa binti huyo.

Moja ya ujumbe wa vitisho unaodaiwa kutumwa na Kapuya kupitia simu hiyo unasomeka hivi;  “Mkiuawa itakuwa vizuri…itawapunguzia gharama za kuishi, usitake kugombana na serikali mtoto mdogo kama wewe, sisi ndiyo wenye nchi yetu, mwenye hilo gazeti ni Mbowe sasa mwambieni nyumba ya kuishi si mmemuingizia hela leo? Mnatumika tu bure watu wanaingiza hela nyingi, ila mmenitibua lazima niwaue wiki hii haitaisha, nitapiga kambi kote, jana si wamekuficha tuone utalindwa milele maana washatengeneza hela, lazima mvae sanda tu hilo sio ombi ni wajibu wenu, mnajitia na nyie mafia watoto siyo, watoto wetu wanauza unga nani anawakamata? Nani atapingana nasi.”

Pia simu hiyo iliwahi kutuma ujumbe mfupi wa maneno unaosomeka hivi; “Ni lazima nitakuua wewe na ndugu yako na atakaetaka kuwasaidia, huyo Sitta asijiingize kwenu, yaani nitakuua tena sijui leo mtalala wapi? We unadhani nani atakaenifunga, ndo nishakupa ukimwi, sasa nakutaka uache mara moja kuongea na mtu, nitakuwinda popote tuone.”

Mbali na kutishia kumuua binti huyo na ndugu yake na mtu mwingine yeyote atakayejitokeza kumsaidia, Tanzania Daima limenasa baadhi ya mawasilino ya simu za ujumbe mfupi wa kuhamisha fedha kutoka kwa Profesa Kapuya kwenda kwa binti huyo ambaye mbunge huyo alikana kumfahamu na kwamba hajawahi kukutana naye.

Tanzania Daima  pia lilinasa mawasiliano ya kutumiana fedha kutoka kwa Kapuya kwenda kwa binti huyo.

Baadhi ya mawasiliano hayo ni pamoja na yale yaliyofanyika Agosti 31 mwaka huu kupitia simu ya Kapuya ambapo alituma sh 300,000 kwenda kwa binti huyo kama sehemu ya makubaliano ya kutuma pesa kila mwezi kwa ajili ya matunzo.

Mawasiliano hayo ni kama ifuatavyo: U26UG365 Imethibitishwa Umepokea Tsh 300,000 kutoka kwa JUMA KAPUYA Tarehe 31/8/13 saa 3:28 PM Salio lako la M-PESA ni Tsh 300,000

V04EU470 Imethibitishwa Umepokea Tsh 400,000 kutoka kwa JUMA KAPUYA Tarehe 24/9/13 saa 2:38 PM Salio lako la M-PESA ni Tsh 400,040.

R93NY448 Imethibitishwa Umepokea Tsh 505,000 kutoka kwa JUMA KAPUYA Tarehe 21/6/13 saa 11:07 AM Salio lako la M-PESA ni Tsh 505,000.

Kutokana na mfululizo wa habari hiyo, Profesa Kapuya kupitia kwa wakili wake Yasin Memba, ametishia kuliburuza mahakamani Tanzania Daima endapo halitamwomba msamaha ndani ya siku saba.

Source: Tanzania Daima

Post a Comment

19 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Uwiiiiii! Mwisho wa ubaya Ni Aibu! Kapuya magereza inakuhusu! Wewe Ni gaidi! Ukimwi uwiiiiiiii! Mbona wakuchelewesha Una maana Kuishi jehanamu Ni kwako!!!

    ReplyDelete
  2. Hatari aiseee hawa ni viongoz wetu, tunapoelekea Mungu atunusuru na vizazi vyetu vijavyo

    ReplyDelete
  3. Wale magaidi wa Global Publisherz walioanza kupindisha ukweli wataumbuka tu. Time will tell, idiots!!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. chezeiya hongo wewe yaan ktk pesa hta ukwel utapindshwa global na lile mburula wote cjui nao walirushiwa ktk cm wamsafishe prof. mmmh

      Delete
  4. Kapuya nilikuwa sitaki kukuhukumu lakini mbona kama kuna ukweli!kweli ikibainika ahukumiwe hata kunyongwa huu ni uuwaji kabisa

    ReplyDelete
  5. Kila siku nasema Afrika atuna viongozi na Ndiyo maana atupati maendeleo ili swala siyo la kufumbia macho, Wanaalibu elimu ili wawezi kuwalubuni dada zetu,ata uyo katibu kuu wa elimu nae ndio michezo yake pamoja na uyo mkurugenzi wa Benk tunawajuwa unawaona, Hmm!! Profesa kweli hii ni aibu ya wasomi na Nchi pia, Na nyie dada zetu achene Tamaa fanyeni kazi na MUNGU atawasaidia

    ReplyDelete
  6. Bingwa wa ushirikina na kafara hapo polisi utaumbuka tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha kuwa mtumwa wa ushetani wewe mdau,kwahiyo unaona ushirikina ndio uko juu kuliko aliyekupa pumzi?

      Delete
  7. Babu seya amefungwa maisha kwa kesi kama hiyo. Kama kweli mnafuata haki na Kapuya mfungeni maisha kwa ubakaji, kuambukiza UKIMWI makusudi na kutishia kuua

    ReplyDelete
  8. Apimwe HIV akiwa nayo well he is guilt

    ReplyDelete
  9. KAPUYA:Huyoo!!!segerea.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wala haendi segerea kashakwambia hii nchi ni Yake na watoto wao wanauza UNGA hakuna wa kuwakamata.upo mdau?wataenda segerea wakina babu seya na papi kocha mutoto ya ilala.

      Delete
  10. we Kapuya ni muuaji aiseee..!

    ReplyDelete
  11. Mimi ntachangia baadae ngoja kwanza nkawacheki P sq...

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kuna ukwel kuhusu agenda kama mh.kapuya kubaka au ndo life la kisiasa lilivo?

      Delete
    2. Kubaka sio lazima umkamate mtu kinguvu,kutembea na under 18 tena na zawadi ya virusi ni ubakaji,kosa la pili kuua Kwa kukusudia,unanijua una Ukimwi unaambukiza watu makusudi.

      Delete
  12. MZEE MZIMA KAUMBUKA KAPUYA

    ReplyDelete
  13. the beautiful ones are not yet born.......hiki kitabu nlikisoma nikiwa o'level na mambo yanayotokea yanareflect ukweli wote wa dunia ya sasa........fuck you kapuya

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad