Kikao kinachojadili maendeleo ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Kanda ya ziwa Mashariki (Mara,Simiyu na Shinyanga) kimemtimua Mbunge wa Maswa Magharibi John Magale Shibuda baada ya kupiga kura ya kutokuwa na imani naye muda mfupi uliopita jioni hii.
Shibuda ambaye alihudhuria kikao hichou kama mbunge wa Kanda hiyo alijikuta akipatwa na zahama hiyo baada ya mjumbe mmoja kutoa hoja kwa Mwenyekiti wa Kikao hicho kwamba Shibuda atoke nje.
Mjumbe huyo alisema Shibuda ni mamluki na kibaraka wa CCM hasa kutokana na matamshi yake kadhaa dhidi ya Chadema na mwenendo wake usioridhisha ndani ya chama.Aliongeza kwamba Shibuda alikuwa kwenye kikao hicho kwa lengo maalum la kukusanya habari na kupeleka CCM.
Hatimaye hoja ya mjumbe huyo iliungwa mkono na wajumbe wote na hatimaye ikapigwa kura ya kutokuwa na imani naye.
Shibuda alikubali kuondoka ndani ya kikao hicho kwa aibu kubwa na hatimaye mkutano umeendelea
Source:JF
begining of the end for chadema
ReplyDeleteNi mawazo yako mgando tu! kakambia nani Shibuda ndo katiba ya CHADEMA? chama imara lazima kiwe na maamuz magum bila kuangalia sura.
Deletewell done
ReplyDeleteMaamuz magum Ni muhim hata chama kikiwa na watu kumi kitsonga tuu
ReplyDeletehcho chama mngewaachia wenyewe wachaga wengne mtanyanyasika tu
ReplyDeleteChadema whre are u going sasa?
ReplyDelete