SHOW YA RAPPER WA KENYA CANNIBAL YABUMA DUBAI, ATUMBUIZA MBELE YA VITI

Show iliyokuwa ikiongelewa sana ya rapper wa Mombasa, Kenya, Cannibal Shattah mjini Dubai imebuma vibaya.

Mahudhurio yalikuwa hafifu kiasi cha waandaji kula hasara na kushindwa kurudisha gharama walizotumia.

Cannibal alidaiwa kushikiliwa kwenye hoteli aliyokuwa amefikia kwa kushindwa kulipa gharama na meneja wake aitwaye Waziri aliambulia kichapo kutoka kwa Wakenya waiishio Dubai na kujeruhiwa usoni.

Cannibal alitumbuiza kwenye ukumbi wa at RockCity Club uliopo kwenye hoteli ya  Howard Johnson, mjini Dubai, November 8.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad