SIRI IMEFICHUKA..DIAMOND NA PENNY NI KUMBE NDUGU

Na Shakoor Jongo
MAAJABU! Jambo zito limefichuka kuwa mastaa walio katika uhusiano wa kimapenzi, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Penniel Mwingilwa ‘Penny’ ni ndugu, AMANI limepekua na kupata mkanda kamili.

Diamond kwa sasa ndiye mwanamuziki aliye matawi ya juu zaidi kuliko yeyote kwenye Bongo Fleva, akisumbua vibaya na kibao chake cha Number One wakati Penny akiingiza mkwanja kupitia utangazaji katika kituo cha Runinga ya Dar es Salaam ‘DTV’.

ISHU YABUMBURUKA!
Sosi wa karibu, ndani ya familia ya Diamond alinyetisha kwamba, Diamond na Penny ni ndugu wa damu lakini jambo hilo limefahamika hivi karibuni na hivyo wanahaha namna ya kuzima aibu hiyo.

Kwa sharti la kutochorwa jina gazetini, sosi huyo alisema: “Ndugu kwenye familia wanagongana. Wanajaribu kufichaficha hili jambo, lakini inashindikana. Unajua kinacholeta shida zaidi ni kwamba Diamond na Penny watakavyokuwa baada ya uamuzi kupitishwa.”

Alisema, pamoja na ukweli huo kugundulika bila shaka kuwa ni ndugu, bado kuna ugumu wa wapenzi hao waliozama kwenye dimbwi la mahaba kisha kuvunja amri ya sita, kuachana na kubaki wakiheshimiana kama kaka na dada.
“Tatizo ni je, Diamond atakubali kumchukulia Penny kama ndugu yake? Kama atakubali na Penny naye atakuwa tayari? Wote kwa pamoja wanaonekana kama wanapingana na jambo hilo,” alisema.

UNDUGU WENYEWE UKOJE?
Akieleza aina ya unasaba wa Diamond na Penny, sosi wetu huyo alisema, bibi mzaa mama wa Diamond na bibi mzaa mama wa Penny, wamezaliwa na mama mmoja.

Hapa anafafanua: “Kwa sababu hiyo sasa, unaweza kuona kuwa, wale ni sawa tu na mtu na kaka yake. Tena wako ndani ya ukoo kabisa, sema hao mabibi, kila mmoja alikuwa na baba yake, walichangia mama tu.

“Familia imejiridhisha kabisa, halafu isitoshe imeonekana kuwa, undugu wa kuchangia mama ndiyo wa uhakika zaidi kuliko wa baba ambao mtu anaweza kubambikwa hata mtoto asiye wake. Kifupi Penny na Diamond ni ndugu. Sema ndiyo hivyo historia za wazazi wao zinashangaza mpaka basi.”

Kwa mujibu wa sosi wetu, majina ya bibi hao wanaounganisha undugu ni Khadija Said Abas (bibi yake Penny) na Tatu Omar (bibi yake Diamond), wote kwa sasa wametangulia mbele ya haki.

MAMA DIAMOND ACHEKELEA
Wakati jambo hilo likileta msuguano wa kimyakimya ndani ya familia huku wengi wakitaka undugu huo uheshimiwe na uhusiano uvunjwe kabisa, imeelezwa kuwa mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ anafurahia undugu huo

“Kinachoshangaza sasa, mama Diamond amefurahi sana na amezidisha mapenzi yake kwa Penny, ndiyo maana hataki kusikia mwanaye anakuwa na mwanamke mwingine zaidi ya Penny.

“Mwenyewe anasema, kwanza undugu siyo wa karibu sana hivyo haina madhara lakini pia anajua Diamond atampenda, kumheshimu na hatamnyanyasa kwa sababu ni sehemu ya damu ya familia yao,” sosi aliendelea kutiririka.

HAPA AMANI, KULE DIAMOND
Amani lilifanya juhudi za kumsaka Diamond katika simu zake zote za mkononi bila mafanikio, likahamia kwenye mitandao ya kijamii, likamnasa ambapo awali mahojiano yalikuwa na kigugumizi lakini baadaye mambo yalikuwa hivi;
AMANI: Mzee vipi, mbona hupatikani kwenye simu zako zote? Kuna jambo nataka kukuuliza bwana mkubwa.

DIAMOND: Niko Nigeria. Vipi, kuna nini tena?
AMANI: Kuna stori fulani... eti ni kweli bibi yake Penny mzaa mama na bibi yako wewe ni ndugu wa damu kwa maana wamezaliwa na mama mmoja?
DIAMOND: Yeah but wamechangia mama, kila mmoja na baba yake.

AMANI: Kwa hiyo Penny ni dada yako kiasili si ndiyo?
DIAMOND: Yap!
AMANI: Duh! Majanga... kwa hiyo unatembea na dada yako wa damu?
DIAMOND: Nilikuwa najua basi kaka?!

AMANI: Kwa hiyo sasa baada ya kugundua hivyo, unaachana naye au?
DIAMOND: Kama nilivyokuambia, niko Nigeria... halafu niko gym sasa hivi, nitakutafuta nikitoka.
AMANI: Sawa, naomba ujibu hili swali la mwisho. Tumesikia kuwa, mama yako anampenda sana Penny, ni kwa sababu amegundua kuwa una undugu naye?

DIAMOND: Ha! Ha! Ha! Nikitoka gym nitakupigia simu tuzungumze vizuri.
Diamond hakufanya hivyo. Hata alivyotafutwa baadaye kwenye mtandao huo, pia hakuonekana kuwa hewani.

PENNY MIKONONI MWA AMANI
Penny alipopatikana juzi Jumanne, kwa njia ya simu alielezwa ilivyo ambapo alisema: “Ni kweli Diamond ni ndugu yangu wa damu. Tumegundua tukiwa tayari tumeshakuwa wapenzi.

“Hakuna jinsi tena, sanasana naona kama mapenzi yetu ndiyo yamezidi kuimarika. Nampenda sana Diamond wangu na sababu hiyo haitoshi kututenganisha maana kama ni makosa tayari yameshatokea.”

MAMA DIAMOND
Kwa upande wake mama Diamond, baada ya kusimuliwa kila kilichofika mezani mwa Amani na kutakiwa kueleza msimamo wake alijibu kwa kifupi: “Ndiyo ni kweli unayosema, lakini kwa sasa nipo huku Kariakoo (Dar), sipo kwenye nafasi nzuri ya kuzungumza. Njoo nyumbani jioni, tuzungumze vizuri.”

Diamond na Penny wamekuwa kwenye penzi lenye kasheshe nyingi kufuatia mwanamuziki huyo kuhusishwa na wanawake wengine akiwemo aliyekuwa mpenzi wake wa zamani, Wema Isaac Sepetu.
Chanzo:Global Publishers

Post a Comment

20 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Aah tumewachoka hawa nao

    ReplyDelete
  2. Na waendelee tu hakuna shida,undugu wenyewe ni wa mbali.

    ReplyDelete
  3. Jamani hiyo sio sababu ya kuvunjika kwa penzi lao coz cyo ndugu wa mama mmoja wala baba mmoja. Hapo wanafaa kuowana bila wacwac

    ReplyDelete
  4. Jamani hakuna issue zingine mjini khaaa kutwa diamond,penny n wema aaahhh munaboaa jamani khaaa waacheni waishi maisha yao.

    ReplyDelete
  5. Kiukweli hadithi za hawa watu zinaboa everyday wao tu ndo kwamba wataalam wa mapenzi au

    ReplyDelete
  6. Tumewachokaaaaaaaa hawa watuuuuuuu hakuna stori za mastaaa wengineeeeeee?

    ReplyDelete
  7. Hana loloteeee kaona Mali zipo ndio anajidai anampenda ndomo,kipindi kileeeee cha umbagala alikuwa anamcheka shoga Yake wema eti diamond Yuko too local kuwa na wema.mjini chuo kikuu.

    ReplyDelete
  8. Magazeti Kwa chumvi mmmh mi ni ndugu ya penny lakini hii habari ndio naisikia Leo kuwa diamond ni ndugu yetu.labda.

    ReplyDelete
  9. Shit! Pumbavu kabla, kwenye hela undugu hakuna,Hiyo Penny hana lolote anashobokea noti za Hiyo jamaa. By Malanga A N

    ReplyDelete
  10. Penny bwana nimechekaaaa ALIVYOSEMA DIAMOND WANGU PESA KITU KINGINEEEEEEEE MAJINA YOTE DIAMOND ATAITWA.wallai

    ReplyDelete
  11. Mama mkwe nae kasharogwa kweli penny mtangA kweli.Alishasema mwaka huu tutamjua yeye ni nani,olewa bibi weee tupumzike kucoment Umu.

    ReplyDelete
  12. Hahahan ngojen couple ya nguvu inakujaaaaa sipat pichaaa mieeeee domo tupa kureeeee nw hbari za chini ya uvungu ni mafamee na A.Kk naona kuchelewa jmn....sipat pic huyo mtoto watakaemzaaa.....domo ndo mwisho wako huooooo

    ReplyDelete
  13. Hawawezi koana bwana ao ni ndugu kabisa mama mdogo na mama mkbwa mtatia aib hyo familia yao ndg kuoana loo

    ReplyDelete
  14. Wabongo ndio maana hatuendelei Kila kukicha diamond/wemma/penny. Who gives a phage tuck about them. Nigga plz

    ReplyDelete
  15. Watazaa chura mwaka huu

    ReplyDelete
  16. udugu gani huo wa kuvuta na kamba huo ndugu ni nasaba kutoka kwa wazazi wa kiume bana

    ReplyDelete
  17. diamond na pennyyy mnadanganyana kama nimechoka ya keisha.....

    ReplyDelete
  18. undungu wa mbali huo hata si first cousin wanaenza kuoana

    ReplyDelete
  19. mxiuuu.. nlifungua nkajua story ya maaana, 2pa kule mxiu

    ReplyDelete
  20. hivi diamond anauboo tofauti na wanaume wengne au???

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad