TAJI LIUNDI " SIKU NILIPOPATWA DHARURA NDIO SIKU MAREHEMU RANKIM RAMADHAN AKAPITILIZA KULALA NA KUFUKUZWA RADIO ONE"

Jana nilienda kutoa heshima za mwisho kwa rafiki yangu Mzee Dj Rankim Ramadhani Nyamka. Nashukuru kwa ukaribisho wake Saigon hadi kwa Mama Mzee. Bila miwani hakunitambua, lakini alinifahamu kwa jina. Akanihudhunisha sana. "Taji, nilikuwa naitwa Mama Mzee, sasa Mzee kaondoka, nitaitwa nani mimi?" Dah. Ngumu sana. Baadaye nikaomba vijana wenzangu katika media tupige picha ya ukumbusho. Kuna mambo mengi sana nilitafakari nikiwa pale. Jinsi maisha yalivyo maua. Nikawaangalia wenzangu. Wengi nawafahamu tangu wanaanza maisha, kila mmoja wetu ana hatua kapiga na wengine wameganda au kudidimia. Nikamkumbuka Rankim. Kipenzi cha wasikilizaji. Hodari wa Udj. Mcheshi. Sio mgonvi wala mbishi. Sauti nzito ya mkwaruzo. Simple, kwa vile hakuwa na makuu ya mambo yang'aayo ktk maisha! 
Ila, alikuwa kakolea kwenye pombe. Sehemu kubwa la anguko la rafiki yangu. Hili nalikumbuka kwa vile alinifundisha uDj akiwa mara nyingi kalala hoi chini ya meza ya utangazaji ananiongoza jinsi ya kupandisha mabolingo. Siku nilipopatwa dharura ndio siku akapitiliza kulala..akafukuzwa kazi Radio One. Ikawa taaabu kupata kazi ya kudumu tena. Baada ya hapo maisha ya Mzee yakawa mihangaiko ya huku na kule. Sisi, tuliomzika, bila shaka kwa wakati fulani kila mmoja wetu alijaribu kumshika mkono. Lakini hakika kabisa, na hili ndio somo..tayari tumeshikwa na tunabeba mengi mazito ktk maisha yetu binafsi. Mabegani, mioyoni, mifukoni, akilini. Utu uzima unadai uwajibikaji. Watu huchoka hata pale moyo unapopenda sana kusaidia. 
Nafahamu sio kawaida kuandika hivi au namna hii baada ya mtu kupita, lakini natambua mwenyewe nilichomudu wakati wa uhai wake. Labda ningejitahidi zaidi. 
Nimejifunza kwake. Nilimpenda sana. Na sasa....maisha yanaendelea!!!!
RIP Zipompapompa!

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ya nini kumsema marehemu vibaya wengine hata tulikua hatujui hilo unawatia uchungu familia yake sio vizuri wandungu muheshimu maisha yake kuna mengi mazuri alifanya mbona unashikilia bango na pombe? acha hizo kaka kila anaefariki tukiamua kuongelea mapungufu yao tu si tutakatishana tamaa humu duniani? heshima kitu cha bure

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha kulaumu ww, kila jambo linalomtokea binadam duniani ni somo kwa wanaobaki duniani. Liundi hajakosea kuandika mapungufu ya marehemu ili iwe fundisho wa wachapa ulabu kazini. huwezi lala sehemu ya kazi ukasifiwa. Na kama ww unamazuri yake basi tundika hapa hapa tusome na tumuige pia. Kufa ni lazima kwa hio usitishe watu eti oooh muheshimu marehemu, kila mtu marehemu mtarajiwa so hakuna jipya.

      Delete
    2. una akili wewe hizo ni hisia za mtu kwa jinsi alivyokuwa anamjua kwani kumsema mtu anakunywa pombe ni vibaya au unadakia

      Delete
  2. Well done Taji Liundi,umetoa somo kubwa sana kwa wanaopenda kudharau kazi

    ReplyDelete
  3. Wewe Taji ulikuwa wapi kumsahihisha marehemu pale ulipokuwa unaona anaenda mrama. Ni kitu gani cha maana ulikifanya au kumsaidia marehemu pale ulipokuwa unaona anaenda mrama. Leo hii bila ya aibu unaanza kumsimanga marehemu. Unatueleza marehemu alikuwa analala chini ya meza ya matangazo akiwa amelewa chakari lakini wakati huo huo ni huyo mlezi wa kupindukia ndio aliyekuwa anakuelekeza namna ya kuchanganya muziki, na wewe kwa maslahi yako na bila ya aibu ulikuwa unanufaika na mchango wake kwako bila ya wewe pia kufanya juhudi za kumsaidia kimawazo aachane na hizo pombe. Na hata japo kumueleza ya kuwa it was unprofessional kwake kuja kazini akiwa amelewa. Sasa leo hii bila ya aibu unatueleza weaknesses za marehemu na kutuambia ya kuwa pengine ni pombe ndizo zilizomuua.
    Ninachotaka kusema ni kuwa wewe ni mnafika mkubwa. Na pia ni ndumi la kuwili. Wewe ni aina ya watu ambao mnajiona kama vile mko so perfect katika maisha kulinganisha na watu wengine. Unajiona kama vile una mafanikio saaaanaa kuliko watu wengine kitu ambacho sio cha kweli. You are just an ordinary person ambaye una ganga njaa kama watu wengine na pia wewe sio kwamba you're that perfect, ni mtu ambaye unazo weaknesses zako chungu mzima pengine hata kulinganisha na za marehemu.
    Ninachoweza kukushauri wewe Taji you better stop that nonsense immediately, stop being hypocrite and stereotype.........wewe ni mburula tu huna lolote. Muache marehemu apumzike kwa amani. Na uwe unafikiri kabla ya kuandika chochote!! Stupid Idiot!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kula zote mdau, Taji is a hypocrite. Where the f***k were you when your opinion mattered to dj Rankeem? Unataka kuonekana kama ulikuwa unamjua saaaana sio? Super stupid egomaniac idiot!!!

      Delete
  4. Nyie wote mliomtetea taji kw hili ni wajnga

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad