-TAMKO rasmi la Ndugu Zitto Z. KABWE (MB) kuhusiana na kinachoitwa "Taarifa ya Siri ya Chadema"
Ndugu Wanahabari,
NILIPOKUWA katika ziara ya bara la Ulaya kati ya Oktoba 21 mpaka Novemba 2 mwaka huu (2013), nilipokea kwa njia ya barua pepe ripoti inayoitwa "Taarifa ya Siri ya Chadema" ambayo pia ilikuwa imesambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
“Taarifa ya Chadema inasema kwamba chama hicho (chama changu) kilikuwa kimechunguza mwenendo wangu tangu mwaka 2008 hadi 2010 na kubaini kuwa mimi napokea fedha kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuivuruga Chadema.
Ripoti hiyo ilinihusisha pia na mwananchi raia wa Ujerumani, Andrea Cordes ambaye, kwa mujibu wa ripoti hiyo, alinisaidia kupokea na kuhifadhi kiasi cha dola 250,000 za Marekani kupitia kwenye akaunti yake binafsi.
Taarifa hii ya kutunga na iliyojaa uongo wa kiwango cha kutisha, imenifadhaisha, kunisikitisha na kunikasirisha.
Taarifa hii iliibuliwa katika kipindi ambacho nilikuwa safarini kutetea haki za Watanzania na Waafrika ambao utajiri wao wa rasilimali unafaidiwa na watu wachache waliohifadhi mali katika nje za nje na pia kupigania makampuni ya mataifa tajiri yalipe kodi stahiki katika nchi zetu.
Pengine lengo la ripoti hiyo lilikuwa ni kutaka kunipoteza kutoka katika nia na dhamira yangu ya dhati ya kutaka Watanzania wafaidike na utajiri wao. Muda ambao watunzi wa ripoti hiyo waliamua kutoa taarifa yao unazua maswali mengi kuliko majibu.
Nafahamu kwamba mimi ni mwanasiasa ambaye nimekuwa mlengwa (target) wa mashambulizi kutoka kwa makundi mbalimbali ya wanasiasa na vikundi vyao. Kama mwanasiasa, niko tayari kupokea changamoto zozote zinazokuja na uanasiasa wangu.
Hata hivyo, ambacho sitakubali ni kwa watu kutumia jina langu na uanasiasa wangu kunichafua mimi binafsi na watu wengine wasiohusika kwa sababu ya kutaka kutimiza malengo yao ya kidhalimu.
Raia huyo wa Kijerumani tayari amekana kuhifadhi fedha zangu. Kwa maelezo yake kwa baadhi ya viongozi wa Chadema amekana kuwa na akaunti inayotajwa na amekana pia kuwepo nchini Ujerumani katika siku na wakati uliotajwa kwenye ripoti hiyo.
Ripoti hiyo imemtaja pia mtu kama Dk. Charles Kimei, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB ikidai kwamba nilikutana naye na alishiriki kwenye igizo hilo la kunipa fedha.
Niseme mapema kwamba tangu kuzaliwa kwangu sijawahi hata mara moja kukutana na Dk. Kimei popote pale ndani au nje ya nchi. Kumuingiza mtu ambaye amejenga jina lake kwenye taaluma ya kibenki kwa sababu tu ya lengo ovu la kumchafua Zitto Zuberi Kabwe si uungwana bali ni unyama.
Kutokana na uchafuzi huu wa wazi dhidi ya taswira yangu binafsi na watu wengine walioingizwa kwenye mkumbo huu, nimeandika rasmi kwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Wilbrod Slaa kumwomba athibitishe kwamba kinachoitwa Taarifa ya Siri ya Chadema ni kweli ni taarifa ya chama au kiikanushe ili niweze kuchukua hatua za kisheria dhidi ya waandishi wa hekaya hiyo.
Cha ajabu, nimepokea ujumbe wa kutishiwa maisha kutoka kwa mtu anayejiita Theo Mutahaba na kuahidiwa KUPOTEZWA endapo nitaendelea na jitihada zangu za kupambana na ufisadi na kutafuta haki kwa Watanzania wote pasipo kujali tofauti zao za kiitikadi, kikanda, kikabila na kidini.
Natarajia kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wote ambao wamehusika na utungaji na uenezi wa taarifa hii. Nitahakikisha kwamba wahusika wanatafutwa na kufunguliwa mashitaka stahiki ya upotoshaji na kuchafuana.
Ni matarajio yangu kwamba wale wenye mapenzi mema na Tanzania, mimi binafsi na utawala wa sheria, wataelewa nia yangu ya kutafuta haki katika suala hili.
Nimeamua kujitolea maisha yangu kwa ajili ya Watanzania na kama alivyopata kusema Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela; “Struggle Is My Life.”
Forward Ever, Backward Never- Kwame Nkrumah
Zitto Kabwe (Mb)
10/11/2013
Pole sana ndugu.ucrudi nyuma hao maadui zako kisiasa MUNGU atawalani na wataumbuka.wezi mafasadi nchi hii wamejaa Na nyny chdma tuliwaamini kumbe hamna lolote
ReplyDeleteBilabila,kukanusha taarifa unatakiwa kudisprove kila ishu,cjaona unadeny mawasiliano ya cm,kurushia wajumbe pesa kwa kutumia cm. This is passive admission to certain hard facts,its tym, zitto should go.
ReplyDeleteatadisprove nini ka hajatumiwa iyo pesa subiri matamko afu tujue ni nini
DeleteWewe anonymous wa 7:11AM you're so stupid. Kudisprove ndio lugha gani. I am not sure if that word exist in the world. Halafu kwa ujinga wako you pointed out eti hard facts. Ni hard facts gani ambazo unazo wewe. You can go to hell with your fuckin ignorance usituletee maupuuzi yako hapa. Hayo maupuuzi yako mpelekee mke wako kitandani. Wewe una combination of both illiteracy and ignorance. Mburula mkubwa weeeee......
Deletecc tupo nyuma yko tunakuunga mkono
ReplyDeleteWewe anonymous wa 9:42 lazima ni utakuwa ni mke wa Kabwe!
DeleteKwa nini viongozi wakuu wa CHADEMA wanakaa kimya muda wote huu bila ya kukiri wala kukanusha taarifa potofu dhidi ya kiongozi mwenzao????????.......Pole sana Zito Kabwe. Nakutakia kila la heri katika safari yako ngumu ya uana siasa.
ReplyDeleteZito naye ni sehemu ya viongozi wakuu wa chadema. Asiwe kiongozi anayekimbia responsibility na kutafuta wa kulaumu; jambo hilo limetokea katika eneo ambalo anawajibika nalo, yeye akiwa naibu katibu mkuu ni mtu wa pili kwenye ofisi ya utendaji inayoongozwa na katibu mkuu.
DeleteZitto we ni bravo,pambana allah yu nawe wote tu wapita njia hapa dunia, kwao dunia ni janah(pepo) lakini wakumbuke kuna maisha baada ya kifo.
ReplyDeleteUsiogope ZITTO,hao mafsadi wasikutishe,kama mungu kakuinua wanadamu hawatakushusha,pambana mbele kwa mbele ,ss twakuombea.ABARIKIWE ATAKAYEKUBARIKI NA ALAANIWE ATAKAYE KULAANI.
ReplyDeletemh! sasa ata mimi nashangaa,haiwezekan ccm wampe mtu maela kibao eti kwa kumpunguza kas,kwani yeye zito ni nani hasa ktk bunge,mbona wapo wengne kina Tundu vip na wao wamepewa mihela ama kutangaziwa dau au wanaogopwa,huu ni ujinga wa siasa za kibongo
ReplyDeleteI support you Kamrela Mtekateka. Halafu hao viongozi wa CHADEMA badala ya ku fight for na ku deny hizo allegations against Zitto Kabwe wanakaa kimya. Even if nothing has happened. Kwa kweli they're so insecure and fear of Zitto Kabwe. Wanaleta uchagga wao hapa. No way we gonna vote for them.period.
DeleteJamani kweni zito ni nani ktk nchi hii au hata CDM tu? mbona mnakuza saaana issue zake? siasa ni kupakaziana ili ushinde kura hilo lipo ccm, nccr, tpl nk. Mbona Zitto anapenda kulia lia wajemeni na anaijua fika siasa ya maji taka, iliwakumba kila Mwakyembe, Rostam, Lowasa, nn zito bana? uso mbuzi koko apambane tu na yeye amwage mboga badala ya kutafuta huruma kwa watu , mi sipendi wanaume wa kulia lia kaa hujahongwa funga domo lako zitto au acha siasa , vijana wapo wengi tu.
DeleteZitto naye anachemsha kiajabu, labda ni kwa sababu ya kutafuta political popularity. Kwa vile yeye ni naibu katibu mkuu wa chama chao na jambo hilo limetokea huko huko kwenye chama chake, ambacho yeye ni sehemu ya uongozi wake, ilitakiwa alishughulikie jambo hilo huko kwenye chama chake kabla hajaweka matangazo ya umma kama haya. Hii ni mara ya pilia kuonyesha kuwa amemuandikia barua katibu wake mkuu badala ya kusema amejadiliana na katibu wake mkuu. Kiongozi huyu inaelekea anajua sana propaganda lakini nina wasiwasi na uwezo wake wa kuendesha organization. Watu wa namna hii ndio wale ambao wanapokuwa na madaraka bado watakuwa wanalalamika kuhusu watendaji wao badala ya wao wenyewe kuchukua hatua.
ReplyDeleteWewe umeenda shule sanaaaa, nimependa uchambuzi wako sana , i do share yo view ila sikujua niandikeje.
DeleteKwa anonymous 10:51 AM......Sijui ni nini ambacho unakiona hapo. Zitto Kabwe hana sababu ya kutafuta political popularity kwa sasa. Kulingana na misimamo yake kuhusu mistakabali mbalimbali ya nchi ya Tanzania na kwa namna anavyoisimamia hiyo pekee inamfanya awe popular and the most extra ordinary politician of this decade, at least in Tanzania. You have pointed out kuhusu mawasiliano yake na Katibu Mkuu Wake, lakini mimi ninacho staajabu ni jinsi gani hiyo flow of communication within the leaders itakuwa that effective wakati the same leaders wanayo hiyo NEGATIVE notion against him na ni kwa sababu ya uroho wao wa madaraka pamoja na ukabila. And therefore wanaishia ku target yeye with all this nonsense allegations. Sasa what do you expect him to do kwa aina ya uongozi unaoshindwa ku support na ku back up yeye kwa mambo anayoyasimamia?????......No way hata ningekuwa ni mimi ningemwandikia barua huyo Katibu Mkuu ili awajibike based on the party constitution na role yake pia......By the way huyo Katibu Mkuu anafaa ku resign kwani kazi imemshinda, anaachia Chama kina ingia kwenye crisis kubwa bila hata ku respond. Nadhani pia uzee unamsumbua. Na sidhani kama ni kweli ni mwana siasa muwajibikaji of course by comparison to Zitto Kabwe. Na zaidi ni ku entertain ukabila which is typically inappropriate. Hiyo sio Kenya wala Uganda au Rwanda.
DeleteZaidi tunayoyaelewa kuhusiana na viongozi wahuni wa CHADEMA ni huyo Katibu Mkuu kuacha role yake ya upadri na kwenda kuiba mke wa mtu na kumuoa. I hope hilo kila mtu analielewa. Na pia mheshimiwa Lema anawajibika na kumbaka mwanamke anayeitwa Flora Lyimo wa UK. Halafu unategemea hawa aina ya viongozi wasiokuwa na leadership morals wala ethics wasichakachue katiba ya chama kwa maslahi yao??????
DeleteKuna watu haongei mantiki hapa. Bila kutafuta kuchafuliana majina kwa mbali, tuangalie jambo la msingi ambalo ni kuwa ni kuwa Zito ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, yaani ndiye mtendaji wa pili kutoka Katibu Mkuu, Inakuwaje sasa yeye acheze kama vile ni mtu wa pembeni, ina maana ama hajui kutumia madaraka yake au ni mlalamishi kwa vile anajua kuwa tayari ni popular basi lolote atakolofanya atapata sympathizers na hivyo kuchukiwa kwa baadhi ya viongozi wenzake.. Mimi ningependa tuangalie CHADEMA kama organizatsion ambamo Zito naye ni sehemu ya uongozi. Kukimbilia kusema fulani ni popular au fulani aliiba mke wa mtu ni upuuzi usiohusika hapa. Katibu mkuu wa Chadema naye ni popular, na Zito naye aliwahi kuhukumiwa kutemeba na mke wa mtu marehemu Chifupa, Kwa hiyo hakuna mtu clean kati yao ila tuangalie tu jinsi wanvyotekeleza majukumu yao katika chama chao. Anaposhindwa kukabiliana na uzembe mdogo namna hiyo ndani ya chama anachoongoza ni wazi hataweza kukabiliana na uzembe mzito uliko ndani ya serikali iwapo atapewa madaraka serikalini.
DeleteKwa Anonymous 2:53PM......Unaposema kuchafuliana majina una maana gani?? Kwani ni uongo ya kuwa huyo Katibu Mkuu hakuwa padre??? Kwani ni uongo ya kuwa hakuiba mke wa mtu mpaka mjamaa akafikia hatua ya kwenda kufungua kesi kwenye court kudai mke wake??? Je kwani ni uongo ya kuwa LEMA hana kesi ya kujibu huko UK kwa allegations za kumbaka mwanamke wa KiTanzania aitwae Flora Lyimo.........Na kwa taarifa yako hatuko sana nje ya hiyo unayoiita mantiki, kwa sababu mienendo na matendo yao katika jamii inanipa walakini na uwezo wao kiutendaji kama viongozi wa Chama Cha Upinzani.Zitto Kabwe hachezi kama mtu wa pembeni. Ni kwamba anachokosa ni support na back up kutoka kwa huyo Katibu Mkuu wa CHADEMA ambaye hana ethics za uongozi, sasa sijui unategemea nini.Na si kweli eti Zitto Kabwe anatafuta sympathizers bali anachofanya ni kuwa ana deny hizo allegations kwa kuweka facts hapo nje ili wanachama na wananchi kwa ujumla wachague kati ya pumba na mchele.Na basically anafanya hivyo kwa sababu he does not get enough cooperation from other leaders to tackle the crisis. And what we see from other leaders within the party is that they are attacking him as an individual instead of attacking the issues. Sasa wewe kwa akili yako hulioni hilo.Na ninasikitika unaposhindwa rationalize the whole crisis ambayo imegubikwa na Tamaa ya Uongozi, Matumizi Mabaya Ya Fedha Za Ruzuku Ya Chama na Ukabila. Na katika maelezo yako unashindwa kutueleza wasomaji ni jinsi gani Zitto Kabwe anashindwa kukabiliana na huo uzembe unaouita mdogo. Tatizo lililopo hapa ni kuwa Zitto Kabwe amezungukwa na viongozi ambao ni wahuni wasiojuwa dhamana yao na uwajibikaji.
DeleteWewe wa 5:17 acha kengele zisizokuwa na maana ukaanza kusakama mtu binafsi. Iwapo unajali hilo la kutembea na wake za watu kwa nini usimuulize na Zito ambaye pia aliingilia ndoa ya Mpakanjia mpaka akaisambaratisha na kusababisha afya za wanandoa hao kuharibika kutokana na msongo wa mawazo hadi wakafikwa na mauti. Usijifanye kupiga kele za kutaka kuleta mgogoro kwa njjia ya kuchafuliana majina kama vile upande wako ni msafi.
DeleteSwali la muhimu hapa ni hilo kuwa Zito kwa nini apige kelele kama mtu wa nje ya chama hicho ilihali yeye mwenywe ni sehemu ya Uongozi? Hiyo tabia ya kupiga kelele ili kusikilizwa na watu wa mbali ndiyo inayonitia shaka na uwezo wa jamaa huyu kiuongozi. Uongozi wa kusikilizwa na kushabikiwa siyo uongozi kabisa huo, Ile busara ya kujua maana ya madaraka yake ni jambo kubwa kuliko umaarufu. Kwa sasa hivi anaonyesha kuwa hajui kabisa maana ya madaraka yake. Ni afadhali Mnyika anajua sana maana ya madaraka yake kuliko huyu Zito.
Inashangaza sana et anachukua mihera kwa kuuza cri za chama??? Mi cjaona logic ya kupewa mapesa yote hayo!!! Kwa sir gan zilizo ndan ya chadema zenye thaman ya mapesa yote hayo mpaka ccm watoe mihela yote hyo kuzinunua...eti anawatumia kina tindu lisu na wenza sh lak 150,000-200,000 hv ni kwel hawa jamaa wanaweza kufanya uas kw hela hii mbuz??? Mbona inakua vigumu kuelewa by the way kama ni kwel mlikua mnamfuatilia zto toka 2008 so iweje mkae nae miaka yote hyo hal ya kua mnajua ana2as toka kpnd hicho hadi leo hii..kama ni kwel mlitambua hlo altakiwa achukuliwe hatua muda mrefu xana.. Huu ni unafk ucokubalka ila mcdhan kama mnajenga chama bali mnakibomoa.
ReplyDeletemtuache na chama chetu CHAGA DEMOCRATIC MOVEMENT ASSOCIATION (CHADEMA)
ReplyDeleteCHAGA DEMOCRATIC MOVEMENT ASSOCIATION (CHADEMA HAHAHAHAHAHAHAHAHAAAHAHAHAAHAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA UMETISSHER
ReplyDeletezitto kabwe ana akili sana na anatumia psychologia yake kubwa against ndogo ya watz ku manupulate akili zenu..zitto anataka kuwa rais wa tz one day so atafanya meng kuachieve his dreams..tujiulize ilikuwaje kwenye madini b4 ajapewa uongozi huko akakaa kimya?!
ReplyDeletezitto kabwe ana akili sana na anatumia psychologia yake kubwa against ndogo ya watz ku manupulate akili zenu..zitto anataka kuwa rais wa tz one day so atafanya meng kuachieve his dreams..tujiulize ilikuwaje kwenye madini b4 ajapewa uongozi huko akakaa kimya?!
ReplyDeleteZitto yo'll never stop pop ups and checks behind you..be smart otherwise they'l fix ur butt
ReplyDeleteZito yuda ww ni msaliti hana sela huyo fala tu
ReplyDeleteNavunjika moyo kbxa..ulafi na kuogopana ndo ndo knachotusambaratisha....halafu nanusa harufu mbya ya UDINI hapa...km ztto anmeanza kfatiliwa tangu 2008 na walgundua kua n mchfu mbona hawakmshughulikia kabla ya uchaguz 2010...km chama tuspojtambua vibaraka WATATUVURUGA na 2015 ndo hiyoooooo....
ReplyDelete9:37 kwa kweli, if you have a quety mind, zitto ni msaliti, na miendendo yote iliyotajwa ni ya kweli,kwani rostam aziz alivyompa hela mill m4 si ndio kipindi alinunua HUMMER na hua anaitumia mara chache sana, taarifa hiyo ni ya ukweli. amejibu hadith tuu, na hawezi kuwa makini tena zitto. anasaliti watanzania kwani chadema si wao ni watanzania waote. it pain tulishaanza kukupa imani kumbe ni tawi la chuma chako mapema,? usitumie madhaifu ya watanzania Zito, CCM imeshakushika vizuri na hilo doa walilokupatia halitakutoka mpaka unafifia.
ReplyDeleteMhh! Huu ni mwisho mwingine wa chama cha siasa sasa ni zamu ya NCCR Mageuzi kuwa tena juu hii single Chadema imechuja ngoja tuingize ingizo jipya
ReplyDelete