TETESI:ZITTO AMBURUZA HENERY KILEWO POLISI KWA KUSAMBAZA WARAKA ONLINE


WAKATI Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikimwandikia Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe barua ya kumtaka ajieleze dhidi ya tuhuma zinazomkabili, yeye ameamua kukimbilia polisi akimshitaki mmoja wa viongozi wenzake.

Habari za kuaminika zimedai kuwa Zitto ambaye hivi karibuni alivuliwa cheo chake cha unaibu katibu mkuu wa CHADEMA, inadaiwa amefungua mashitaka polisi akimtuhumu Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kileo kwa madai ya kusambaza waraka katika mitandao ya kijamii.

Akithibitisha tukio hilo, wakili wa Kileo, Peter Kibatara, alisema kuwa mteja wake amemriwa kufika makao makuu ya Jeshi la Polisi leo Jumatano saa nane mchana na kuonana na mmoja wa maofisa wa juu wa jeshi hilo, aliyetajwa kwa jina moja tu la Mbutta, kufuatia mashitaka yaliyofunguliwa na Zitto dhidi yake.

Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu, Kileo alikiri kuitwa polisi, ingawa alidai hajui ni waraka gani anaotuhumiwa kuusambaza unaomchafua Zitto.

“Kwa kweli sijui hata mimi ni waraka gani, ingawa hivi karibuni kulikuwa na waraka wa siri uliodaiwa kutoka CHADEMA, na ambao ulijaa tuhuma za usaliti. Lakini huo tuliishaukana siku nyingi. Labda kuna mwingine,” alisema Kileo.

Zitto kutwa nzima ya jana hakuweza kupatikana kwa njia ya simu kufafanua mashitaka aliyofungua polisi. Simu zake zote za kiganjani zilikuwa zimezimwa.

-Tanzania daima.
Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Simu zipo na mama?.

    ReplyDelete
  2. safi sana zito wewe ni mnyamaaaa kutoka unyamaniiiiiiiiiiii

    ReplyDelete
  3. kileo ni mwamba wa kaskazini,chaga de mangi(chadema

    ReplyDelete
    Replies
    1. ila huyu kileo huyu mwache tu hajakoma alivyosweka lupango sasa kitakachompata hiki kinachokuja atasimulia kwa mkewe Joyce Kiria..sasa hivi si anamficha yaani toka ajue ana ukaribu na Mbowe tu basi anaona keshafika Chadema bado tunakuvutia siku tu..

      Delete
  4. zitto jikaze usikiache chadema kwani ukiondoka chadema watajua nikweli ulikua unakihujumu chama kisha ukimbie

    ReplyDelete
  5. halafu jamaa si yuko uingereza au

    ReplyDelete
  6. Chaga de kilimanjaro chama cha maigwena.wabinafsi,zito zuberi kabwe ndo star wa hicho chama.sijui we zito ulikosa chama cha kujiunga mpk ukaenda kujiunga na watu wenye tamaa!kusema kwako ukweli basi ndio sababu ya wewe kuvuliwa uongozi unatakiwa ukiwa cdm unyamaze ulisau sheria za wafalme haurusiwi kuhoji chochote?maigwena uwagusa pabaya ulivyowaambia wakaguliwe.mfano Lema Ahadi zake hamna hata moja aliotekeleza matokeo yake hata zile fedha za mfuko wa jimbo zimegeka zake pia viwanja vya umma anaandika jina lake mfano ni kiwanja cha burka cha machinga complex.hawa wamekuja kutukomboa au wamekuja kutafuta maisha?kwa maono yangu chadema hakifai coz ni chama cha familia fulani na chama cha wananchi wote.watanzani wenzangu tunatakiwa kuwa waangalifu na watu kama hawa from no where tunawaamini.hawa ni madikteta wenye uchu wa madaraka.igweeeena de kilimajaro chaga style.zito hana kosaaaaaa amaeoneeeewa kwa kusema ukweeeeeli

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad