================
UPDATES
- M/Kiti Mh. Freeman Mbowe ameshawasili na ameanza kwa kusema kuwa Kamati Kuu imemteua Mh. Tundu Lissu kuwa Mwanasheria Mkuu wa Chama na pia Kamati Kuu imefikia maamuzi ya kinidhamu kwa baadhi ya viongozi.
Anamkaribisha Mh. Tundu Lissu kwa ajili ya kutoa taarifa ya maazimio ya Kamati Kuu kwa niaba ya M/Kiti
- Tundu Lissu anaanza kwa kusema kuwa Kamati Kuu imenasa waraka wa mkakati wa siri wa kukipasua Chama vipande vipande unaohusisha watu wanne ambao ni Zitto Kabwe, Dr. Kitila Mkumbo, Samson Mwigamba na mtu mwingine ambaye hajajulikana.
- Anasema lugha iliyotumika katika waraka huo ni ya siri ambapo kuna mtu anaitwa MM ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe, M1 ni Dr. Kitila Mkumbo, M2. Hajajulikana na Dr. Mkumbo alikana kumfahamu kabisa M2, na M3 ni Mwigamba.
Lissu anasema Waraka huo uliojulikana kama Waraka wa Ushindi unavunja katiba ya Chama kwa sababu umepandikiza chuki za kidini, majungu na kukashifu viongozi wa Chama kinyume na katiba ya CHADEMA.
Lissu anasema tuhuma zote zilizoko katika waraka huo hazijawahi kuwasilishwa kwenye kikao chochote halali cha chama kinyume na matakwa na masharti ya katiba yetu
- Anasema Kamati Kuu imeamua kuwavua nyadhifa zao zote watu wote waliotajwa katika waraka huo ambao ni Zitto Kabwe, Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba.
Pia kamati kuu imeunda kamati ya kuchunguza na kufuatilia mhusika mwingine M2 ambaye anadaiwa ni Mtumishi wa Makao Makuu ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yake
Kamati Kuu imeagiza wahusika wote waandikiwe barua za kujieleza ni kwanini wasivuliwe uanachama kwa makosa hayo makubwa waliyofanya.
- Pia Kamati Kuu imeagiza mchakato wa kumvua Zitto nafasi yake ya Unaibu wa Kambi ya Upinzani Bungeni.
- Lissu anasema Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe na Dr. Kitila Mkumbo waliomba kujiuzulu nyadhifa zao zote baada ya waraka wao kukamatwa lakini Kamati Kuu iliwakatilia baada ya kuona kuwa kukubaliana na maombi yao hayo ilikuwa ni kama kuwaacha wajiuzulu kwa heshima ambayo hawaistahili hata kidogo.
- Kamati Kuu pia imeazimia kuusambaza waraka huo kwenye vyombo mbalimbali vya habari ili watanzania waone na kujua ukweli.
Lissu anamalizia kwa kuwaomba watanzania na Wanachama wote wa CHADEMA nchi nzima wasife moyo na waendelee kukijenga Chama na nchi yao.
- Kamati Kuu pia imemteua Wakili Msomi Mh. Peter Kibatara kuwa Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa Chama
- Mh. Mbowe anasema waraka wa siri za Zitto haukutengenezwa wala haukutoka Makao Makuu. Alikuwa akijibu swali la Mayage kuhusu zitakapopatikana fedha za kutekeleza mpango huo
Jamii Forums
HONGERA SANA CHADEMA KWA UAMUZI MGUMU,HUKU KIGOMA KASKAZN ZITTO WALISHAMCHOKA SAIZ ANAELEKEA KUPOTEA KWENYE SIASA.
ReplyDeleteUkabila na udini umetawala ndani ya cdm. Mtamjutia zito kwa sababu hamjui ndio kawafikisha hapo mlipo.
ReplyDeletecdm sio kama wale wew. kumbuka hii ni nguvu ya umma
DeleteSio kweli ,chadema ndio imemfikisha zito hapo alipo.he was going vry well na age ilikuwa inamruhusu kukaa vzuri zaidi bdae.binafsi nampenda zito kwa ujasiri wake,bt kama haya ni ya kweli,dogo kachemka.so sad,nilikuwa naona kesho yako ndani ya chadema nw haka ni kadoa.hembu kaa na wakubwa wako wa chama mtengeneze hlo boma lililotoboka.smtimes mjifunze ku admit mnapokosea hta kama umaarufu umesha overflow.
ReplyDeleteNadhn kama mnadhn mwakihimarisha pole ZITTO THE MAN OF THE PEOPLE.
ReplyDeleteNilishasema awali kuwa Tanzania hakuna upinzani ni ubabaishaji tu,wako wapi hawa walijitutumuaaa,mwisho wanaumbuana na kufukuzana wenyewe acheni ccm ishike dola maana ndio wenye nguvu hizo,co kwa namna hii mwaka 2015 ni mtereko kwa ccm poleni xsana jamani,huo si ukomavu wa siasa ni ulegevu wa siasa,watu wanafanya chama ni cha makabila fulani
ReplyDeleteHamna lolote hicho chama kimejaa udini hiyo ipo wazi,dini flan flan ndo viongoz na undugu,wale wale 2 na chama tawala
ReplyDeletetunaitaji chama chenye uwezo wa kufanya maamuzi magumu hata kujidhuru chenyewe ili kusimamia haki na weredi. maamuzi haya yasingeweza kufanywa na chama chochote tz hii hata na hao wanaojihita ni wakomavu wa siasa. Hii si mara ya kwanza kufanya maamuzi magumu ili kujenga chama na nchi kwa ujumla, kwa hakika mmenisibithishi mimi na watanzania kua mnaweza hasa kuongoza nchi. chadema hakika haitishiki na nguvu binafsi ya mtu ktk siasa sio kama baadhi ya vyama vingine vyenye kulea na kuogopa watu hata kama wanahujumu nchi. safi sana chadema we ndo mkombozi wa kweli wa mtanzania
ReplyDeleteChadema Ckuhz Wahun 2 Na Nyie Bwana.
ReplyDeletemmekwisha, mtoeni zito muone chama kitakavyokatikakatia vpande vipande vya vigaes shwain nyie
ReplyDeleteAMANI THUS ALL WE NEED TANZANIA.CHADEMA CCM NOTHING WATU KUJIJALI WENYEWE NA FAMILIA ZAO TU...
ReplyDeletei sorry
ReplyDelete