USHAURI KWA ZITTO: MAJUNGU UNAYOPIGWA YANATOKANA NA KUTOKUJENGA UHUSIANO BINAFSI NA WENZAKO

Tatizo la Zitto sio ukanda, udini, ukabila, usomi na siamini Waraka ambao wanasema Zitto anahusika kwasababu umeandikwa kitoto sana.

Tatizo kubwa la Zitto na Chadema ni uhusiano binafsi na watu anaofanya nao kazi. Ukweli ni kwamba kazi ni zaidi ya sera, sheria za kwenye vitabu.

Viongozi wengi ni watu wa kawaida na wana uhusiano wa karibu hata wa kifamilia tumeona Kikwete analala kwa magufuli kwasababu Magufuli amegundua uhusiano binafsi ni njia moja wapo ya kufanikiwa kwenye jambo lolote. Hivyo Zitto hayo majungu yanatokana na kutokuaminiana kwasababu hujachukua muda kuweka mahusiano ya karibu na watu unaofanya nao kazi na hili ni tatizo kila mahali hata kwenye biashara au kazi nyingine.

Je unajua familia za wenzako, unajua wameamkaje asubuhi, unajua matatizo waliyonayo kama wagonjwa nyumbani? haya yote ni muhimu kwa watu unaofanyakazi nao sehemu moja. Vitabu vipo, sera zipo na sheria zipo lakini kwenye Chama kama Chadema ambacho ndicho kinakuwa na viongozi wachache kutupiana maneno kwenye mtandao inaonyesha hakuna mahusiano binafsi ambayo mnaweza kuongea kwenye chai ya asubuhi na kumaliza.

Hakuna jambo duniani linalofanikiwa kwa sera pekee bali mahusiano ni muhimu sana. Vilevile ni lazima uelewe mahusiano ni kati ya mambo muhimu ambayo ni lazima ukubali kama ni upungufu wako na kulifanyia kazi kama alivyofanya magufuli.

Magufuli pia alikuwa anaogopwa na JK na wengine kwa misimamo lakini aligundua hilo na kujenga mahusiano.

Zitto unakipaji na huna sababu ya kuwaeleza watu hilo kwasabbau kipaji ni kutoka kwa mungu na hakuna anayeweza kukichukua hivyo focus on your weakness.

Huu ni ushauri wangu kujibizana nani yuko sawa na nani hayuko sawa haitakusaidia popote pale na kwenye chama chocote au biashara.
Kitakacho kusaidia ni mahusiano-relationship
Tags

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. huyu juha gani ambaye kanisumbua kusoma upuuzi usioeleweka? Kama hujui sababu za zitto kaa kimya usijifanye unajua kumbe hujui,

    ReplyDelete
  2. Usimfundishe zitto!zitto ni kiongozi ambaye anajuwa namna ya kuishi na watu hii ni siasa zitto anataka kumalizwa kisiasa na na viongozi wakuu wa chadema kina dkt mbowe wanaojifanya wana demokrasia kumbe majambazi mabaradhuki wakubwa?zitto kiboko yao!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. mhh wabongo wakikosolewa ni kama umetangaza vita na Alshababu, nisichoelewa mbona wenzetu viongozi wa majuu wanakosoana na kiongozi akiondoka kwenye chama haanzishi majanga ya kusema majungu, sijui wivu, anasema ukweli pale kweli kwenye tendo hili nilichemsha kwa sababu sikuliangalia kwa mtazamo wa undani zaidi na mkinipa chance nyingine nitarekebisha nimeshajua nilichokosea,haya ya kuwekeana vita kushinda majukwaani kujibu kwa nini wamekufukuza hizo nguvu si ungezielekeza kwenye kuchimba visima Kigoma angalau wananchi wananufaika maneno matupu hayaendeshi nchi

      Delete
  3. Mnamwona zitto mkamiliiifu! Msiwe na imani hizo na ni uzembe kumwona binadamu aliyezaliwa kama wewe yeye ndo kila kitu, mjuzi wa yote. Na ndio hao wanaompotosha na kumtoa ktk system ambayo ingemfanya zitto awe bonge la kiongozi badae. Mnamharibia kwa kumpa heko kwa kila jambo. Hongera CHADEMA kwa kumrekebisha zitto, naye alitambue hilo kulifanyia kazi ktk maisha yake.

    ReplyDelete
  4. Mnamwona zitto mkamiliiifu! Msiwe na imani hizo na ni uzembe kumwona binadamu aliyezaliwa kama wewe yeye ndo kila kitu, mjuzi wa yote. Na ndio hao wanaompotosha na kumtoa ktk system ambayo ingemfanya zitto awe bonge la kiongozi badae. Mnamharibia kwa kumpa heko kwa kila jambo. Hongera CHADEMA kwa kumrekebisha zitto, naye alitambue hilo kulifanyia kazi ktk maisha yake.

    ReplyDelete
  5. Ukweli ndo huo ulosema mtoa mada. Kama anatafuta umaarufu wa peke yake na siyo chama chake na yeye, basi awe mwanamziki ka diamond atatoka kivyake na siyo ktk siasa.

    ReplyDelete
  6. chadema kwisheney

    ReplyDelete
  7. Hongera CHADEMA kwa maamuzi magumu. Hakuna chama kinaweza kuchukua hatua kama hiyo. Na Zitto bila CHADEMA umaarufu kwishneyyy.

    ReplyDelete
  8. Sasa chadema tuwaeleje kama hamtaki mtu wa kuwachalenge mnataka mbowe awe madarakani daima

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad