WEMA AWAJIBU BONGO MUVI BAADA YA KUMSUSIA MSIBA WA BABA YAKE

HUKU akiwa na majonzi ya kuondokewa na baba yake mzazi, Balozi Isaac Abraham Sepetu aliyefariki dunia Jumapili iliyopita kwa ugonjwa wa kisukari, baadhi ya wasanii wanaounda Klabu ya Bongo Movie (muvi) Unity wanadaiwa kuchekelea kifo hicho na kumsusia msiba mwingizaji mwenzao, Wema Isaac Sepetu. 

Habari kutoka chanzo chetu makini zilidai kuwa hoja dhaifu iliyotumiwa na wahusika hao ni kwamba Wema huwa haendi kwenye misiba ya wenzake hivyo naye amzike baba yake mwenyewe.
MFANO; MSIBA WA SAJUKI

Ulitolewa mfano wa msiba wa aliyekuwa staa wa filamu za Kibongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki dunia Januari 2, mwaka huu ambapo Wema alidaiwa alishindwa kufika kwa sababu alikuwa studio akirekodi wimbo wake mpya ambao haujatoka hadi leo.

Wapo waliokwenda mbele zaidi na kudai kuwa hata ukifunua madaftari yao wanapopatwa na misiba huwezi kukuta jina la Wema akiwa amesaini wala kufika.

SHARO, KANUMBA “Kwa njia moja au nyingine, Wema bwana huwa hashiriki sana katika misiba ya wasanii wenzake, kuna mtu muhimu sana na ana sauti pale Bongo Movie amesema kuwa katika misiba iliyotokea ameshiriki misiba miwili tu, wa marehemu Sharo Milionea (Hussein Mkieti) na (Steven) Kanumba kwa sababu alikuwa mtu wake.

Wanadai mara nyingi amekuwa akijitenga na misiba ya wenzake na wala huwa hatoi hata pole kwa wafiwa kama wafanyavyo wengine wanaposhindwa kufika msibani kutokana na sababu mbalimbali hasa za kimajukumu au kuwa safarini,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
 
“Kuna habari za chinichini kuwa walikaa kikao na kukubaliana kutohudhuria msiba wa Wema. Ilitengenezwa meseji ikatumwa kwa memba wote.

Chanzo hicho kiliendelea kudai kuwa kiongozi wa kundi hilo (jina tunalihifadhi kwa sasa) ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa uhamasishaji watu wasiende msibani kwa kigezo cha Wema kutojumuika na watu wengine katika matatizo yao.

WEMA ANASEMAJE?

Akizungumzia ishu hiyo ya kususiwa msiba wa baba yake Wema alisema: “Nimesikitishwa na kitendo hicho. Nahisi siyo sahihi kwa kuwa nimekuwa nikihudhuria misiba ya watu mbalimbali.

“Hawakuwa sahihi kunifanyia hivyo katika kipindi hiki kigumu, hata hivyo, wangekuja kwanza tumzike baba ndiyo nijifunze ila kutokuja kwao hakujanipunguzia chochote.”
Kitendo hicho kilitafsiriwa kuwa ni kama kumuongezea machozi mara mbili kwani tayari alikuwa na chozi la kuondokewa na baba yake kipenzi na la pili likawa ni kususiwa msiba.

Baada ya habari hizo kujaa tele, wanahabari wetu walizungumza na baadhi ya mastaa wanaounda Bongo Muvi juu ya kumsusia msiba Wema ambapo kila mmoja alikuwa na utetezi wake;

Ray: Mh! Kweli Wema haendagi kwenye misiba ya watu hata mimi sikumuona kwa Sajuki ingawa sijui kama alionekana baadaye ila kwa sasa niko sehemu mbaya nitakupigia baadaye tuongee kwa kirefu.

Halima Yahya ‘Davina’: Sikwenda msibani kwa sababu na-shoot na nina mambo yangu ya kifamilia ila niliambiwa nisiende.

Steve Nyerere: Mi nilifiwa na mwanangu sikumuona Wema, tunaangalia kwenye kumbukumbu za wasanii wanaofariki dunia Wema hajawahi kuonekana. Mi’ naomba wasanii wapendane kikweli siyo kinafiki.

William Mtitu: Niko shooting wiki nzima ila kama Wema hakuonekana kwenye misiba ya watu hasa kwa Sajuki alikuwa anakosea sana. Pia alikosea kwa kuwakandia wasanii kwenye vyombo vya habari, kama walikosea angekaa nao akawaambia.

Kulwa Kikumba ‘Dude’: Nilikwenda msibani kutoa pole kwa sababu wale ni ndugu zangu lakini nilivyofiwa na mama yangu Wema hakuonekana wala hakunipa pole na huwa haonekani kwenye misiba ya wengine kama ilivyotokea kwa Sajuki ingawa mimi siwezi kulipa kisasi.
 
ZANZIBAR; DIAMOND NDANI
Kutoka visiwani Zanzibar alikozikwa baba Wema Jumatano iliyopita, ripota wetu alimshuhudia mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiungana na wasanii wengine waliokuwa bega kwa bega kumfariji mrembo huyo.

Habari za kina zilidai kwamba kwa kuwa Diamond hakufika kwenye msiba nyumbani kwa akina Wema, Sinza-Mori, Dar ilibidi aungane na mrembo huyo visiwani Zanzibar kwani naye amekuwa akimendewa na kashfa hiyo ya kuhudhuria misiba mikubwa na kupotezea ya watu wa kawaida.

Aidha, wasanii wengine walioamua kwenda msibani bila kujali onyo la kutokwenda ni pamoja na Yobnesh Yusuph ‘Batuli’, Elizerbeth Michael ‘Lulu’, Kajala Masanja, Mahsein Awadhi ‘Dokta Cheni’, Salumu Mchoma ‘Chiki’ na Jaqueline Wolper

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. admin n ajeee ndo ktk jungu kuu la j2 umekutana na hii khaaa unafulia bhana kurudia ktu kimoja wk nzma mwachen mzee wa watu apumzike salama khaaaaa

    ReplyDelete
  2. Hawana haya hao. Msiba wa sajuki usiwe kipimo. Mbona alihudhuria msiba wa sharo na kanumba;-:- ni wivu tu unawasumbua na dhiki.

    ReplyDelete
  3. Unafiki na majungu ndo mmekalia...mbwa nyie ndo maana hata sanaa yenu haikui pumbavu sana,mwenzenu babake kazikwa na watu wa maana,tutaona kwenu sasa,tatizo bongo movie hakuna mwenye elim hata mmoja ndo maana akili zenu znafanana,manina zenu,kwahiyo mlivoacha kwenda mmetengeneza movie mpya? Au mmeimprove kwenye sanaa? Maskini nyie..Hahaha wema anapesa hvy husda zenu hazmpi shida nyoko nyie,mavuzi yenu yamechongoka,sura zimewaparamaaa bila make up na mikope ya bandia hamtoki nje,wasenge kabisa mikundu yenu ipo vsogoni,mmenchefua sana,tena we ray ndo ckupendi km cku zangu....matuc yote ya duniani ya kwenu,chaka vuzi nyie.

    ReplyDelete
  4. Hata wasipoenda hata wangeenda kwani hajazikwa na ww admn huna mambo yakuandika hii imepita tafuta mpya

    ReplyDelete
  5. Mbwa nyie....mbna msiseme wema alichangia kias gan kwa sajuki wkt anaumwa? Wema mama ucjal na pole tena na tena achana na hao vinyago

    ReplyDelete
  6. Kweli shukrani ya punda ni mateke, kama na wastara hakwenda msibani kw sababu wema hakuja msibani kwa sajuki mungu atamlaan

    ReplyDelete
  7. Wema usijali kitu chochote hawajakupunguzia kitu chochote hao.. kwani kutokuja kwao hakujazuia baba yetu kipenzi Abraham kuzikwa..shughuli mbona imekwenda vyema tu na kama alistahili kuingia peponi kafika salama..hiyo haijalishi wala haizui kitu chcht tenda wema nenda zako na VISASI haviruhisiwi na havistahili katika biblia imekataza.
    pole mwaya Mungu ni mwema

    ReplyDelete
  8. ni wivu tu huo na upungufu wa akili kwani kama wema aliwakera walipaswa wamweleze mapema na ninaamini angeomba msamaha kwani Wema ni mstaarabu sana na ana akili timamu.

    ReplyDelete
  9. Hivi wema akihuzuria misiba yote iliyotajwa si itakuwa mwaka mzima yeye ni misiba tu Mimi naona Wana jones tu wivu hamna lolote

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad