Kupitia kipindi chake cha ‘In My Shoes’ cha jana, Wema Sepetu alieleza jinsi alivyojisikia baada ya baadhi ya waigizaji wenzie wa Bongo Movie kugoma kuhudhuria msiba wa baba yake, Balozi Isaac Abraham Sepetu, mwishoni mwa mwezi uliopita kwa madai kuwa yeye hakuwa akifanya hivyo kwenye misiba mingine.
“Imeshatokea, wameacha kuja kwenye msiba, ni wao,” alisema Wema. Sio Bongo movie nzima, ni baadhi tu ya watu ambao wanauelewa na upeo mdogo ambao waliamua kutokuja. Lakini niliona Bongo movie wengi, walikuwepo marafiki zangu wengi, akina Batulli, akina Esha, Wolper alikuja, Lulu, JB alikuja, Jokate alikuja, Adam Kuambiana alikuja. Ambaye napenda nimpe my special thanks and appreciation, ambaye alijitolea from the beginning wa msiba mpaka to the end ni Dokta Cheni kwakweli. Dr Cheni, I thank na ntazidi kumshukuru,” alisema.
“Marafiki zangu kama akina Kajala, akina Zamaradi, wale sio marafiki, wale tayari ni ndugu, kwahiyo siwezi kuwaweka kwenye appreciation wala kwenye thanks.”
Katika kipindi hicho pia, Wema alisema yeye na ndugu zake walijua kuwa baba yako ni muumini wa dhehebu la Roman Catholic siku chache kabla ya kufariki dunia.
Balozi Issac Abraham Sepetu (71), alizikwa kikristo katika kijiji cha Mbuzini,mkoa wa Kusini Unguja October 30 ambapo mazishi yake yalihudhuriwa pia na Rais wa Zanzibar,Dk Ali Mohammed Shein pamoja na viongozi wengine.
Bongo5.com
WEMA AWAJIBU WAIGIZAJI WA BONGO MOVIES WALIO SUSIA MSIBA WA BABA AKE
12
November 14, 2013
Tags
ACHANA NA MAMBURULA WEMA
ReplyDeletewell said mdau, mburura mwenyewe mmoja tu Steve Nyerere ona umeaibikaje kaka endekeza chuki binafsi uone itakufikisha wapi
DeleteHUYO RAY AKADEAL NA SWALA LA MAINDA NA JOHARI , KUSHADADIA KUSHAWISHI WATU WASUSIE MSIBA WA KIONGOZI WA SERIKALI NANI KAPOTEZA HAPO ?? MMEKOSA NAFASI YA KUKAA NA WAHESHIMIWA
ReplyDeletewema uko juu kama muashoki, watake wasitake , habari ndiyo hiyoo
ReplyDeleteyaan jina lako wema na uawema moyoni mwako loh mungu akubariki sana usijali ona ni changamoto mzee amelala sisi wakristo tun sema hivyo pia maisha yana songo mbele nakujua unamoyo mwema sahau usilipe baya wkipata mabaya wewe wape pole ple unapoweza ndio maana mungu ana zidi kuiwakisha nyota yako ipo juuuu .sana pole na msiba wa baba
ReplyDeletewatajicary tajir asusiw msiba ww maraisi walikuwepo mawaziri na viongoz kibao afu bongo movie akupe pressure wakafie mbele team wema for lyf
ReplyDeleteUcjali WEMA wacha na wao wapate msiba tuone kama kuna Rais ataenda. hao ovyo zao . ww uko juuu
ReplyDeleteUsijali mamy binadamu ndo walivyo wasamehebure
ReplyDeleteWorry out tuko pamoja team wema ndo mpango.we wetu c tupo nawe kwa maombi.una roho nzuri ulimsaidia my ndugu mmoja hata siyo star ila ulimpa support we una huruma hawakujui.wana roho za kwanini.mungu akupe zaidi.
ReplyDeleteucjar wema yote maisha nawao ikitokea ucende ten et cumepat wa kuzika bila ya kamat japo inaum wao kutokuja ciz mim nilijua nikija ntawaina master lakin nahis wamefat ushaur wako msanii utakiwi kuoneka ovyo-ovyo so wangekuja weng tungewahona
ReplyDeletePole sn Wema hao wanaojiita cjui Bongo Movies wamechemsha sn kuzika ni thawabu sasa wao wanalipiza kisasi kweli. Hata hivyo, kama huyo Ray yy alikuwa amegombana na Kanumba mbona alivyokufa alikuwa mstari wa mbele mara kwenye kamati ya mazishi mara kuuza tshirt za Kanumba alikuwa anajipendekeza tu. Laiti kama Kanumba angestuka ghafla mbona yeye Ray angeaibika. Hana lolote ni roho mbaya tu inayomsumbua na chuki. Mbona Marehemu Balozi Sepetu amezikwa na watu muhimu sana achana nao.
ReplyDeleteray kwa kanumba si alikua anauza suuura!hujastuka tuu! akadeal na case yake na mainda na johari! wake za wa2 ndo mpango wake! kiongozi hawez kuwa ray! god forbid! mnafiki huyo kakak! sura kama anaomba change! hata wakipata msiba hata balozi wa nyumbakumi hafiki itakua raisi! huyo steve nyerer ni uzee unamsumbua na amesahau kuwa wazee ni hazina
ReplyDelete