JACKLINE WOLPER 'FILAMU NILIYOTOA KUMUENZI STEVE KANUMBA ILINIPA HASARA YA MAMILIONI YA SHILINGI"

NYOTA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa filamu yake aliyoitoa kumuenzi marehemu Steven Kanumba iitwayo After Death ilimlostisha kwa kuwa ilimpatia hasara kubwa.

“Nilitengeneza ile filamu kwa hela nyingi kidogo, kama milioni 35 au 40, nikafanya na uzinduzi pale Leaders Club uliogharimu kama milioni 13 hivi, lakini nilipokwenda kwa Wahindi wakanipa shilingi milioni 25, yaani inakatisha sana tamaa,” alisema muigizaji huyo wakati alipofanya mahojiano maalum na waandishi wetu.

Alisema hasara aliyoipata na ambayo hata wasanii wenzake huipata inatokana na uwepo wa wasambazaji wachache wa kazi za wasanii, kitu kinachowafanya watu hao kujipangia bei bila kujali gharama ambazo wameingia katika utengenezaji wake. 

Chanzo: GPL

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tatizo kubwa ni kwamba mnawekeza pesa ndogo kwenye hizo filamu zenu,na matokeo yake ubora wa filamu unakuwa mdogo,ukilipwa pesa ndogo unalalamika,watu wanatumia miezi sita mpaka miaka miwili kutengeneza filamu moja,nyie mnatengeneza kwa mwezi mmoja je unategemea nini kitatoka hapo?,pia kwa swala la distributors wafanyabiashara wa tanzania wamezubaa hivi ni kwanini kila kitu wafanye kina patel?,inabidi watu wafunguke wawekeze kwenye fursa hii ya usambazaji wa filamu labda kdogo inaweza punguza malalamiko

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad