ZITTO AJIWEKA NJIA PANDA

Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe amejiweka katika mazingira magumu zaidi kisiasa ndani ya chama hicho, kutokana na shaka kubwa iliyougubika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Dar es Salaam juzi.

Zitto pamoja na viongozi wengine wawili wa Chadema; Dk Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba walivuliwa nyadhifa zao na Kamati Kuu ya Chadema baada ya kubainika kupanga mbinu za uasi, kupitia waraka ambao ulikuwa ukieleza mkakati wa kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani.

Leo, uongozi wa Chadema umeitisha mkutano wa waandishi wa habari ambao pamoja na mambo mengine, utajibu baadhi ya hoja za utetezi ambazo zilitolewa na Zitto pamoja na Dk Kitila. Katika mkutano wa juzi, Zitto na Dk Kitila ambaye alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, walizungumzia kuvuliwa kwao madaraka, lakini maandalizi na uendeshaji wa mkutano huo yanazua shaka kutokana kuwahusisha watu wanaodaiwa kuwa ni wanachama wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM).

Miongoni mwao, wamo waliowahi kuwa wanachama wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Habib Mchange na Mtela Mwampamba ambao walitimuliwa kwa makosa yanayofanana na yale yalizosababisha Zitto na wenzake kuvuliwa nyadhifa zao.

Mchange na Mwampamba pamoja na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Bavicha, Juliana Shonza, walivuliwa uanachama wa Baraza hilo Januari 5, mwaka huu baada ya kupatikana na hatia ya kutumia mitandao ya kijamii kukihujumu Chadema na kuwatukana viongozi wake wakuu. Baadaye walihamia CCM wanakoendeleza harakati zao za kisiasa.

Jana, Machange alipotafutwa, alisema: “Mimi sikuwahi kuondoka Chadema, nilifukuzwa kihuni kama walivyowafanyia Zitto na Kitila. Nimepeleka malalamiko yangu tangu Januari hadi leo sijajibiwa, hivyo siwezi kusema nimeondoka.

Nataka nimuunge mkono mwathirika mwenzangu kama ilivyokuwa mimi lakini nitabakia kuwa mwanachama mwaminifu.

“Mimi ni mwanaChadema na sikuwahi kujiunga na CCM au chama chochote, walioondoka ni Mwampamba na Shonza.” Mwampamba alisema: “Nilijitokeza pale kuonyesha mshikamano kwa sababu mimi pia ni mwathirika. Kwa hiyo nilitaka ulimwengu ufahamu kuwa mimi ni kati ya wanaopinga siasa za aina hii... Chadema ni chama kinachojiandaa kuchukua dola, sasa kama kila mwenye mawazo tofauti anaonekana mhaini itakuwaje siku wakichukua dola? Ubaguzi huu haujalishi uko chama gani, hata kama niko CCM, hilo halinizuii kuungana na mtu aliyepatwa na tatizo kama langu.”

Kuwepo kwao katika mkutano wa Zitto kunaweza kutumiwa na uongozi wa Chadema kuwa uthibitisho wa kiongozi huyo kushiriki katika uasi na kunaweza kupuunguzia nguvu utetezi unaotolewa na Dk Kitila kwamba hakuwa sehemu mpango wa kuuondoa uongozi wa sasa madarakani. Zitto, Dk Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba wanasubiri kukabidhiwa barua za kuvuliwa kwao madaraka na katika siku 14 wanapaswa wawe wamewasilisha utetezi wao wakieleza kwa nini wasifukuzwe uanachama kutokana na tuhuma zinazowakabili.

Dk Slaa

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa alisema jana kuwa ilikuwa lazima viongozi hao wavuliwe madaraka hasa baada ya Dk Kitila kukiri kuhusika na waraka ambao anasema ulilenga kushinda kupitia uchaguzi halali ndani ya chama hicho.

“Hata katika ya nchi ukihusika kutengeneza mbinu za siri lazima ushughulikiwe.Hakuna Katiba itakayokuruhusu kufanya mipango ya siri. Kwanza uchaguzi wa Chadema nani katangaza mpaka mipango ianzwe kutengenezwa sasa hivi?” alihoji Dk Slaa.
Alikiri kwamba watuhumiwa hao hawajapewa barua za uamuzi wa Kamati Kuu na alipoulizwa sababu, alisema Katiba ya chama hicho haitoi mwisho wa mtu kupewa barua, huku akihoji: “Wao nani kawaambia waende kwa waandishi wa habari?”

“Mimi ndiye Katibu Mkuu. Katiba inasema ni lini barua iandikwe? Utatokaje kwenye kikao alfajiri na wakati huohuo uandae barua za kuwapa?” alihoji Dk Slaa.

Mkutano leo

Mkutano wa waandishi wa habari ulioitishwa leo unatarajiwa kujibu  baadhi ya hoja za utetezi za viongozi hao zilizotolewa juzi. Zitto alifichua kile alichokiita tuhuma zilizotolewa dhidi yake mbele ya Kamati Kuu akimaanisha kwamba tuhuma zilizotamkwa kwenye vyombo vya habari na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hazikuwa kamilifu.

Habari zinasema uongozi wa Chadema utaweka wazi kile kinachodaiwa kuwa ni “Zitto kujitungia tuhuma, kisha kuzipatia majibu”, badala ya kujibu hoja ambazo zilitolewa na Kamati Kuu.

Jana, Dk Slaa akizungumzia suala hilo alisema Kamati Kuu haiwezi kuchaguliwa tuhuma za kusema na za kuacha... “Hiyo hoja walete kwenye vikao, nani anayeipangia Kamati Kuu ichukue hatua gani pale inapotaka kufanya hivyo?”

Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene akizungumza jana alisema: “Kamati Kuu ilijadili mambo mengi na hayo ndiyo tunataka umma ufahamu msimamo wetu kama chama.”

Habari ambazo zimelifikia gazeti hili zinasema katika mkutano huo, huenda uongozi wa Chadema ukaweka wazi “makosa mengine” ambayo Zitto anadaiwa kuwa amewahi kuyafanya na kuonywa katika vikao vya ndani ikiwa ni pamoja na kiongozi huyo kutofika makao makuu ya chama hicho kwa zaidi ya miezi sita. “Kuna makosa mengi (Zitto) ameyafanya yenye sura ya kukiumiza chama chetu na alionywa mara nyingi tu, tena na vikao vya juu vya chama kuhusu mwenendo wake, lakini aliendelea na uasi.Sasa Kamati Kuu imechoka,” alisema mmoja wa maofisa wa Chadema Makao Makuu.

Habari zaidi zinasema katika mkutano wake wa leo, chama hicho kitatoa ufafanuzi kuhusu mikutano yote ya kichama ambayo imekuwa ikifanywa na Zitto, huku kukiwa na hoja kwamba alikuwa akifanya hivyo bila kuwashirikisha maofisa wa makao makuu wala sekretarieti ambayo kimsingi ndiyo inapaswa kuiandaa.

Wasomi wanena

Akizungumzia mgogoro huo, mtaalamu wa mambo ya siasa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Richard Mbunda alisema hali inayoendelea ndani ya Chadema ni matokeo ya vyama vya siasa kutofanya kazi kama taasisi.

“Misingi ya vyama haiweki wazi misingi ya watu kuwa viongozi. Kwa mfano, kesho nikitaka kujiunga na Chadema nitaweza kuwa Mwenyekiti? Misingi ya wazi hakuna,” alisema Mbunda.


Alisema hali ilivyo ndani ya Chadema kwa sasa ni furaha ndani ya CCM, kwani watu wanaona kuwa chama kilichoonekana kuwa mbadala hakiwezi hata kushughulikia mambo yake ya ndani.

Mhadhiri Mwandamizi wa Sayansi ya Siasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Alexander Makulilo alisema vyama vya siasa ni watu au kikundi cha watu wenye malengo na mitazamo tofauti.

“Ukisoma huo waraka utaona kuwa unazungumzia uongozi, upungufu uliopo kwenye uongozi na namna ya kubadili uongozi, mimi binafsi niseme ieleweke kwamba hata kwenye jumuiya yoyote mambo haya yapo hasa kwa kuwa walikuwa wanaelekea kwenye uchaguzi,” alisema. Alisema haoni kwa nini Zitto na Dk Kitila waonekane wahaini kwa kupanga mikakati yao ambayo walitaka kuitekeleza kupitia uchaguzi.


“Mabadiliko ni jambo la kawaida, hali hii ya kuwaondoa kwenye nyadhifa zao inawezekana ikawagharimu Chadema na inaweza kuwagharimu zaidi wakiwafukuza uanachama,” alisema Makulilo.
Tags

Post a Comment

21 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. imeshawacost chadema watajibeba bila zitto hakuna chadema

    ReplyDelete
    Replies
    1. Msenge kweli wewe bila zitto hakuna CDM nani kakudanganya, zitto ni mtu wa Arudha au Moshi au Mbeya. Ndio nyie mnaoabudu watu ndio maana tz haopigi hatua, alikuwepo baba wa Taifa hapa akafa CCM hio bado ipo, so zitto hawezi kuwa kila kitu, hata kama ni bora kwa maoni yako ila bado anakasoro nyingi tu kama vile kujiona bora kuliko wengine na kujifanya anajua kila kitu. Wapumbavu kama wewe wanaoabudu mtu badala ya Mungu ndio tatizo zaidi kuliko hata Vurugu za CDM

      Delete
  2. Wewe Amon 11:29 sio bure utakuwa na mtimbiliko wa mavi kichwani au ndio sera za kutokubali ukweli.Angalia mfano wa uchaguzi wa 1995 pale Mrema alipojiunga na NCCR mageuzi. Na chama kilikuwaje baada ya Mrema kutoka.Kifo cha NCCR ndio kitakuwa kifo cha cdm wakimfukuza Zitto.na kama mbishi subiri tuone ukweli wa maneno yangu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sio kweli Chadema ilikuwa juu hata kabla ya zitto.afu huyu jamaa alishanunuliwa na chama tawala siku nyingi akiwa mwenyekiti tu nakwambia itakuwa CCM C maana CCM B ni CUF

      Delete
  3. wote nyinyi ni mbula pamoja na chadema yenu!!!

    ReplyDelete
  4. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  5. Ufisadi ubinafsi na kupenda madaraka ya juu kwa nguvu yote hayo ndio yamenchangiya chadema kumalizika

    ReplyDelete
  6. Ni kweli lazima taasisi yeyote iwe na watu ambao wanamawazo yanayokinzana. Na ili tasisi hiyo iweze kuendelea mawazo kinzani hayo lazima yawe siri. Sijaona kosa la Dr. Kitila kwani katika uchaguzi wowote lazima muwe na mipango ya siri ili kufanikisha ushindi. Na ukizangatia waraka ulikuwa ni wa watu watatu. Nikija hadharani na kupayuka kwamba mboye anaudhaifu kadhaa nahakika utakuwa ni uadui wa kudumu na ni matatizo makubwa. hivyo, kama waraka ulikuwa ni wa siri si tatizo mandhari ushindi ungepitia njia halali za uchaguzi. kanachotokea sasa kwa chadema kinadhihirisha udhaifu na uoga wa viongozi wakubwa wa chadema. Nimesoma waraka na naomba wote musome, upo sahihi kabisa na udhaifu wote ni kweli na tunahitaji kufanya mabadiliko kwa chama chetu. Naomba wote tusome warak

    ReplyDelete
  7. huwezi kuwa kiongoz mzur kama hutakubali kupingwa,mbowe lazima akubali kupingwa,hata ccm kataka kipind cha uchaguz wa ndan hua kunakua na mambo kama haya,watu hukashifiana na kutukanana matusi ya utani ikiwa njia mojawapo ya kutafuta ushindi,uchagzi ukipita alieshinda anaheshimika na maisha yanaendelea,sasacdm kama chama kinachohubir demokrasia hakitaruhusu upinzan ndan ya cha hakuna demokurasia hapo

    ReplyDelete
  8. Tatizo wanataka kuigeuza CDM iwe Kama taasisi ya kimila au kichifu. Sielewi kwanini mkwe Wa Mbowe Mzee Mtei aje juu kila anaposikia mtu anataka awe Mwenyekiti.

    Na huyu Slaa ndio anyamaze kimya kamtoa mhasibu kisha nafasi hiyo kampa mie mdogo, Sasa ruzuku itapona kweli hapo? Na hiki ni chama au NGO ya kifamilia?

    ReplyDelete
  9. chadema mkubali mkatae mmekwisha.

    ReplyDelete
  10. Wao walisema ni malaika hawakosei tuone sasa maneno yao,mwisho umefika wa uwongo wenu,tizama tu wanaoitetea chadema matusi imewakaa midomoni na hasira kama viongozi wao,mkipewa nchi hakika magereza zitajaa na kujengwa zingine kwa kuwa hamtataka kukosolewa,hivyo kila atakaejaribu kunyanyua mdomo jela,ingekuwa ccm inafanya mnayoyafanya chadema yote mngeishia jela,lakini ni watu wanaoelewa siasa na demokrasia ni nini,zito kutaka uwenyekiti ni kosa maajabu sana kwa chama inayojigamba kuwa ni chama kinachotetea demokrasia,wakati ndani ya chama hakuna demokrasia,watanzania wenye akili hawawezi kuunga mkono watu wa jinsi hii,kawapeni wavuta bangi viroba na sh 5000 mpigiwe madebe barabarani na siasa zenu za uchochezi,lakini kukamata dolla sahauni,nyie wote ni mabedui,hamuwezi kufanya ya ndani ya chama ya nchi mtafanyaje,bado kabisa mko nyuma kisiasa hichi ni chama cha EDWIN MTEI,NA FREEMAN MBOWE ci chama cha watanzania

    ReplyDelete
  11. Hilo ni dogo sana kwa chadema ya sasa. Ni kama kumpiga teke chura. Chadema wametengenezewa makesi kibao wameyapangua, na hadi kupigwa mabomu lakn chadema hiyo mnaiona. Litakuwa swala la zito bhana. Zitto alishajitoa cku nyingi chadema, na chaguzi zimefanyika na chadema wamenyanyua ndoo palipo kuwa na wabunge/madiwani wa ccm. Nyie kama vp itokee uchaguzi hata kesho mwone kitakachotokea. Endeleen kumwabudu zitto atawasaidia mnachotaka.

    ReplyDelete
  12. Hilo ni dogo sana kwa chadema ya sasa. Ni kama kumpiga teke chura. Chadema wametengenezewa makesi kibao wameyapangua, na hadi kupigwa mabomu lakn chadema hiyo mnaiona. Litakuwa swala la zito bhana. Zitto alishajitoa cku nyingi chadema, na chaguzi zimefanyika na chadema wamenyanyua ndoo palipo kuwa na wabunge/madiwani wa ccm. Nyie kama vp itokee uchaguzi hata kesho mwone kitakachotokea. Endeleen kumwabudu zitto atawasaidia mnachotaka.

    ReplyDelete
  13. Hilo ni dogo sana kwa chadema ya sasa. Ni kama kumpiga teke chura. Chadema wametengenezewa makesi kibao wameyapangua, na hadi kupigwa mabomu lakn chadema hiyo mnaiona. Litakuwa swala la zito bhana. Zitto alishajitoa cku nyingi chadema, na chaguzi zimefanyika na chadema wamenyanyua ndoo palipo kuwa na wabunge/madiwani wa ccm. Nyie kama vp itokee uchaguzi hata kesho mwone kitakachotokea. Endeleen kumwabudu zitto atawasaidia mnachotaka.

    ReplyDelete
  14. Chama cha wachaga,na ww ni mmoja wao

    ReplyDelete
  15. pumbavu chadema acheni malumbano njoon tuingie mitaan kupinga ongezeko la umeme ccm na mawaziri wake hawana akili wanataka turudie vibatari

    ReplyDelete
  16. WANA CHADEMA TUSIENDELEE KUBISHANA TUGEUKENI NYUMA ONENI ADUI WETU KWA WANANCHI: umeme umeme jamani wanataka kupandisha bei.

    ReplyDelete
  17. Chama cha maigwena wa kichaga zito ndo alikuwa star wenu bila zito chadema hamna.Mnajionyesha zahiri shahiri kwamba mna tamaa na uchu wa madaraka wala hamna huruma hata chembe ya kupambana kusaidia wanyonge.chadema kimekaa kikabila,kivurugu,kimaslahi binafsi!kibabe!kidkiteta!.acheni kuwadanganya wananchi chochote.mfano lema amehadi nini na ametekeleza nini?igwena Mbowe anaiua chama cha baba mkwe wake kwa kung'ang'ania madaraka!hichi chama sio cha watanzania kama vilivyo vyama vingine,hiki ni cha jamii ya wachaga hususan mtei.bado watu watafukuzwa tu hamna jinsi coz demokrasia hamna hapo.ukisema ukweli tu kosa.lema tunauliza mfuko wa jimbo uko wapi na kiwanja ulichopewa burka kwa ajili ya machinga complex umeandika jina lako!wapi ambulace?huna lolote wewe sio mwanasiasa umedandia fani kwa kukosa msosi.wananchi fungueni macho

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad