LILE GARI LA WOLPER AINA YA BMW X6 ALILOPEWA NA DALAS LAOZEA YADI DAR

LILE gari aina ya BMW X6 alilokuwa akitanulia mwigizaji Jacqueline Wolper linaendelea kuoza katika yadi ya Majembe, Mwenge jijini Dar kutokana na kudaiwa ushuru.

Taarifa ambazo Risasi Jumamosi limezipata kutoka katika vyanzo tofauti, zimeeleza kuwa hakuna uwezekano wa gari hilo kurudi katika mikono ya Wolper kwani aliingizwa mkenge tangu aliponunuliwa na aliyekuwa mpenzi wake, Abdallah Mtoro ‘Dallas’.

“Wolper aliingizwa mkenge tangu aliponunuliwa lile gari, lilikuwa linadaiwa ushuru sasa yeye bila kujua akaingizwa mkenge na pedeshee Ndama na kisha mtego wa kulinasa ukafanyika, Ndama huyohuyo akaja kumgeuka akawa anaeneza uvumi kuwa Wolper kaingizwa mkenge,” kilidai chanzo.

Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Wolper aliweka bayana kuwa gari lile alilonunuliwa kwa dola 130,000 (zaidi ya Sh. Mil. 170 ) kipindi penzi lake na Dallas lilipokuwa likichanua, mwaka jana polisi wa kimataifa (Interpol) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) walilikamata kwa kudaiwa ushuru.

“Sina ujanja tena kwani hata mimi nilikuwa sijaelewa kama linadaiwa lakini Ndama ndiye aliyejua mchongo mzima, akaniingiza chaka. Hadi sasa linaozea pale Majembe,  sina jinsi, namuachia Mungu,” alisema Wolper na kuongeza:
“Nilipolikabidhi Majembe na kuonesha documents (nyaraka) zote, niliambiwa nitalipata baada ya muda lakini mpaka leo sijaambiwa lolote. Linaozea pale.”
Chanzo:Global P

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Bado hujawa mtoto wa mujini Wolper, utaliwa kekundu kwa kuhongwa vitu fake mpaka ukome, documents za gari mpaka card zake zinapatikana mtaani tu so its up to u kujua ni za kweli ama la na ni lazima uende na file la gari yako TRA wakague page kwa page na ku compare na za kwao. Sasa vile nyie mnahongwa kwa mahaba ni ngumu kumtolea mimacho mpnz wako ili akupeleke tra ku prove , so unakuta gari kiuhalisia ipo kwa jina lake ila katengeneza document fake mpaka kadi ya gari kwa jina lako, unaliwa kekundu weee cku kakuchoka anafata gari yake kwa ufunguo wa pili au tatu aliobaki nao anachukua gari lake popote utakapopark, sasa nenda polisi ukadai umeibiwa kama hutageuziwa kibao na ukawa mwizi wewe.

    ReplyDelete
  2. nunueni kwa pesa zenu japo ni starlet kuliko kugawa mbunye/uroda kwa magari/vitu vya kifahari ambavyo mwisho wake ni majembe.

    ReplyDelete
  3. Madai ykae hakupitiwa na dallas huyu kwamba dallas alikuwa mfungon inakuaje mdau unasema kagawa uroda tena

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad