RAY "JOHARI NA MAINDA TUPA KULE CHUCHU HANS NDIO MKE WANGU"

Stori: Brighton Masalu
SINEMA ya madai mazito dhidi ya mastaa wa filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’, Ruth Suka ‘Mainda’ na Chuchu Hans ambaye ni mke wa mtangazaji Frank Mtao kuchanganywa kimapenzi na Vincent Kigosi ‘Ray’ sasa inaendelea na mhusika mkuu Ray amefunguka na kueleza yake ya moyoni huku akisisitiza: “Chuchu ndiye mke wangu, tarajieni makubwa soon (hivi karibuni).”

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, wikiendi iliyopita katika Viwanja vya TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam ambapo kulikuwa na mechi kati ya wasanii wa Bongo Fleva na Bongo Muvi, Ray aliwashangaa waandishi kwa kumshambulia kutoka kimapenzi na Chuchu.

Mwandishi wetu alianza kwa kumwuliza: “Ray magazeti yanaandika kuhusu wewe kutoka na Chuchu Hans ambaye ni mke wa mtu. Mainda amezungumza mengi. Kukaa kwako kimya bila kufafanua chochote siyo kitu kizuri. Tafadhali, hebu zungumza japo kidogo kuhusu madai ya Mainda.”

RAY: Sikia nikuambie, huyo Mainda utoto unamsumbua. Haniumizi kichwa kabisa. Kuhusu Chuchu... si mmeshaandika? Endeleeni kuandika lakini soon mtashuhudia kitu kikubwa sana.

RISASI: Ni kitu gani hicho? 
RAY: Niacheni na Chuchu wangu.... kifupi ndiye mke wangu na itawashangaza wengi. Halafu mimi nawashangaa sana. Yaani mimi kutoka na Chuchu mnakuzaaaa... mbona alivyokuwa na ma-boyfriend zake wengine hamkuandika? Kwa sababu ni Ray basi mkaona ni habari. Mimi ninavyojua Chuchu siyo mke wa mtu.

Kwanza mimi sijamchukua kutoka mikononi mwa mumewe kama mnavyosema. Chuchu tayari alikuwa na maisha yake mapya. Nilimchukua kutoka kwa Libert (hajafafanua zaidi ni nani). Mbona alivyokuwa na huyo Libert  hamkuandika? Kifupi niacheni na maisha yangu.

RISASI: Vipi kuhusu Johari?
RAY: (Huku akikimbia kuingia uwanjani) Tena huyo mama yako (akimuonesha mwandishi Johari) anakuja.
Mwandishi wetu aliachana na Ray aliyekuwa akiingia uwanjani na kumfuata Johari lakini hakuwa tayari kusema chochote achilia mbali hata kumsikiliza mwandishi wetu!

TUJIKUMBUSHE
Hivi karibuni gazeti hili liliandika habari yenye kichwa MAINDA: NIMETOA MIMBA YA RAY. Ndani yake Mainda alifunguka mengi ikiwemo kuchanganywa kimapenzi na Ray, yeye na wenzake Johari na Chuchu Hans.
GPL

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ray anaitaji kokombolewa' stupid! Virus tu hapo!!!!

    ReplyDelete
  2. Maskin Johari wa watu na mamilioni yote aliyokupa mkafungua ofisi leo umempiga chini?mbivu una kula na chuchu?mke wa mtu na mama mwenye watoto wawilo?kweli hii ndio Tanga mapumbu shurti kwenye kisosi na maji ya iliki.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndio ujiulize Frank Mtao yalimshinda nini kwa Chuchu mpaka na wewe unataka kuingia kichwakichwa.?Chuchu ni malaya mbwa sio mke hafai.Ray utajutaaaa.Kweli bongo movi ni bongo ngono tu.Maana wasanii wanachukuana wenyewe kwa wenyewe.Duu hatariii

      Delete
  3. Johari si yupo canada jamani

    ReplyDelete
  4. Maskin Johari wa watu na mamilioni yote aliyokupa mkafungua ofisi leo umempiga chini?mbivu una kula na chuchu?mke wa mtu na mama mwenye watoto wawilo?kweli hii ndio Tanga mapumbu shurti kwenye kisosi na maji ya iliki.

    ReplyDelete
  5. Tehtehteh mapenzi nikama bahari ukiogelea huku wenzio wanaogelea kuleee

    ReplyDelete
  6. omba yasikukute

    ReplyDelete
  7. HUYO CHURA HATA SIO MZURI OVYO WOTE

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad