PROF.MUHONGO AMTWANGA NYUNDO NZITO MENGI MPAKA AKAWEWESEKA MDAHALONI

Jana nikikua katika mdahalo wa rasilimali pale ukumbi wa Nkurumah ,waliopewa nafasi ya kuzungumza katika kungamano lile ,Dr Mengi nea alipewa nafasi,yeye katika kuongea alikazia swala la watanzania wazawa wapewe nafasi ya kumiliki vitalu vya gesi ili waweze kunufaika la rasilimali hiyo akitolea mifano nchi kama NIGERIA na ANGOLA wazawa binafsi walivyopewa nafasi ktk nchi zao,,ilivyofika nafasi ya prof Muhongo yeye alitonyesha presentation na twakimu na data zinazoonyesha watanzania wanaomiliki maeneo makubwa ya uwekezaji,,,katika twakimu hiyo Dr Mengi anashika nafasi ya 3 na anaukubwa wa eneo ambalo ukubwa wake mara 3 ya dar es salaam,,laini hamna cha maana anachonufasha watanzania badala ya yeye tu kutajirika binafsi..baada ya data hizo kutolewa Mengi alikua hana amani pale alipokaa na alikua anasimamasimama huku akinyosha mkono apewe nafasi ya kuongea wakati yeye alishaongea,,baada ya mdahalo kuisha dr Mengi,Mnyika,Tundu lisu,na Mtatiro wakajihisi wapo DEFEATED baada ya ile nyundo ya Muhongo,,wakaamua kukusanya watu na kuhaidi kua ule mdahalo utaendelea tena jpili ijayo na utarushwa na ITV ili wajibu ile nyundo ya 

MUHONGO..Muhongo alikua anaongea kwa data wakati wao walikua wanaleta maneno matupu tu ndio maana walioloa JASHO jana..

Prof Muhongo amtwanga nyungo nzito Mengi mpaka akaweweseka...
Tags

Post a Comment

17 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mulongo simuamini ni muongo sana najua ana bifu na tajiri mengi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha ujinga ww mtuakisema ukweli ww unaleta maneno yako ya kilevi.. Kama una Comment nenda kalale..

      Delete
  2. kila siku nawaambia watu akina mengi maneno mengi yasiyo na ukweli wowote. wanataka kupendelewa tu ili hali hawana uwezo wa kufanikisha wanachotaka kwa masilahi ya watanzania. issue ya gas kina mengi hawawezi sababu hawana experience, capital, manpower, positive ambition so the govt should go for investors who are ready to pay 75% loyalty fee not these guys. they better talk foreign investors and buy some shares. hope minister Molongo and president will stand and stick to their decisions on gas exploration in Tz. Politics should not play any part in this Please.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ach kua mjinga ww cc waTz 2naiuza nchi yetu taratibu. wawekezaji wazawa wanaitajika ww unafkiri ln waTz watapata hyo expirienc bila kujaribu. Na viongoz wetu wanataka kutufichaficha 2 ili waendelee kutunyonya..Wazungu wanakuja kuwekeza hapa hawana ata sent tano wanachofanya wanaandika business plan nzur wanaenda kwenye serikal zao na mabeki yao wanapewa funds ss tunabaki hapa tunajisemea hatuna uwezo wakati mali iko kwetu hatutaki kuumiza akil zetu..acha ujinga ww fikiria kabla ya kupost kitu ww..

      Delete
  3. Ule mdahalo nimeuangalia mwanzo mwisho. Prof Muhongo yuko fit sana na alieleza kile kinachotakiwa bila kuficha ficha, ana data za kutosha (facts and figure) sio wanaolalama tu kwa kelele za kisiasa. Big Up sana Muhongo aliwaumbua watu wanaolalama tu na kuficha ukweli. Kwa data zile hakuna mtanzania anaweza kuwekeza kwenye gesi, yuko sahihi na sio kwamba ana kejeli watu. Mtaji wa kuinvest kwenye gesi sio mchezo, ni trillion of money na benk hawawezi kutoa mikopo kama ile coz unaweza kuinvest na ukapata hasara. Wanasiasa wetu wanazungumza bila data zaidi ya porojo tu na maneno mengi, walikuwepo wanaongoza kwa kupiga makele wote akina Lissu, Mtatiro, Mnyika, na wengine kibao ila kwa data zile walitepeta. wamezoea kuwasumbua mawaziri wengine wazembe ila kwa Prof walinywea. Acheni watu wapige kazi na tuappreciate kile wanachojitahidi kufanya, things are not easy like that, wanaolalama wanaweza kupewa nafasi na wakashindwa vile vile. BIG UP PROF, ukitaka kumjua vizuri kamuangalie kwenye CV yake na kama wewe ni msomi na unajua vitu utafunga mdomo.

    ReplyDelete
  4. KUWEKIZA KTK GAS SIO MCHEZO WA KUPATA NA KUKOSA SAFI PRO KWA DATA MENGI NI FIZI AKIONA MFUPA ANATAKA

    ReplyDelete
  5. safi sana prof. umewapa sure hao wamezoea kuonea sababu ya kuongea hawana lolote uliza data hawana wanalojua zaidi ya porojo tu.

    ReplyDelete
  6. Professa Muhongo the man of facts and figures and always speaks the bitter truth hahaha

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mara nyingi watu wanaotoka Mkoa wa Mara sio wanafiki huwa wako straight forward, na Muhogo ni mtoto wa Musoma mjini, please watch out!

      Delete
  7. Umuona eeeh!mudau achana na watto wa kijitaz. Ni wasema ukwel

    ReplyDelete
  8. PROF. Muhongo ni kichwa..Mi nataka DVD yake..Nitaipata wapii...
    ?

    ReplyDelete
  9. Next time Dr.Mengi nae aje na presentation..sio maneno tu..!

    ReplyDelete
  10. Cha kujiuliza..ni lini tutaacha kualika wazungu ili watuchimbie mafuta..? Kulikoni kukaa tukililia udalali wa kuuza vitalu...

    ReplyDelete
    Replies
    1. yaan ww ndo mtu umepost fact inayotakiwa apa..Watanzania wajifunze kupitia nchi kama China na S Korea..they started from zero leo tunagombana tuna sema haiwezekani..

      Delete
  11. Ndio maana tutakuwa maskini hadi mwisho kwasababu ya ushabiki wa kijinga, nani kakwambia kuwa haiwezekani?mbona nchi za wenzetu wameweza ina maana walikuwa na matrioni, jamani hamjajifunza tu kwenye issue nyingine.Dah kweli kizazi cha laana hiki hata baya kwao zuri.kumbukeni kule kusini gesi...

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante sn kk Nchi kama S Korea na China walikua kama sisi sasa badala tutafute namna walivyofanya tunajisemea hatuwezi 2naendelea kunyonywa tu..

      Delete
  12. Hapa Mh Prof: Muhondo kazungumza kweli tupu, kazi ya Uchimbaji mafuta c mchezo Vimillioni vyako 500 uliweka Uswis utashitukia ghafla Vimeyayuka Mh Mengi, kwanza nitakupa hisabu ya haraka haraka Bit moja ya kuchimbia beiyake kama dollar laki4, kuna MUD za kuchanganya bei zake si chini ya dolla$ laki2, kuna tools za MWD, na Tools za DD ( Dirrection Driller) kuzikodi si chini ya Dolla 1 Million, hapa bado kuna Tools nyingine kama company tatu tofauti zinatia vitu vyao yaani kwa haraka haraka si chini ya dollar 3 hadi kisima kianze kutoa mafuta.

    Hapo Bw Yesu asaidie isije kuganda tools ndani ya kisima. hapo ndio kasheshe...maana hisabu ya haraka haraka Millioni 5 us$ zikishindikana kutoka Mwekezaji azilipe bila kupata kitu.

    Vilevile kuna uwezekano wa kukosa Petrol, hapo pia Mamilioni ya dollor zishatoka ndio maana Prof: anakazania kusema kwa muda huu bado WaTanzania tunahitaji Elimu ya kutosha kabla hatujawapa Vitalu vya Gasi.
    Nina Uhakika Dr.Mengi ni Mjanja sana anahitaji vitalu kisha apate wawekezaji wa nje apate asilimia zake katika uchimbaji na hilo analijua ila anatumia mingongo ya WaTanzania kwa Maslahi yake binafsi.
    Kwakuwa anamiliki vyombo vya habari hatosita kujisafisha lakini ukweli utabakia kuwa ukweli kuwa WaTanzania bado uwezo wetu mdogo kwa Muda huu kuweza kuingia katika biashara hii bila kuwashirikisha makampuni makubwa nyenye uwezo hadi siku za Usoni tutakapopata ujuzi zaidi. hatuwezi kuwa kama ng'ombe mwenye kutiwa shemero kina Mengi wakatupelekesha kwa Maslahi yao binafsi.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad