Kundi la watu lasambazwa mikoani kumshughulikia
*Mwenyewe akiri kupata taarifa, Chadema yasema ni ratiba ya kawaida
BAADA ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kumvua madaraka aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwe, chama hicho sasa kimechukua hatua ya kusambaza kundi la watu katika mikoa mbalimbali nchini kwa kazi maalumu ya kushughulika na upepo uliosababishwa na hatua hiyo.
Habari ambazo zimelifikia Rai Jumapili zinaeleza kuwa kundi hilo limepewa maelekezo mahususi kutoka makao makuu ya Chadema kwa ajili ya kwenda kuwashawishi wafuasi na wanachama wake waamini kwamba kijana huyo ni msaliti.
Kwa mujibu wa habari hizo, kundi hilo la watu karibu 15 litazunguka mikoani kupeleka kile inachokiita elimu kuhusu kuvuliwa uongozi kwa Zitto pamoja na Mwanazuoni kutoka katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Kitila Mkumbo litalenga kuwafikia wafuasi wa chama hicho hususani vijana kupitia mabaraza yao ya chama ambao kwao Zitto amekuwa akionekana kama nembo ya mtu anayepigania mabadiliko.
Source: Mtanzania
BAADA YA ZITTO KUVULIWA UONGOZI KUNDI LA WATU LASAMBAZWA MIKOANI KUMCHAFU
0
December 01, 2013
Tags