MUONEKANO WA MABASI YAENDAYO KASI YATAKAYO TUMIKA BONGO [PICHA]


Mabasi ya mwendo kasi 2014 kimara kivukoni.  Picha kwa hisani ya Deo Mutta Mwanatanga
Basi la kwanza la mradi wa mabasi yaendayo kasi limewasili nchini na kuanza kufanya majaribio katika barabara zilizokwisha kamilika huku mengine yakitarajiwa kuwasili mapema mwaka kesho.

Mtendaji mkuu wakala wa mradi wa mabasi yaendayo haraka Bi Asteria lambo amesema basi hilo ni miongoni mwa mabasi madogo yatakayoingia nchini yenye uwezo wa kubeba zaidi ya abiria 40 na makubwa yatabeba abiria zaidi ya 150 na kuwataka wakazi wa jiji la Dar es Salamu kuendelea kuwa na subira na kuwahakikishia mradi huo sio ndoto na adha ya usafiri itapungua mapema mwaka kesho.

Nao baadhi ya wakazi wa jiji walioshuhudia gari hilo wameelezea kufurahishwa na kuanza kuwa na imani na serikali yao ambapo wamesema kama mradi huo utakamilika kwa muda uliopangwa utakuwa faraja sana kutokana na adha kubwa ya usafiri wanayokumbana nayo  huku wakitoa wito kwa mamlaka husika kupanga mikakati ya kupunguza nauli za mabasi hayo pindi yatakapoanza kufanya safari zao.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. PIA muweke vivuko ,vya miguu ,na taa barabarani na semina kuelimisha abiria na wasafiri kwa miguu jinsi ya kutumia barabara na madereva pia,bongo kuvuka bara bara ni shughuli nzito sana,watu na madereva hawajali alama za bara barani,tuwe makini kuokoa maisha ya watu,pia high way ziwe ,hazipishani barabara ,au magari yasikutane uso kwa uso,ilikuepuka ajali barabarani,pia kuwepo na mwendo na alama za mwendo kwenye barabara,tuweke alama nyingi sana za maelezo pia na elimu kwa kupitia TV .AU luninga.

    ReplyDelete
  2. Huu mradi wa mabasi hauwezi kufanikiwa serikali ya ccm ikiwa bado madarakani,wataufisidi na utakyfilia mbali kama ule mradi wao wa mabasi ya wanafunzi ulisimamiwa na uvccm chini ya fisadi william Lukuvi.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad