Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa leo atakuwa na ziara ya siku moja katika Jimbo la Kigoma Kaskazini ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya siku tisa mkoani Kigoma kwa ajili ya kuimarisha chama.
Jana jioni, Dk Slaa alifanya mkutano wa hadhara Mjini Manyovu na kusema kuwa hatishwi na waandamanaji wala vitisho vya kuuawa na kusisitiza kuwa ataendelea na ziara yake kama kawaida hadi Kigoma Mjini.
Awali, akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Malumba wilayani Kasulu, juzi Dk Slaa alisema siyo mara yake ya kwanza kutishwa na kusema analindwa na Mungu.
Licha ya kukabiliwa na upinzani kutoka kwa baadhi ya wanachama wanaodai kupinga hatua ya Kamati Kuu kumvua nyadhifa zake zote, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwe alisema ataendeleza kazi kuimarisha uhai wa chama kama ratiba ilivyopangwa.
Akiwa katika jimbo hilo linaloongozwa na Zitto, Dk Slaa atatembelea Vijiji vya Nyarubanda na Kidahwe na kufanya mikutano ya hadhara inayosubiriwa kwa hamu na wadau wa siasa nchini kutokana na mzozo huo uliokikumba chama hicho kikuu cha upinzani nchini.
Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Kigoma Kaskazini, Ally Kisala alisema maandalizi ya mikutano hiyo yamekamilika na kwamba hakuna hofu yoyote ya kutokea vurugu katika mikutano hiyo.
“Tumedhibiti aina yoyote ya vurugu iliyokusudiwa licha ya kuwapo baadhi ya watu wanaotamani hayo yatokee kwa lengo lao binafsi, sambamba na kunufaisha masilahi ya makundi binafsi, lakini hayatatokea,” alisema.
Juzi, wanachama na wafuasi wa Chadema wanaomuunga mkono Zitto waliandamana kupinga ziara ya Dk Slaa katika jimbo lao kupinga hatua ya kumvua mbunge wao madakara.
“Tunaamini mikutano yote ya kesho (leo Jumanne) itafanyika vizuri na watu watapata ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu wetu (Dk Slaa), na pengine wale wanaopiga kelele na kutaka kuleta mgawanyiko ndani ya chama watapata fursa ya kuujua ukweli wa mambo ndani ya chama.
“Vita yetu si kukigawa chama, bali ni kuhakikisha tunaingia Ikulu katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015,” alisema Kisala.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Zedekia Makunja alisema jeshi lake limejipanga kuhakikisha usalama unakuwapo katika ziara hiyo.
“Tunawajibika kuhakikisha usalama unakuwa vizuri na kila jambo linaendelea kama lilivyopangwa. Mwito wangu kwa viongozi, wanachama na wapenzi wa Chadema ni kuhakikisha wanamaliza tofauti zao mapema ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza, hatupendi kuona askari wetu wakilazimishwa kutumia nguvu kudhibiti hali ya usalama,” alisema Makunja.
mtajibeba shwain nyie labda msubiri 2025 but 2015 patupu
ReplyDeleteUncle samy singida. We msenge na we ndo shwain ya kanguruwe ww, CHADEMA ndo inarekebisha tz, naona unakirus cha ccm nakuapisha tapika kw jina kubwa la CHADEMA
ReplyDeleteFanya kazi yako Dr Slaa, wewe ni mtu muhimu sana ktk taifa hili, tunahitaji mabadiliko tumechoka maisha haya ya dhuluma. Wa tz wenye akili timamu kama waliokupigia kura za urais wanaielewa CHADEMA chama makin na wa tz wataelewa tu hakuna kurudi nyuma. God bless you Dr. Slaa.
ReplyDeleteFanya kazi yako Dr Slaa, wewe ni mtu muhimu sana ktk taifa hili, tunahitaji mabadiliko tumechoka maisha haya ya dhuluma. Wa tz wenye akili timamu kama waliokupigia kura za urais wanaielewa CHADEMA chama makin na wa tz wataelewa tu hakuna kurudi nyuma. God bless you Dr. Slaa.
ReplyDeleteRest In Peace Chadema
DeleteAmeeeen!
Deletehahahaaaa
DeleteChadema bado sana kuongoza nchi, but we love them kwa kuleta challenge na kusababisha uwajibikaji. Gudluck both Chadma and Ccm
ReplyDelete"MKE YA MASAMAKI"
Umenena hapo juu, sio hao wasenge vibaraka wa ccm basi wanashangilia cdm ikiyumba without knowing that kimsingi cdm ndio inaleta uwajibikaji na kuibua ufisadi wa serikali na ccm, bila upinzani tz italiwa mwaka mmoja tu fedha za madini yetu na kodi zitakuwa Swiss Bank.
DeleteMbona povu lakutoka joto hasira,una njaa
ReplyDeletekeep it up tunakutegemea dr.slaa chadema ndan ya jumba 2015
ReplyDeletehizo ni ndoto za abunuasi,hazina tofauti na mtu anaeota ameokota pesa nyingi akaweka ktk beg afa asububui anakimbilia kufungua beg il azione
Deletego ahead dr. ccm wataisoma namba 2015
ReplyDeleteMMESOMEKA! MIMI NI MWANA CCM DAMU~DAMU HIVI RAIS WETU NYERERE SI ATASHINDA TENA 2015? AU MNASEMAJE WADAU?
ReplyDeleteAtashinda tena kwa kishindo
DeleteChadema ndo namba ONE bwana TZ, Mungu ibariki Chadema ishike dola 2015 watanzania warudi kwenye hali zao za kawaida siyo zakinyampala, na mafisadi yachinjiliwe mbali.
ReplyDelete