DR SLAA TUKISHIKA DOLA TUTARUHUSU UTENGENEZAJI WA POMBE YA GONGO KISHERIA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetoa mpya baada ya kueleza kuwa kitakapofanikiwa kushika dola kitaruhu Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) kutengeneza mitambo ya kutengenezea pombe aina ya gongo. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Willbroad Slaa, akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kasulu Vijijini alisema kama gongo itatengenezwa kwa mitambo maalum itaondoa mianya ya rushwa kwa polisi ambao wamekuwa wakiwakamata wanaotengeneza kwa kificho na kuwafanya vitega uchumi vyao.

"Gongo sasa hivi ni haramu sababu inatengenezwa kwa kificho katika mazingira machafu, tukishika dola tutataka SIDO itengeneze mitambo ya kutengeneza gongo ili iwe katika hali ya usafi," alisema.

Mitambo hiyo itakayotengenezwa na SIDO itakapouzwa itaiingizia mapato serikali pia wauzaji wa gongo watafanya biashara hiyo kwa amani tofauti na sasa ambapo wanaifanya kwa kificho na wakikamatwa fedha zote wananufaika polisi.

Dk. Slaa alisema hata suala la kukamata watu wanaotengeneza silaha linapaswa kuangaliwa upya kwani wanaokamatwa wakifanya kazi hiyo wangekuwa wanashikiliwa kwa muda na baadaye wanapelekwa katika kiwanda cha serikali cha kutengenezea silaha ili watuhumiwa hao wapeleke ujuzi huo huko badala ya kuwafunga jela.

Dk. Slaa alisema matatizo yote yanatokana na wasomi kutofikiri namna ya kuisogea nchi mbele kimaendeleo.

"Nchi hii imelala, imechoka sababu waliopewa madaraka wamelala, wamejisahau hawatambui kuwa wamepewa nafasi hizo ili kuwatumikia wananchi," alisema.

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. balaaaaa si dogo haya wanywaj gongo matumaini ya uhuru hayo pia chadema wasisahau kuruhusu pia biashara ya mirungi.....

    ReplyDelete
  2. Pumbavu sanaaaaaa ndo sera hizo!hampati ng'ooooooooooo!nilikua chadema ila kwa hili kura yangu mmeikosa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe ndiyo pumbavu usiyejua maana ya liberty na madhara ya kuwabana raia kwa jambo linalihus liberty yao. Leo hii ni zaidi ya miaka hamsini na gongo bado ni haramu lakini bado inategenzwa. Huoni wenzio Marekani walipoona ugumu wa kubana bangi wakaamua kuiruhu? Binadamu ukizidi kumbana ndipo anapojificha na kufanya kweli, ukisema ruksa, soon utashangaa watu wanaachana nayo.

      Mwananzoi mwa miaka ya sabini serikali ya Nyerere ilitaka kuhalalisha gongo kwa kufungua kiwanda cha konyagi kusudi gongo itengezwe kitaalamu lakini bei ya Konyagi ile ikawa kubwa kuliko uwezo wa watumia gongo. Kwa hiyo wazo la kujenga viwanda vidogo ambavyo vitahakikisha usalama wa wanywaji bila kuingilia liberty yao ni jambo jema kabisa. Fikirieni nje ya boksi.

      Delete
  3. ndio baba mchungaji

    ReplyDelete
  4. Ninaimani hata msuba utauhalalisha uweze kutuongeze pato la nchi. chadema safi sana.

    ReplyDelete
  5. Umri.wote huo.hujawahi kushika dola mchungaji? Vp bangi maana inatumka sana hapa Tz?

    ReplyDelete
  6. hahahaa simba akikosa nyama hula hata nyasi@ aah pipoooz!!

    ReplyDelete
  7. wewe ni dokta wa theolojia siwezi shangaa uwezo wako wa kufikiria ujinga kama huo, umekosa cha kuongea?!

    ReplyDelete
  8. hata biashara ya ngono ataruhus kisa imekatazwa but inafanyka c ndio mchangiaji wa hapo juu

    ReplyDelete
  9. hata biashara ya ngono ataruhus kisa imekatazwa but inafanyka c ndio mchangiaji wa hapo juu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mfano wako uko out kabisa, hebu jaribu tu kuangalia tofauti baina ya gongo na brandy ndipo utakapojua kwa nini kufanyia improvement ya distilling process ya gongo ili iwe salama kwa watumiaji na kuifanya iwe taxable product ni jambo jema sana.

      Delete
  10. Hata sisi malaya mashoga,wasagaji,pusha,haki yetu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad